Uamuzi mgumu CCM katika kamati kuu leo

Uamuzi mgumu CCM katika kamati kuu leo

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,699
Reaction score
9,591
Dodoma/Dar. Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM inakutana leo mchana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete huku ikitarajiwa kufanya uamuzi mgumu wa mchakato wa Katiba.

Kikao hicho kinaketi mara ya pili katika muda mfupi, baada ya hivi karibuni kukaa jijini Dar es Salaam na kueleza kuridhishwa na mchakato huo.

Hata hivyo, safari hii kikao hicho kinaketi kukiwa na maswali lukuki ambayo hayajapata majibu: Je, Bunge la Katiba liendelee au livunjwe? Je, lisitishwe kwa muda kupisha maridhiano au la? Je, kuna umuhimu wa maridhiano? Kuna ulazima wa kuwapo Ukawa bungeni?

Akizungumzia kikao hicho, mtaalamu wa sayansi ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema jambo kubwa litakalojadiliwa katika kikao hicho ni kauli tofauti zilizotolewa na wananchi kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya.

"Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba ameshauri yafanyike maridhiano kwanza na wapo wanaCCM waliomuunga mkono. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema naye ameonyesha wasiwasi wake, Ukawa na Jukwaa la Katiba Tanzania nao wamesema yao. Nadhani kuna jambo CCM wameliona na wanataka kuliweka sawa," alisema Dk Makulilo.

Aliongeza, "Kujua nini wataamua ni ngumu lakini kutokana na hali ilivyo kwa sasa ni wazi kuwa wanakutana kuona nini kifanyike."

Kwa upande wake Bashiru Ali alisema, "Tangu mwanzo mchakato wa Katiba haukuwa katika ilani ya CCM, sasa unaweza kujiuliza wanakwenda kujadili nini wakati hata katika mikakati yao ya miaka 10 na 20 ijayo hakuna mpango wa kuandika Katiba."

Habari zilizozagaa mjini Dodoma zinadai kikao hicho pia kinaweza kupendekeza kuwashughulikia wanachama wake waliotoa kauli zinazopingana na msimamo wa chama hicho.

Miongoni mwa waliotoa kauli zinazopingana na chama hicho ni Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba kutokana na matamshi yake ya kuhoji uhalali wa vikao vya Bunge la Katiba kuendelea bila uhakika wa akidi.

Mbali na Mwigulu pia wabunge kadhaa wa CCM akiwamo, Esther Bulaya (Viti Maalumu), Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ridhiwani Kikwete (Chalinze) nao wamekaririwa kwa nyakati tofauti wakitoa misimamo inayokinzana na chama chao kuhusu uhalali wa Bunge la Katiba kuendelea bila kuwapo maridhiano na Ukawa.

Hata hivyo, habari nyingine zinasema iwapo kuna mpango huo, Mwigulu anaweza kuondolewa kutokana na utaratibu wa chama hicho kuwaondoa kwenye sekretarieti wajumbe wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa serikalini.

Chanzo chetu kinasema ikiwa hilo litatokea kwa sababu ya Mwigulu kuteuliwa Naibu Waziri wa Fedha, basi mpango huo hautamwacha nyuma Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje, Dk AshaRose Migiro ambaye pia hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na gazeti hili jana, alikanusha kuwapo kwa mpango wa kumwondoa Nchemba katika nafasi yake na kwamba kikatiba kikao chenye uwezo huo ni Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

"Hizo taarifa ni za uongo kabisa, kikao kweli kitakutana kesho (leo) saa 8:00 mchana chini ya Mwenyekiti Rais Kikwete na ajenda ni moja tu, ambayo ni mchakato wa Katiba. Kikao maalumu huwa na ajenda moja maalumu, hakuna mengineyo wala nini," alisema Nnauye.

Alisema CC itapokea taarifa kuhusu mchakato wa Katiba unavyokwenda itakayotolewa na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk Asha-Rose Migiro na baadaye kujadiliwa na wajumbe.

