Uamuzi huu wa Magufuli ni faida au hasara kwa Taifa?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,315
152,113
Ukikatisha mkataba wa mtumishi bila shaka ni lazima umlipe haki zake zote kwa kukatisha mkataba na hapo hapo ni lazima uajiri mwingine kuchukua nafasi yake.

Sasa kwa mfano,mtumishi ana mkataba wa miaka 5 au 3 alafu unaamua kuukatisha mkataba wake wakati amebakiza miaka 3 au 2 kukamilisha mkataba wake. Hapa bila shaka itabidi umlipe haki zake zote kutegemeana na muda uliobaki kwa kuzingatia mashariti ya mkataba na sheria za utumishi wa umma na hapo hapo inakubidi uajiri mwingine ndani ya muda huo.

Sasa kipi bora,usubiri hiyo miaka 3 au 2 iishe au usitishe mkataba wa mtumi kisha umlipe na hapo hapo uajiri mwingine ambae itabidi nae umlipe mshahara wa hiyo miaka 3 au 2 iliyokuwa imebaki?

Je,hii si itakuwa ni gharama mara mbili ya kulipa watu wawili tofauti (mwajiriwa mpya na yule uliemsitishia mkataba) kwa kazi moja ndani ya muda ule ule (miaka 3 au miwili iliyokuwa imebaki)?
 
CHADEMA imekuwa mtetezi wa wala rushwa na mafisadi.

Inasikitisha sana.
Kama serikali ya chama chenu iliruhusu watu kulipana mishahara ya kifisadi kwa mikataba iliyohalalishwa na wenye dhamana alafu leo mkaikatisha mikataba hiyo na kisha mkatumia hela za walipa kodi kuwalipa kwa kukatisha mikataba hiyo?Je,hapa hamuoni kuwa nyie ndio mafisadi na wazembe?
 
umejitoa Fahamu mpaka umesahau sheria za kazi? Meli ya uvuvi leo hii Serikali inalipa mabilioni, nyumba za Serikali zilienda kwa bei chee viongozi wanapangishiwa nyumba kwa bei kubwa, jaribu kuwa unakumbuka nyuma kisha tumia Lugha ya Taifa Kingereza ni Ulimbukeni.
We jichanganye tu,magufuli is a person who never take heed to stupidity opinions like these.
 
Ukikatisha mkataba wa mtumishi bila shaka ni lazima umlipe haki zake zote kwa kukatisha mkataba na hapo hapo ni lazima uajiri mwingine kuchukua nafasi yake.

Sasa kwa mfano,mtumishi ana mkataba wa miaka 5 au 3 alafu unaamua kuukatisha mkataba wake wakati amebakiza miaka 3 au 2 kukamilisha mkataba wake. Hapa bila shaka itabidi umlipe haki zake zote kutegemeana na muda uliobaki kwa kuzingatia mashariti ya mkataba na sheria za utumishi wa umma na hapo hapo inakubidi uajiri mwingine ndani ya muda huo.

Sasa kipi bora,usubiri hiyo miaka 3 au 2 iishe au usitishe mkataba wa mtumi kisha umlipe na hapo hapo uajiri mwingine ambae itabidi nae umlipe mshahara wa hiyo miaka 3 au 2 iliyokuwa imebaki?

Je,hii si itakuwa ni gharama mara mbili ya kulipa watu wawili tofauti (mwajiriwa mpya na yule uliemsitishia mkataba) kwa kazi moja ndani ya muda ule ule (miaka 3 au miwili iliyokuwa imebaki)?
Hivi mtu aliyeleta hasara ya B.400 ,bomba la mafuta..halipimwi...ukimwacha miaka miwili amalizie mkataba tafsiri yake nini?...,pumbavu kabisa...wakiachwa mnasema wanalindwa..wakichukuliwa hatua,wanaonewa....ndio maana wengine wanaondolewa madaraka...wanasoma magazeti kwa miaka miwili iliyobaki then...anaondoka...usimwachie mbowe ashike akili zako utapotea.
 
CHADEMA imekuwa mtetezi wa wala rushwa na mafisadi.

Inasikitisha sana.
Chadema ndiyo unawatetea Escrow? Lugumi?
CHADEMA imekuwa mtetezi wa wala rushwa na mafisadi.

Inasikitisha sana.
chadema ndiyo inawatetea escrow, UDA, NIDA, NSSF, ATC, bomba la Gesi, mikataba ya madini, Chenji ya rada na ile ya bunge la katiba, kivuko feki, mabehewa chakavu? Umekariri Akili za Nape nini?
 
