Ubabe ukizoeleka utazaa usugu wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubabe ukizoeleka utazaa usugu wa Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchonga, Dec 31, 2010.

 1. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ubabe umetumika kuzuia chaguzi za mameya katika halmashauri kadhaa nchini au kulazimisha chaguzi katika manispaa nyingine kinyume na taratibu.

  Tumeshuhudia wabunge wakipigwa hadharani, wananchi wakipigwa mabomu na wakurugenzi wakishinikizwa kupinda taratibu.
  Tumeshuhudia wanafunzi wakiandamana kwa amani na kupigwa mabomu.
  Tumeshuhudia vyama vya siasa vikinyimwa haki ya kukutana katika nchi huru.
  Tumeshuhudia vyombo vya habari vikitishwa au kubaguliwa katika kupewa habari.
  Tumeshuhudia wakuu wa vyombo vya habari, tena vya umma, wakifukuzwa kama mbwa koko kwa sababu eti tu, wamewapa wapinzani nafasi ya kuonekana! Kwa ubabe, wapinzani wanafanywa kuwa ni wabaya kuliko mafisadi, wabaka uchumi wa nchi, na hata magaidi.

  Nani ataiambia hii serikali ikasikiliza?
  Wana habari wamesema hawakusikilizwa;
  Wana harakati wakapuuzwa;
  Vyama vya upinzani vikaitwa majina mabaya badala ya kusikiliza hoja zake;
  Wazee wenye hekima waliobakia wakasema wakatukanwa;
  Viongozi wa dini wakasema na kuzushiwa kuwa wana udini;
  Wahisani wakadokeza na kuambiwa wafanye lililowaleta;
  Bunge likajaribu, spika akaundiwa zengwe na kupozwa kwa cheo feki;
  Nani mwingine aliyebaki?

  Watanzania wakiota sugu kwa ubabe huu, suluhu itapatikana kwa gharama kubwa. Nasema hivi kwa sababu, hata polisi wanaotumika kuwaumiza ndugu zao kwa mabomu, pia wao wana mahitaji. Siku polisi wakigoma, nani atawapiga mabomu?
   
Loading...