Habari ambazo zililifikia gazeti hili jana zinasema hatua dhidi ya kiongozi huyo wa juu katika chama zinatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni "kuwaudhi makada wa CCM" kutokana na kauli yake hiyo.

Nchemba jana alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kupitia ujumbe mfupi wa maandishi, "Sina taarifa za kung'olewa, nimealikwa kwenye kikao kama NKM (Naibu Katibu Mkuu wa CCM)."

Hata hivyo, ikiwa CCM itafanya uamuzi wa kumwondoa Nchemba, huenda ukapokewa kwa hisia tofauti na umma wa Watanzania ikizingatiwa kwamba pamoja na kutoa kauli zinazokinzana na msimamo wa chama chake, amekuwa akiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali.

CC ya CCM ambayo hivi karibuni ilibariki Bunge la Katiba kuendelea hadi lifike mwisho, inakutana leo kwa dharura wakati mchakato wa Katiba ukidaiwa kutokuwa na uhalali wa kisiasa kutokana na kususiwa na idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge Maalumu ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kutokana na kutokuwapo Ukawa ndani ya Bunge, kuna hofu kwamba Bunge linaloendelea na vikao vyake Dodoma litakosa theluthi mbili ya kura kutoka Zanzibar, hivyo kutopatikana Katiba Mpya.

Kutokana na hali hiyo, Mwigulu amekaririwa mara kadhaa akisema hakukuwa na haja ya Bunge hilo kuendelea na vikao bila kuwa na uhakika wa kutimiza akidi, vinginevyo itakuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma, na wananchi hawatawaelewa.

Kutokana na mazingira hayo, vyanzo vya habari vinasema CCM lazima ifanye uamuzi mgumu wa ama kuziba masikio isisikie kelele za makundi yanayotaka Bunge lisitishwe hivyo iamue liendelee, au igeuke jiwe kwa kulisitisha na kukiuka uamuzi wake wa awali.

Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa kwamba viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakifanya vikao vya siri na wale wa vyama vya upinzani kwa lengo la kufanyia marekebisho Katiba ya sasa ili kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi mkuu mwakani iwapo Katiba mpya itakwama.

Miongoni mwa maeneo ambayo vyama hivyo viliyaainisha katika vikao vyake vya siri ni pamoja na kuwapo kwa Tume Huru ya Uchaguzi, matokeo ya kura za Rais kuhojiwa mahakamani na mgombea binafsi.

Chanzo: Mwananchi
 




Hata hivyo, ikiwa CCM itafanya uamuzi wa kumwondoa
Nchemba, huenda ukapokewa kwa hisia tofauti na umma wa Watanzania ikizingatiwa kwamba pamoja na kutoa kauli zinazokinzana na msimamo wa chama chake, amekuwa akiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali.



Chanzo: Mwananchi

Hapo kwenye red utapingwa sana.
Mtu anayetumia vifo kama mtaji wa kisiasa unasema anaungwa mkono na wananchi ?
 
Mkuu Martinez hata mimi nimesoma mara tatu tatu! nikagundua huyu kanjanja alikuwa na lake Jambo si bure
 
Hata kama UKAWA wangepewa nafasi na uhuru kamili wa kujadili Katiba, nina uhakika kuwa hakutakuwa na uelewano, na hakuna litakalofanikiwa.

LABDA IDADI YA WABUNGE INGEKUWA NI 10 TU NA (SIO WANASIASA) NADHANI KUNGEKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA SANA.
 
CCM watakuwa na wazimu zaid kama hawatashuulikia mpasuko na badala yake kuanza kushuulikia watu wenye nia ya Maridhiano.,
 
CCM watakuwa na wazimu zaid kama hawatashuulikia mpasuko na badala yake kuanza kushuulikia watu wenye nia ya Maridhiano.,
Najaribu kuimagine, hivi ikitokea kweli, CCM wamefunuliwa maono, na Mungu na kufanya maamuzi hayo magumu ya kuliahirisha bunge hilo la katiba.

Hivi akina Samuel Sitta, Stephen Wassira, William Lukuvi na 'vuvuzela' wao Nape Nnauye, sijui sura zao watazifichia wapi?