Hivi mtu aliyeleta hasara ya B.400 ,bomba la mafuta..halipimwi...ukimwacha miaka miwili amalizie mkataba tafsiri yake nini?...,pumbavu kabisa...wakiachwa mnasema wanalindwa..wakichukuliwa hatua,wanaonewa....ndio maana wengine wanaondolewa madaraka...wanasoma magazeti kwa miaka miwili iliyobaki then...anaondoka...usimwachie mbowe ashike akili zako utapotea.
Acha kutoka nje ya mada.Hoja iliyotolewa ni kuwa wana mishahara mikubwa na si mafisadi kama unavyozusha hapa!
 
Kabla ya mkataba wa ajira kuvunjwa nadhani kuna team inayochunguza hasara zitakazopatikana kwa kuuvunja mkataba dhidi ya hasara itakayopatikana kwa kuendelea kufanya kazi na huyo muajiriwa.Sidhani kama hawaangalii haya mambo.
 
Hivi mtu aliyeleta hasara ya B.400 ,bomba la mafuta..halipimwi...ukimwacha miaka miwili amalizie mkataba tafsiri yake nini?...,pumbavu kabisa...wakiachwa mnasema wanalindwa..wakichukuliwa hatua,wanaonewa....ndio maana wengine wanaondolewa madaraka...wanasoma magazeti kwa miaka miwili iliyobaki then...anaondoka...usimwachie mbowe ashike akili zako utapotea.
wewe mbona umeshikiliwa akili na akina January waliopiga pesa za ccm bilion 1.7 na sasa kuwatapeli wataliano kwa kivuli cha ikulu huku akishiriki kumsaidia Lugumi na kitwanga wasitumbuliwe jipu, Maliza vimeo Hivi vya Kivuko kibovu, mabehewa feki, Uuzaji nyumba za Serikali na Madili yenu mengi ndipo uje na hizo Akili za kukariri kila mnalolishwa na Nape na January.
 
Kabla ya mkataba wa ajira kuvunjwa nadhani kuna team inayochunguza hasara zitakazopatikana kwa kuuvunja mkataba dhidi ya hasara itakayopatikana kwa kuendelea kufanya kazi na huyo muajiriwa.Sidhani kama hawaangalii haya mambo.
Kesi ya meli, kesi ya kuvunja kituo cha mafuta kule mwanza ziliishia vipi?
 
Ukikatisha mkataba wa mtumishi bila shaka ni lazima umlipe haki zake zote kwa kukatisha mkataba na hapo hapo ni lazima uajiri mwingine kuchukua nafasi yake.

Sasa kwa mfano,mtumishi ana mkataba wa miaka 5 au 3 alafu unaamua kuukatisha mkataba wake wakati amebakiza miaka 3 au 2 kukamilisha mkataba wake. Hapa bila shaka itabidi umlipe haki zake zote kutegemeana na muda uliobaki kwa kuzingatia mashariti ya mkataba na sheria za utumishi wa umma na hapo hapo inakubidi uajiri mwingine ndani ya muda huo.

Sasa kipi bora,usubiri hiyo miaka 3 au 2 iishe au usitishe mkataba wa mtumi kisha umlipe na hapo hapo uajiri mwingine ambae itabidi nae umlipe mshahara wa hiyo miaka 3 au 2 iliyokuwa imebaki?

Je,hii si itakuwa ni gharama mara mbili ya kulipa watu wawili tofauti (mwajiriwa mpya na yule uliemsitishia mkataba) kwa kazi moja ndani ya muda ule ule (miaka 3 au miwili iliyokuwa imebaki)?

Sheria ya ajira na mahusiano ya kazini kuanzia kifungu namba 35 hadi 44 inazungumzia yafuatayo kuhusiana na swala la kusitishwa kwa ajira ya mfanyakazi:

35. Masharti ya sehemu ndogo hii hayatatumika kwa mfanyakazi mwenye pungufu ya miezi sita ya ajira na mwajiri yuleyule, ikiwa ni katika mkataba mmoja au zaidi.

36. Kwa lengo la Sehemu hii Ndogo -
(a) ''kusitishwa kwa ajira” kunajumuisha-
(i) kusitishwa ajira kwa haki chini ya sheria za kawaida zisizoandikwa;
(ii) kuacha kazi kwa mfanyakazi kwa sababu kuendelea kwake na kazi kunakuwa kugumu kwa sababu ya mwajiri;
(iii) kushindwa kuongeza mkataba kwa kipindi maalumu katika masharti yaleyale au yanayofanana nayo kama kulikuwa na matarajio ya kawaida ya kuongeza;
(iv) kushindwa kumruhusu mfanyakazi kurudi kazini baada ya kuchukua likizo ya uzazi inayotolewa chini ya Sheria hii au likizo nyingine ya uzazi iliyokubaliwa; na
(v) kushindwa kumwajiri tena mfanyakazi kama mwajiri amesitisha ajira ya wafanyakazi wengi kwa
sababu ileile au inayofanana na hiyo na ameamua kuwaajiri tena mmoja au zaidi kati yao;
(b) ''sitishwa ajira” ina maana inayofanana na “kusitishwa kwa ajira”.

