Ubinafsishaji kiwanda cha UFI: Nani alipiga dili?

Ubinafsishaji kiwanda cha UFI: Nani alipiga dili?

Makao Makuu

Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
7
Reaction score
4
Ndugu zangu,
Kiwanda cha Ubungo Farm Industries (UFI) ni miongoni mwa viwanda vya umma ambavyo ‘vilipitiwa’ na zoezi la ubinafsishaji. Lakini mchakato wote ulilenga katika kukiboresha kiwanda hicho ili kizalishe zana bora za kilimo – kwa uwezo wetu Watanzania, ili kuhakikisha wakulima wanapata zana za kutosha.

Hata hivyo, kuna mambo ambayo yanaleta utata kuhusu namna mchakato wa ubinafsishaji wa kiwanda hicho ulivyofanyika na uzalishaji wa zana hizo ambazo hauendelei kwa sasa.

Badala yake pale kunazalishwa mabomba ya maji, mradi ambao taarifa zinasema uliletwa na vigogo wa serikali katika Awamu ya Tatu ili kuzalisha mabomba kwa ajili ya Mradi Mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria.

Je, nani alihusika na mchakato wa ubinafsishaji wenye utata ambao siyo tu unakwenda kinyume na malengo ya serikali ya kuboresha uzalishaji wa bidhaa husika, lakini pia kuna kila dalili ya udanganyifu, rushwa na ufisadi?

Kwa mukhtadha huo, je, Tanzania ya Magufuli ya Viwanda inaweza kufanikiwa?

Pengine uelewa wangu ni mdogo, lakini inawezekana humu ndani wapo wanaolifahamu jambo hili vizuri, hivyo nakaribisha mjadala.
 
Ngoja n'a mimi nisubirie majibu maana ningependa sana kufahamu.....Ila nna wasi wasi uzi huu wale jamaa zetu wakaupita kwA mbali..

OVA
 
Wakati huohuo wajanja waliishawishi serikali ikadhamini mkopo wa mabilioni kwa UFI kutoka benki ya Exim China. pesa hizi pamoja na riba zitalipwa na nani. Kutoka kuzalisha pembejeo hadi mabomba. Na Bora Shoe je, kutoka kutengeneza viatu hadi mipira ya baiskeli, HAKI ya MUNGU nchi hii! na Mbeya Textiles kutoka kuzalisha nguo hadi kuwa maghala ya kuhifadhi tumbaku. Hakuna haja ya kujenga viwanda vipya, tufufue hivi vilivyopo.
 
Mambo haya yanachanganya. Tunaambiwa UFI iliingia ubia - na nani na kwa makubaliano gani? Zoezi la ubinafsishaji kweli lilikuwa na manufaa? Rais alikuwa Ben Mkapa, Waziri Mkuu alikuwa Fred Sumaye, Waziri wa Fedha alikuwa Simon Mbilinyi, baadaye Mramba na Daniel Yona, Katibu Mkuu Hazina alikuwa Gray Mgonja, Waziri wa Maji alikuwa Edo Lowassa. Nazungumzia katika kipindi hicho cha mwaka 1995 hadi 2005 wakati zoezi la ubinafsishaji lilipopamba moto.
UFI ilikuwa miongoni mwa mashirika 32 yaliyoingia ubia, lakini ubia wa UFI ulikuwa mwaka 1996! Lakini nani aliyehusika? Nani aliingia mkataba wa ubia wa mashirika haya particularly UFI?
Orodha ya mashirika 32 yaliyoingia katika ubia ni hii hapa chini, pengine itakuwa vyema kama tukiyachambua hapa.

MASHIRIKA YALIYOINGIZWA KATIKA UBIA

1. Shamba la Mkonge – Msowero (TSA) – 1992

2. Shamba la Mkonge – Rudewa (TSA) – 1992

3. Shamba la Mkonge – Toronto (TSA) – 1993

4. Shamba la Mkonge – Mnazi (TSA) – 1993

5. Shamba la Mkonge – Mkumbara (TSA) – 1993

6. Shamba la Mkonge – Ndungu (TSA) – 1993

7. Kampuni ya Bia Tanzania (Dar & Arusha Plants) – 1993

8. TBL Farms Ltd – 1993

9. Tanzania Maltings Ltd – 1993

10. Mwanza Breweries – 1993

11. Mwanza Tanneries – 1993

12. Tanzania Tanneries – Moshi – 1993

13. Morogoro Tanneries – Morogoro – 1993

14. TANELEC – 1995

15. New Africa Hotel – 1993

16. ALAF – 1995 (but outright sold)

17. Morogoro Shoes – 1993

18. Morogoro Canvas – 1994

19. Tanga Cement Company – 1995

20. Imara Wood Products Company – 1993 investor pulled out and was re-advertised.

21. Buckreef Gold Mining Co. – 1993

22. Williamson Diamonds – 1994

23. New Almasi Company – 1994

24. MOPROCO – 1995

25. Pugu Kaolin Mines Ltd – 1993 but investor pulled out

26. Tanzania Cigarettes Company – 1995

27. Lupa Gold Mines – 1994

28. Light Source Manufactures – 1994

29. Urafiki – 1996

30. State Travel Services – 1996

31. UFI – 1996

32. NABICO – 1996
 
Back
Top Bottom