UAMUZI WA BUSARA

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
UAMUZI WA BUSARA

(Dr. Muhammed Seif Khatib)


Wanadamu wanaamini kuwa dunia imeumbwa na Mwenyenzi Mungu. Ingawa mwanadamu ndiye anayeijenga lakini mwanadamu huyo huyo kwa kutumia silaha alizozitengeneza mwenyewe huibomoa dunia anayoijenga ikawa haitamaniki. Ili dunia iwe na maendeleo endelevu, amani, haki na usawa; vyama vya siasa huundwa kwa kazi hiyo. Tanzania ni sehemu ya dunia, inahitaji nayo ipige hatua ya maendeleo na iwe katika ustawi. Vyama vya siasa vimeota kwetu kama uyoga. Ni vyama vinavyohitajika kuleta ushindani wa kisiasa kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu. Nami ninacho chama changu, chama Chama Cha Mapinduzi chenye uongozi wenye busara na hekima ambao hufanya kazi kwa pamoja ili hatimaye kiendelee kushika dola. Wanachama wa chama changu huridhika na kuamini juu ya dhamira, lengo na mtazamo mmoja. Dhamira na malengo yetu ndiyo inayoshawishi fikira za wengi na jamii pana ili iendelee kutuunga mkono. Kazi hii imefanyika katika chama changu. Miaka kumi ya uongozi wa Rais Kikwete na Uenyekiti, imemalizika. Yeye aliwekwa madarakani katika Urais na chama changu. Miaka kumi ya uongozi wake umemalizika. Ni mengi aliyoyafanya ya kimaendeleo. Yeye akiwa Rais hakuwa “mtakatifu”. Na wasaidizi wake hawakuwa “malaika”. Wote ni binadamu ambao hawakosi upungufu. Uchaguzi Mkuu umemalizika, Chama changu kimeshinda tena. Tutakuwa madarakani kwa miaka mitano ya kwanza. Tumeshinda kwa sababu tulijiandaa kushinda. Tukiwa chama cha siasa, tumeteua wagombea turufu kama maeneo tofauti kwa nchi nzima. Uteuzi wetu makini na sifa mwanana za wagombea wetu zimetuvusha katika mchakato wa ngazi ya Rais, Wabunge wengi, Wawakilishi wote na Madiwani wengi. Bila ya shaka waliotaka nafasi hizi ndani ya chama ni wengi lakini walioteuliwa ni kidogo. Kazi hii ya kuteua wagombea bulibuli imerahisisha wapiga kura kuwa na uamuzi wa busara. Kazi ya pili iliyotupa ushindi tuliyoifanya ni ya kuwanadi hao wagombea kwa mipango mizuri. Tulisambaza mabango, vipeperushi, kutumia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara, mikutano ya faragha na kufanya kampeni nyumba kwa nyumba. Jambo la tatu, tulinadi sera za chama chetu kuonesha azma ya kuendelea kutenzua kero za watu ikiwemo rushwa, ufisadi, kutowajibika na ujenzi wa miundo mbinu. Jambo la nne lililoleta ushindi kwa chama changu, ni utaratibu mzuri wa kujipanga katika kampeni. Nani ende wapi. Nani aseme nini na kwa nini? Matumizi bora ya aina ya viongozi na makada katika mazingira maalum kwa madhumuni maalum. Ushindi unapatikana kwa kuvijua vyama vya upinzani nguvu zao na udhaifu wao. Wagombea wao, dhambi zao, uzuri na udhaifu wao? Kutambua mikakati yao na mipango yao. Kubainisha kwa kebehi na dharau sera na zao ni kazi tuliyoifanya. Kulinganisha na kulinganua sifa bainifu za wagombea wetu kwa kuwapa hadhi na heshima wakati huo huo kuonesha dosari zao. Tulionesha kwa mfano kuwa wao hawawezi kufua dafu mbele ya wagombea wa chama chetu. Kura hazipo mjini na vijiweni lazima makundi ya kampeni yawafate watu popote pale walipo. Sisi tumewafata popote pale walipo. Tumeyafata makundi yao kirika, kijinsia, kaamali na kikazi. Ushindi wa chama changu siyo wa juu ya sahani mezani. Mikakati ilisukwa ikasukika. Maandalizi yalipangwa yakapangika. Ilikuwa hakuna kulala. Si usiku si mchana. Si mvua si jua. Hatimaye serekali zote mbili ya Zanzibar na ya Muungano zimewekwa mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi. Bila ya shaka chama changu kinajiandaa kuwashukuru wale waliotuunga mkono. Chama kinatarajia wale wote walioshinda katika nafasi mbalimbali watafanya wajibu wao katika kuwaondolea kero wananchi waliwapigia kura. Utekelezaji mzuri wa ilani ya chama chetu ni faraja kwa wanachama na wapenzi wa chama chetu. Hatukufanya kosa kuwapigia kura wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Ulikuwa uamuzi wa busara Tunasubiri matunda ya uamuzi wetu.
 
security guard

Mkuu bandiko lako sikulisoma kwa sababu linachosha ukiliangalia tu. Pengine maudhui yake yana maana lakini mimi sitayajua.

Hivi huyu Dokta alieandika hili bandiko hajui uwepo wa aya (paragraphs) na vichwa vidogo (sub-headings) vya habari?

Tuoneeni huruma sisi wasomaji. Tafadhali lifanyie marekebisho bandiko lako halafu ulirudishe hapa. Sio shurti.
 
Back
Top Bottom