Kuachishwa kusiko kwa haki
37.
-(1) Itakuwa si halali kisheria kwa mwajiri kusitisha ajira ya mfanyakazi bila ya kufuata haki.

(2) Kusitishwa kwa ajira na mwajiri si kwa haki ikiwa mwajiri atashindwa kuthibitisha -
(a) kwamba sababu za kusitisha ni halali;
(b) kwamba sababu ni sababu ya haki -
(i) inayohusiana na mwenendo wa mfanyakazi, uwezo au kuendana; au
(ii) inayohusiana na mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri; na
(c) kwamba ajira ilisitishwa kwa kufuata taratibu za haki.

(3) Haitakuwa sababu ya haki kusitisha ajira ya mfanyakazi-
(a) kwa sababu kwamba-
(i) amefichua taarifa ambazo mfanyakazi ana haki au anatakiwa kufichua kwa mtu mwingine chini ya Sheria hii au Sheria nyingine;
(ii) ameshindwa au amekataa kufanya kitu chochote ambacho mwajiri hawezi kisheria kuruhusu au kumtaka mfanyakazi kufanya;
(iii) ametekeleza haki yoyote iliyotolewa kwa makubaliano, Sheria hii au sheria yoyote nyingine;
(iv) amejiunga au alijiunga kwenye chama chochote cha wafanyakazi; au
(v) ameshiriki katika kazi halali za chama cha wafanyakazi, ikujumuisha mgomo halali;
(b) kwa sababu-
(i) zinahusiana na ujauzito;
(ii) zinahusiana na ulemavu; na
(iii) ambazo ni za kibaguzi chini ya sheria hii.

(4) Katika kuamua kama usitishwaji na mwajiri ni wa haki, mwajiri, msuluhishi au Mahakama ya Kazi italazimika kutilia maanani kanuni za utendaji mzuri zilizotangazwa chini ya kifungu cha 99

(5) Hatua ya kinidhamu ya aina ya adhabu, kuachishwa au kufukuzwa haitachukuliwa kwa mfanyakazi ambaye anashitakiwa kwa kosa la jinai mpaka maamuzi ya mwisho ya mahakama yatakapotolewa na rufaa inayohusiana na hiyo.

Kuachishwa kunakotokana na mahitaji ya uendeshaji
38
.-(1) Kusitishwa kokote kwa ajili ya uendeshaji (kupunguza wafanyakazi), mwajiri atatakiwa kufuata kanuni zifuatazo, hii ni kusema atatakiwa -
(a) kutoa notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi mara tu baada ya kuona hivyo;
(b) kutoa taarifa zote muhimu zinazohusiana na upunguzaji wa wafanyakazi uliokusudiwa kwa ajili ya mashauriano mazuri;
(c) kushauriana kabla ya kupunguza wafanyakazi -
(i) sababu za kupunguza wafanyakazi kunakokusudiwa;
(ii) hatua zozote za kuzuia au kupunguza upunguzaji wa wafanyakazi;
(iii) utaratibu wa kuchagua wafanyakazi wa kupunguzwa;
(iv) muda wa kupunguza wafanyakazi; na
(v) kiinua mgongo kinachohusiana na kupunguza wafanyakazi;
(d) kutoa notisi, kutoa taarifa na kushauriana kwa mujibu wa kifungu hiki kidogo na-
(i) chama chochote cha wafanyakazi kinachotambulika kwa mujibu wa kifungu cha 67.
(ii) chama chochote cha wafanyakazi kilichosajiliwa chenye wanachama katika sehemu ya kazi ambacho hakiwakilishwi na chama cha wafanyakazi
kinachotambuliwa;
(iii) wafanyakazi ambao hawawakilishwi na chama cha
wafanyakazi kinachotambulika au kilichosajiliwa.

(2) Kama wakati wa mashauriano yanayofanyika kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande husika suala litatakiwa kupelekwa kwenye usuluhishi chini ya sehemu ya VIII ya Sheria hii.