Kwa kuwa hao ndiyo walikuwa 'frontline' kuwatukana na kuwakashifu ukawa, kuwa kutoka kwao kwenye bunge la katiba, si lolote na si chochote, kwa maana ya kwamba idadi ya wabunge wa ukawa ni ndogo mno, kiasi ambacho haiwezi kwa namna yoyote, kutowezesha upatikanaji wa 2/3 ya wabunge wa Tanganyika na wa Zanzibar, ili kuwezesha kupitisha Rasimu yao ya magamba.

Kwa bahati nzuri sana kwa Mwigulu Nchemba, yeye alishajichongea Safina yake, kama enzi za Nuhu, na kuwakana wenzie, kuwa piga ua, bunge hilo haliwezi kupata theluthi 2 inayotakiwa, kupitisha katiba hiyo.

Hivi sasa Mwigulu Nchemba, anaendelea 'kusepa' na safina yake akiwa na maccm wenzake wachache, akina James Lembeli, Kangi Lugora, Esther Bulaya na Deo Filikunjombe, but the rest of CCM entourage, wamei-miss safina ya Mwigulu Nchemba, hivi sasa wanaendelea kuyabwia, maji ya mafuriko yaliyowakumba, na kama ilivyotokea kwenye enzi za Nuhu, kizazi hicho cha wabunge wa magamba, kinaelekea kuteketezwa chote, kama adhabu ya Mungu, kutokana na kiburi chao cha kupitiliza, cha 'kuisigina' Rasimu ya Tume ya Warioba, iliyokuwa na maoni ya wananchi!!
 
Huu mkutano wa majambazzi wa nchi hii haujaisha tu watuambie ujambazi wao unahamia wapi maana huu wa BMK wameona utawatokea puani.
 
Kinachoendelea dodoma ni uchakachuaji wa mabilioni ya shilingi ya walipa kodi bila tija!
 
Binafsi sitarajii chochote cha ajabu zaidi yawao kwenda kulipana posho tu nakuahidi wasiyoweza kutekeleza kama kuvuana magamba na ahadi lukuki,ingekuwa CC ya Cdm ningekaa mkao wakusikia mtikisiko.Nawashauri Ccm wajifunze kutoka CDM
 
Hata kama UKAWA wangepewa nafasi na uhuru kamili wa kujadili Katiba, nina uhakika kuwa hakutakuwa na uelewano, na hakuna litakalofanikiwa.

LABDA IDADI YA WABUNGE INGEKUWA NI 10 TU NA (SIO WANASIASA) NADHANI KUNGEKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA SANA.

hata ukawa wangebaki pekee yao wangetoka nje ya bunge.kumbuka kikako cha awali tundu lisu alipinga hija aliyiwasilisha mwenyewe wakati akiwakilisha rasimu ya uendeshaji vikao vya bunge
 
Siku hizi cc ya ccm haina mshindo wala msisimko kama ambavyo inapokaa cc ya chadema, badala yake ccm wanaenda kupanga mikakati ya kuimaliza cdm kwa kuwabambikia kesi ya mauaji ya chacha wangwe, mama zito, mwangosi,n.k
 
Walisha kosa mvuto hata hiyo cc ikikaa watanzania Swazis nayo na hii ni kwa sababu ya dhuluma na dharau kwa watanzania
 
Hapo kwenye red utapingwa sana.
Mtu anayetumia vifo kama mtaji wa kisiasa unasema anaungwa mkono na wananchi ?




Hizi siasa za kijinga zimetoka wapi?
Hamuoni zitakigharimu hili taifa siku si nyingi?
Mwigulu Nchemba amemuua nani? Hebu tutajie huyo aliyeuawa n Nchemba? Hizi siasa za maji ya chooni zimeanza kurudi tena ndani ya Chadema na inakipukutisha chama na bado hatuoni atari ya kupakaziana.
 
Kwahiyo CCM ndiyo yenye mamlaka ya kuamua BMK kuendelea au kutoendelea??
 
Back
Top Bottom