Ielewe biashara ya (online taxi) Uber, bolt nk
HESABU.
Kuna aina 2 za marejesho ya hesabu.
1.Rejesho la hesabu linaloambatana na mkataba wa makabidhiano ya gari, hapa moja kwa moja baada ya kipindi cha muda fulani gari hubaki kwa dereva.
Kipengele hiki cha mkataba sehemu kubwa ya service kitamhusu dereva na akimshirikisha mmiliki wa chombo kuhusu matengenezo ya chombo ili kutoathiri maelewano ya hesabu mf gari ipo gereji hlf mmiliki anataka pesa (hesabu) itakuwa siyo busara.
Ktk kipengele hiki hesabu hutegemea ubora wa chombo (gari) pamoja na kipindi cha muda wa mkataba.
Mf gari ikiwa mpya muda wake wa mkataba hatakama ukiwa mfupi basi hesabu yake huenda ikawa kubwa kutokana na maelewano ya mmiliki na dereva .mfano huweza kuwa kwa miaka 2 na nusu ( 2.5) kwa Tsh 170k -180k kwa wiki.
2. Rejesho la hesabu lisilohusisha mkataba wa makabidhiano ya moja kwa moja, Hapa mmiliki wa chombo atalazimika kupokea kiasi walichokubaliana na dereva wake na ktk kipengele hiki service ya kila hitilafu kwenye gari itamhusu mmiliki wa chombo (Boss) na muda wowote mmiliki wa chombo anaweza akasitisha ukomo wa kazi na dereva wake. Ni ktk kipengele hiki wamiliki wengi wa magari huingia mkenge ama kutoelewana na madereva kutokana na historia na simulizisi zisizo na uhalisia wa hizi kazi hizi wakiamini pesa ni nyingi ambapo ni tofauti na uhalisia
na madereva wengi huingia wakiwa na uhitaji wa kazi tu kuliko kifikilia changamoto za kazi hiyo hii ni kutokana na njaa na kama tujuavyo njaa huweza kuwa kengere ya kumuingiza mtu tumwani hulazimika kukubali kila kitu ilimradi tu tumbo lipate chochote. Mwanzo ataanza na nguvu za ajabu hadi kukesha mfululizo kufikia kipindi kuhatarisha maisha kama tujuavyo huwezi kuendesha muda wote utachoka tu hasa hatar ya usingizi basi wiki kadhaa atamuaminisha Boss na boss ataamini dereva wake yupo vizur cha ajabu ni muda mfupi tu gari lipo service kila muda maana hakuna uangalizi thabiti popote gari litapelekwa njia hata iwe mbovu vipi litapelekwa tu. Baada ya mwezi mambo huwa mabaya Boss haamini kinachomtokea na kuanza kuilani biashara hii.
Hesabu ambayo itamfanya dereva amudu ktk kipengele hiki ni kuanzia 120k-140k kwa wiki.
NB. Nimefanya kazi hii sasa ni kuelekea mwaka wa 3 huu. Wamiliki wa magari niliofanyanao kazi ni wawili tu namshukulu mmoja aliyehamia Dodoma huyu amefanya historia kwenye uwanja huu huyu wa pili nafikir tumeachana kwa amani tangu nianzenae kazi wiki gereji wiki road nafikir passo yake hapo awali haikupata mtu sahihi au inachangiwa na kuchoka kwake sasa tumeiuza kwa bei ya pkipik.
Mmiliki aliye tayar tafadhali naomba tufanyekazi nina weledi na kuthamini mali ya mtu pamoja na utii wa kazi.
##0789702863.