Uamuzi sahihi kufunga machimbo ya mchanga dsm! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamuzi sahihi kufunga machimbo ya mchanga dsm!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mp Kalix2, Aug 1, 2012.

 1. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,211
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]

  Wana JF mliokaribu na maeneo hayo mtujuze wamiliki wa machimbo yanayotarajiwa kunufaika na utaratibu huu ,isije tokea kuna mikono ya Vigogo.Kwani uharaka wa jambo hili unaleta walakini katika uamuzi huu wa Kamishna.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kamishna alitakiwa kuwa tangazia wote wanaochimba Mchanga kwenye maeneo yasiyokuwa rasmi kwa kuwataka kupeleka maombi ili kurasmisha/kuhalalisha maeneo husika kama yatakidhi Kanuni iliyowekwa .[/FONT]
  [FONT=&amp]Hii vile vile ilitakiwa pia iambatane na vigezo vinavyotakiwa au Kanuni inayotakiwa kutimizwa na Mashimo husika na huku pia kuangalia madhara ya kiuchumi kwa wahusika katika kusimamisha shughuli ya kiuchumi ndani ya muda mfupi uliotolewa.[/FONT]
  [FONT=&amp] Madhara ya maamuzi haya ni kama ifuatavyo;[/FONT][FONT=&amp]Shughuli nyingi za kimaendeleo hasa ujenzi kwa watu wa vipato vidogo utasimama au kukwama kabisa kwani gharama ya mali ghafi muhimu kama Mchanga itapande kwa zaidi ya asilimia mia nne (400%) hivyo kushindwa kuimudu .[/FONT]
  [FONT=&amp]Pili zoezi hili itasababisha mafundi na vibarua wengi kukosa kazi.Isitoshe maeneo mengi DSM vijana wengi wamekopeshwa pesa na taasisi za fedha au wameajiriwa na wanaendesha miradi midogo ya kufyatua matofali ili waweze kujikimu wao na familia zao na kwa namna ya kipekee wataathirika na zoezi hili la wizara ya Nishati na Madini.[/FONT]

  [FONT=&amp]Uamuzi huu haukuzingatia madhara ya kiuchumi kwani miradi mingi inayoendelea ya kiujenzi;wajenzi walikwisha piga tathmini ya gharama za awali kwa uwepo wa Upatikanaji wa Mchanga kwa bei iliyokuwapo kabla ya tangazo hii ambayo itafanya nyongeza ya kati ya 300-400% kama mradi uko maeneo ya city kidogo kwa wilaya zote za Mkoa wa DSM.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa maoni yangu uamuzi huu una walakini.[/FONT]

  source;

  [FONT=&amp]Magayane alisema katika kutekeleza agizo hilo, kuanzia Agosti 1 mwaka huu ofisi hiyo itafanya ukaguzi kabambe kwenye maeneo yote yanayochimbwa mchanga ili kuwabaini wakiukaji wa sheria.[/FONT]


  [FONT=&amp]Alitanabisha kuwa zoezi hilo litasimamiwa kwa pamoja na ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki, Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini, Jeshi la Polisi na Maofisa kutoka Halmashauri za Wilaya husika. [/FONT]

  [FONT=&amp]muandishi: JOHN BUKUKU tarehe: 7/10/2012 [/FONT]
   
Loading...