security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
YALEYALE?
(Dkt. Muhammed Seif Khatib)
Iliaminika kuwa mwezi Januari, tarehe 12, siku ya Jumapili mwaka 1964, ingekuwa mwisho wa kilele cha uhasama, ubaguzi wa kikabila, chuki za kitikadi za kichama na dharau kisiwani Zanzibar.
Harakati za kutokomeza uoza huo uliowaathiri Waswahili wa Zanzibar tokea dunia ianze uliasisiwa, kuendeshwa na kufanikishwa na Chama cha Afro-Shirazi.
Chama hiki kilichukua miaka saba kupigania usawa na haki na kuondoa ubaguzi kwa wenyeji wa Zanzibar. Mapinduzi ya mwaka 1964 yangekuwa ndiyo suluhisho. Hali haipo hivyo.
Siyo watu wote wa Zanzibar waliofurahia Mapinduzi hayo. Wapo walionyanganywa “ukuu” “ulua” na “utukufu”. Wapo waliopenda kuendelea kuwamiliki watwana na wajakazi ili kuwatumikia.
Wapo waliopenda kuendelea kuwepo ukabila na ubaguzi wa rangi ili tofauti hiyo iwape heshima wachache wao. Wapo waliotaka wamiliki njia kuu za uchumi kama mashamba na ardhi ili waishi kwa jasho la wengine.
Mapinduzi ya mwaka 1964 yamepiga dafrau dhuluma na uonevu huo. Lakini haikuwa rahisi kufanikisha Mapinduzi. Afro-Shirazi ilipambana vikali sana na chama cha siasa cha Hizbu (ZNP) ambacho kilikuwa kinaongozwa na viongozi vibwanyenye na waliokuwa wanalinda masilahi yao.
Hawa waligubikwa na siasa za uhafidhina. Viongozi hawa wa Hizbu ili kuwavunja moyo wanachama wa Afro-Shirazi katika kudai haki na usawa, vituko kadha walifanyiwa wanachama wa Afro-Shiraz.
Kila uchaguzi ukiwadia Waswahili wengi walikuwa wanakipigia kura chama chao cha Afro-Shirazi. Vituko hivyo wakati huo wa harakati za kudai uhuru vilivyofanywa na viongozi na wanachama wa Hizbu dhidi ya wanachama wa Afro-Shirazi vilikuwa vingi.
Vyote hivi vililenga kuwakomoa wanachama ili wasikipigie kura chama cha Afro-Shirazi. Wanachama wa Afro-Shirazi walifukuzwa katika mashamba ambao wengi wao wamiliki wake walikuwa Waarabu.
Maeneo ambayo wanachama waliokuwa wanauza mazao yao pia walifukuzwa. Maduka ambayo yalikuwa ya wanachama wa Hizbu waliwanyima wanachama wa Afro-Shirazi kuwauzia bidhaa.
Magari yaliokuwa wakimikiwa na wanachama Hizbu waliwanyima kuwapa huduma za usafiri wanachama wa Afro-Shirazi. Maiti ya Afro-Shirazi wakigomewa kuzikwa na wanachama wa Hizbu.
Askari polisi wenye asili ya bara ya Tanganyika walitolewa kazini. Hata hivyo, Afro-Shirazi juu yaunyonge wao wakachangisha pesa na kununua shamba la Kilembero huko Unguja na wanachama wao waliofukuzwa katika mashamba ya Waarabu walipewa ili waishi humo na walime.
Eneo la Kariakoo Mjini Unguja lilinunuliwa na Afro-Shirazi wakati huo na kuwapeleka wanachama wao katika soko hilo ili wafanye biashara. Afro-Shirazi ikafungua maduka yake kwa ajili ya wanachama wake kupata huduma.
Hasama hizi na uonevu huo dhidi ya Afro-Shirazi ukawaleta matokeo mabaya ya fujo na mauaji mwezi June 1961. Uhasama huo ukasababisha watu 68 kuwawa, kati yao 3 Waafrika na 64 Waarabu.
Watu walioumizwa sana 51, Waafrika 39 Waarabu. Waliokamatwa 144, kati yao 137 Waafrika na 9 Waarabu. Haya yalitokea Unguja. Serikali ya Kiingereza ikaleta askari kutoka Kenya, Bataliani ya 5 na 6 ya King’s African Rifles. Haikuwa dawa. Fujo za June 1961 zikatunga mimba ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.
Leo imepita miaka hamsini na mbili baada ya Mapinduzi. Tunayona yale yale yaliyotokea Zanzibar, sasa yanatokea tena huko kisiwani Pemba. Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, warithi wa Afro-Shirazi Party, wanafanyiwa maovu na madhila yale yale na CUF.
Tofauti ni kuwa badala ya kufanywa na chama cha Hizbu leo hujuma zinafanywa na Chama cha Wananchi. Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wananyanyaswa na kubaguliwa kwa maelekezo ya viongozi wa Chama cha Wananchi.
Nyumba za wanachama wa Chama Cha Mapinduzi zinatiwa moto na kubomolewa. Mazao yao yanafyekwa na mengine mashamba yao yatiwa moto. Wananyimwa usafiri katika magari yao.
Wanagomewa kuuziwa vyakula katika maduka na magulio. Na haya yote yamepata baraka kutoka kwa viongozi wao wa Chama cha Wananchi.
Hivi wanachama wachache wa Chama Cha Mapinduzi, waliopo Pemba, kosa lao nini? Kutumia haki yao ya kikatiba kukipigia kura chama chao? Wanachama hawa wachache ndiyo waliowazuia wao wengi wasiende kupiga kura?
Hivi yale maeneo ambayo Chama Cha Mapinduzi wapo wengi na wanachama wao kidogo nao walipe kisasi kwa wanachama wao? Nyumba za wanachama wao zitiwe moto? Mashamba yatiwe moto?
Maduka na masoko yao yagomewe? Hivi wanachama wa Chama cha Wananchi kutoka Pemba kwa hili wanaashiria nini? Wanataka kuzuke fujo kama zile zatarehe 1, Juni 1961 au wanachochea mapinduzi mengine yatokee? Wanachama wa Chama cha Wananchi ninawashauri waigomee serekali ya SMZ lakini wasitese Wapemba wenzao.
Wagomee kwa kutokwenda skuli, kutotumia hospital, kutokwenda kazini na kutotumia maji, umeme na barabara za serekali ya Zanzibar. Kwa kufanya hivyo wataikomoa serekali wasioichagua!