Uber yasitisha rasmi huduma zake Tanzania kuanzia Januari 30, 2026

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Kampuni ya teknolojia ya kimataifa, Uber, imetangaza kusitisha rasmi huduma zake nchini Tanzania kuanzia Januari 30, 2026.

Uber, ambayo inajulikana kwa kutoa huduma za kuunganisha abiria wanaohitaji usafiri na madereva kupitia programu ya simu, pamoja na huduma za uwasilishaji wa chakula (Uber Eats) na usafirishaji wa mizigo, imeeleza kuwa uamuzi huo umefikia mwisho wa safari yake katika soko la Tanzania.

Katika taarifa yake, kampuni hiyo imetoa shukrani kwa wateja na wadau wote waliokuwa wakitumia na kuunga mkono huduma zake, ikisisitiza kuwa imekuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya safari za kila siku za Watanzania, hasa katika Jiji la Dar es Salaam, kwa kutoa huduma za usafiri wa uhakika, salama na kwa gharama nafuu.

"Tuna habari ngumu. Kuanzia leo, 30 Jan 2026, huduma za Uber hazitapatikana tena Tanzania.

Tunajua kuwa hili linaweza kuwa jambo la kukatisha tamaa, na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaoeweza kujitokeza. Tangu tulipozindua huduma zetu Dar es Salaam, imekuwa heshima kubwa kwetu kuwa sehemu ya safari zenu za kila siku, tukikusaidia kusafiri kwa usalama, uhakika na kwa bei nafuu.

1769927432271.png

Sura hii inafika mwisho, lakini shukrani zetu kwako zinabaki. Asante kwa kukaribisha App ya Uber maishani mwenu na kuwa sehemu ya historia yetu Tanzania.

Kwa shukrani za dhati,

Timu ya Uber"
1769927358247.png
 
Hawa jamaa si kuna mwaka waliondoka/Walikuwa banned ulingoni, kwa Tz tukabaki na Bolt (Zamani Taxify), wameamua kuondoka moja kwa moja?
 
Kampuni ya teknolojia ya kimataifa, Uber, imetangaza kusitisha rasmi huduma zake nchini Tanzania kuanzia Januari 30, 2026.

Uber, ambayo inajulikana kwa kutoa huduma za kuunganisha abiria wanaohitaji usafiri na madereva kupitia programu ya simu, pamoja na huduma za uwasilishaji wa chakula (Uber Eats) na usafirishaji wa mizigo, imeeleza kuwa uamuzi huo umefikia mwisho wa safari yake katika soko la Tanzania.

Katika taarifa yake, kampuni hiyo imetoa shukrani kwa wateja na wadau wote waliokuwa wakitumia na kuunga mkono huduma zake, ikisisitiza kuwa imekuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya safari za kila siku za Watanzania, hasa katika Jiji la Dar es Salaam, kwa kutoa huduma za usafiri wa uhakika, salama na kwa gharama nafuu.

"Tuna habari ngumu. Kuanzia leo, 30 Jan 2026, huduma za Uber hazitapatikana tena Tanzania.

Tunajua kuwa hili linaweza kuwa jambo la kukatisha tamaa, na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaoeweza kujitokeza. Tangu tulipozindua huduma zetu Dar es Salaam, imekuwa heshima kubwa kwetu kuwa sehemu ya safari zenu za kila siku, tukikusaidia kusafiri kwa usalama, uhakika na kwa bei nafuu.

Sura hii inafika mwisho, lakini shukrani zetu kwako zinabaki. Asante kwa kukaribisha App ya Uber maishani mwenu na kuwa sehemu ya historia yetu Tanzania.

Kwa shukrani za dhati,

Timu ya Uber"
Hata hivo wamejitahidi sana. Miako yote hyo.... Kufanya kazi na wasukuma ni kazi ngumu sana.
 
SISI tulioajiriwa tukale wapi Sasa?huyu Samia anaua biashara.bora ajiuzulu
 
SISI tulioajiriwa tukale wapi Sasa?huyu Samia anauza biashara.bora ajiuzulu
wewe tahira tulia. Uber wameondoka wenyewe badala ya kupigwa KO na Bolt.
Samia hajawahi kuua biashara ya mtu au kampuni yoyote.
Jiwe mungu wenu ndiye aliyeua maelfu ya biashara enzi zake.
Huo ushetani wenu wa kila jambo Samia Samia mtakuja kuingizwa ndizi makalioni
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Wameyaaga mashindano, bolt wazidi kuchanja mbuga
 
Naona Bolt sasa ndio itanufaika zaidi,ni muda sasa naona kama Uber ilishapoteza mvuto
Walivyositisha tu kipindi kile ushawishi ukapungua.
Hata hivyo katika ushindani wao na Bolt walikuwa wameshapigwa knock out, bolt bei ilikuwa pungufu ukilinganisha na Uber.

Changamoto ya bolt ilikuwa ni kutokuwa na coverage area kubwa.
 
wewe tahira tulia. Uber wameondoka wenyewe badala ya kupigwa KO na Bolt.
Samia hajawahi kuua biashara ya mtu au kampuni yoyote.
Jiwe mungu wenu ndiye aliyeua maelfu ya biashara enzi zake.
Huo ushetani wenu wa kila jambo Samia Samia mtakuja kuingizwa ndizi makalioni
Bora jiwe kaua biashara , Samuya Watanganyika wenzetu elfu 10 na Wakenya 5.
 
Back
Top Bottom