Huu ndio uamuzi wa kesi ya Tanesco v. Dowans ambao ulitolewa na Jaji Dk Fauz Twaib nadhani utasaidia kuondoa mkanganyiko ambao ulijitokeza mara baada ya kutolewa. Waandishi na magazeti mengine yaliulewa visivyo na wakasema kuwa Tanesco imebwagwa mahakamani. Kile ambacho Jaji amesema ni kuwa Tanesco wana haki ya kukata rufaa Mahakama ya Rufaa moja kwa moja bila kibali au ruhusa ya Mahakama Kuu. Hivyo pingamizi la Dowans juu ya maombi hayo limetupiliwa mbali hali kadhalika maombi ya Tanesco ya kuomba ruhusa hayakuwa na maana kwani wana haki hiyo. View attachment TANESCO V DOWANS (RG 20 Feb 2012(3).pdf
Mbona kilichoandikiwa hakikuwa kigumu hivyo kueleweka? Uzuri ni kuwa issue iliyopo sasa ni kujiandaa kutengeneza appeal kwani siyo tu inawezza kugusa sheria bali pia facts of the case. I hope wapambanaji tumewapa zana za kutosha to do both.