Uangamivu wa haki korogwe chuo cha ualimu

Uangamivu wa haki korogwe chuo cha ualimu

falsafa hai

New Member
Joined
Feb 19, 2013
Posts
4
Reaction score
0
KWELI VITA DHIDI YA WAFUJAJI, WABADHIRIFU ITAISHA KWA NAMNA HII?​
Ni swali linaloweza kuonekana jepesi lakini kwa wanaoyashuhudia maumivu ya kusaka haki na kusema ukweli majibu ni tofauti kabisa.Nathubutu kusema na kukiri kabisa kuwa vita hii ni ngumu sana kwa kuwa wezi, wadhulumaji, wafujaji na wahujumu haki za raia wamejikita na kuwa na mizizi sugu sana haswa katika serikali.Kila atakaye jaribu kupigania haki au kuhoji kitu chenye maslahi ya wakubwa huyo ajue hali yake ni mbaya. Aidha kama ni mfanyakazi kibarua chake kitakuwa mashakani, kama ni mfanya biashara basi asubiri zengwe la kila aina litakalopigwa ili kumfilisi kama sio kumchomekea kesi isiyomhusu.Baada ya kufanya uchunguzi wangu mdogo nimejikuta nikishuhudia kwa macho yangu mwenyewe jinsi wakufunzi wa chuo cha ualimu Korogwe walivyonyongwa haki zao bila kificho kwa sababu tu, walihoji mambo magumu yaliyoonekana kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa watawala. Lakini pia cha kunisikitisha kabisa ni kwamba hata baada ya serikali kuja na kushuhudia kuwa yaliyokuwa yakihojiwa ni mambo ya kweli naya wazi bado nayo aidha kwa kukusudia au kwa kupotoshwa na vigogo wachache wenye maslahi yao na taasisi fujaji ikachukua maamuzi mazito na magumu ya kuwaadhibu wale wote waliojitolea hata kwa maisha yao kuleta mabadiliko ya kimfumo badala ya kuwapongeza na kuwahakikishia usalama wao.Najiuliza hivi haya matangazo kwenye Radio, Television na magazeti hivi kumbe ni uwongo wa kuwatafutia wananchi majeneza? Kwa nini basi wanaohamasisha wananchi kuhoji wasitoe na namna au jinsi watakavyowasaidia pindi wakikutwa na dhahama ya mikono ya wabadhirifu? Kumbe ndio maana wanavijiji wameamua kuwa kimya ili kuacha kila mtu na LWAKE. Hapana kuhoji hata bajeti ya kijiji!!!!!!!.Hapa kwetu chuo cha ualimu Korogwe leo kimyakimya wabadhirifu, wezi, wafujaji wameshinda kwa kuwa kamwe hakuna anayethubutu kuhoji hata mimi siwezi kuhoji lakini nadhani hata hao waliohamishwa huko walikopelekwa wenyeji wao watakuwa na funzo kuwa kumbe hawa ndio waliokuwa wanahoji na sisi tukijidai tu kunyanyua midomo yatatukuta zaidi ya haya. Hakika huu ni uangamibvu wa haki na kifo cha utawala bora.Hali hii imejitokeza hapa chuo cha ualimu Korogwe mnamo tarehe 07/03/2013 baada tu ya wakufunzi kumi waliokuwa wakionekana kuuliza vitu ambavyo viligusa maslahi ya wakubwa au kuonekana kuwa wana misimamo katika kutetea hoja zao kupewa barua za uhamisho usiokuwa wa kawaida.Wakufunzi hawa walisaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ya kimfumo katika taasisi baada ya kufichua ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka na madeni sugu ya ndani, lakini jambo walilofanyiwa hakika linarudisha nyuma kama si kuuwa kabisa misingi ya utawala bora. Barua zao zilionesha kuwa ni uhamisho wa kawaida ili tu serikali kujificha nyuma ya mkono wa wahalifu. Hakika wanaichafua serikali na chama tawala kwa maslahi yao kwa kisingizio eti serikali ni wao. Tazama miongoni mwa waliohamishwa wapo wenye miaka miwili, mmoja na nusu, minne, sita na wawili wenye umri mkubwa kidogo. Kubwa zaidi walipewa barua zao chini ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Hivi kweli hili linahitaji miwani kuhoji uhalali wa uhamisho huu? Lakini pia kati ya hawa hayupo hata mmoja aliyekuwa anashutumiwa kwa lolote au kuwa mmiliki japo wa mradi mmoja uliofujwa. Taswira hii ni mbaya kabisa na pia haitoi muonekano wa kweli wa taifa hili kutaka kuwa la haki na kuwa na utawala bora. Sasa tunaweza kuamini kumbe viongozi wetu wakisimama jukwaani husema yaliyo midomoni mwao na si yaliyo mioyoni mwao, lakini pia wakiwa ofisini hutenda yaliyo mioyoni mwao na si yaliyo midomoni mwao. Kumbe hawana nia njema nasisi zaidi tu ya kuwachombeza wananchi wawe daraja lao la kupandia hasa baada ya kuwang’oa wote watakaozuia maslahi yao dhalimu.Kwa yeyote mwenye kutaka kupata taarifa za uthibitisho anaweza kufika Korogwe na kuwahoji watu chinichini nini kilijiri kwa kuwa sote tumejawa na hofu ya kuhojiwa maana hatuna hakika ni nani anayetuhoji na mwisho utakuaje au unaweza kuwasiliana mwenyewe na wahuska waliohamishwa kwenye vyuo vifuatavyo. Bustani, Kinampanda, Marangu, Monduli na mhonda.Hakika kama yupo mpenda haki na mwanaharakati yeyote anayetamani kuona haki na utawala bora kwenye nchi hii vikitamalaki ninawasihi mfuatilie jambo hili mkajionee wenyewe ukiukwaji wa haki za binaadamu na utawala bora. Pasi kuwasaidia watu hawa na kuujuza umma nini kimefichika hakika kama taifa na harakati zetu zote tutakuwa tumekubali wahujumu haki na wauwaji wa utawala bora wajione wako sahihi sana.Ndugu, hata ninapoandika ujumbe huu kwa umma ninahofu kubwa juu ya mustakabali wangu iwapo tu nitajulikana.Nawasilisha.Mdau wa haki Korogwe.:shock:
 
Back
Top Bottom