(3) Ikiwa katika upunguzwaji wowote, sababu ya kuachishwa ni kukataa kwa mfanyakazi kukubali masharti na mazingira mapya ya ajira, mwajiri atatakiwa kuiridhisha Mahakama ya Kazi kuwa njia iliyotumika ya kufungia nje ili kusababisha mabadiliko ya masharti na mazingira ya kazi haikuwa sahihi katika mazingira hayo.

Uthibitisho wa mwenendo wa kuachishwa kusiko kwa haki
39.
Katika mwenendo wowote unaohusiana na usitishwaji wa ajira usiokuwa wa haki, mwajiri atatakiwa kuthibitisha kuwa usitishwaji huo ulikuwa wa haki.

Nafuu kwa kuachishwa kusiko kwa haki
40.
-(1) Ikiwa msuluhishi au Mahakama ya Kazi imeamua kuwa usitishwaji wa ajira ulikuwa si wa haki, msuluhishi au Mahakama inaweza kumwamuru mwajiri -
(a) kumrudisha mfanyakazi kuanzia tarehe ambayo mfanyakazi aliachishwa kazi bila kupoteza mshahara wakati ambao mfanyakazi hakuwepo kazini kwa sababu za kuachishwa kusiko kwa haki; au
(b) kumwajiri upya mfanyakazi katika masharti ambayo msuluhishi au Mahakama inaweza kuamua; au
(c) kumlipa mfanyakazi fidia ya mishahara ya miezi isiyopungua kumi na miwili.

(2) Amri ya fidia inayotolewa chini ya kifungu hiki itakuwa ni nyongeza, na si badala ya kiasi chochote ambacho mfanyakazi ana haki nacho kwa mujibu wa sheria yoyote au makubaliano.

(3) Ikiwa amri ya kurudishwa kazini au ya kuajiriwa upya imetolewa na msuluhishi au mahakama na mwajiri akaamua kutomrudisha kazini au kumwajiri upya mfanyakazi, mwajiri atatakiwa kulipa fidia ya mishahara ya miezi kumi na miwili ikiwa ni nyongeza ya mishahara na faida nyingine kuanzia tarehe ya kuachishwa kazi kusiko kwa haki mpaka tarehe ya malipo ya mwisho.

Sababu nyingine za kuachishwa
41
.-(1) Kama mkataba wa ajira unaweza kusitishwa kwa notisi, muda wa notisi hautakuwa pungufu ya-
(a) siku saba, kama notisi inatolewa katika mwezi wa kwanza wa ajira; na
(b) baada ya hapo-
(i) siku nne, kama mfanyakazi ameajiriwa kwa msingi wa siku au wiki; au
(ii) siku 28, kama mfanyakazi ameajiriwa kwa msingi wa mwezi.

(2) Mkataba unaweza kutoa muda wa notisi ambao ni mrefu kuliko unaotakiwa katika kifungu kidogo cha (1) ikiwa, muda wa notisi uliokubaliwa ni sawa kwa wote; mwajiri na mfanyakazi.

(3) Notisi ya kusitisha ajira itakuwa kwenye maandishi, ikieleza -
(a) sababu za kusitisha; na
(b) tarehe ambayo notisi inatolewa.

(4) Notisi ya kusitisha ajira haitakiwi kutolewa -
(a) wakati wa kipindi cha likizo iliyochukuliwa chini ya Sheria hii; au
(b) kuenda sambamba na muda wowote huo wa likizo.

(5) Badala ya kumpa notisi mfanyakazi, mwajiri anaweza kumlipa mfanyakazi mshahara ambao mfanyakazi angepokea kama mfanyakazi angefanya kazi wakati wa notisi.

(6) Kama mfanyakazi atakataa kufanya kazi wakati wa kipindi cha notisi, mwajiri anaweza kukata kutoka kwenye fedha yoyote inayodaiwa na mfanyakazi huyo wakati wa kusitishwa ajira, kiasi ambacho kingedaiwa na mfanyakazi kama mfanyakazi huyo angefanya kazi wakati wa kipindi cha notisi.

(7) Hakuna kitu katika kifungu hiki kitaathiri haki ya-
(a) mfanyakazi kupinga uhalali wa kusitishwa kwa ajira chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote;
(b) mwajiri au mfanyakazi anaweza kusitisha ajira ajira bila notisi kwa sababu yoyote inayotambuliwa na sheria.

Malipo ya kiinua mgongo
42.-
(1) Kwa malengo ya kifungu hiki, “kiinua mgongo” maana
yake kiasi cha mshahara wa angalau siku 7 kwa kila mwaka ulioisha wa
utumishi wa moja kwa moja na huyo mwajiri mpaka kwa kiwango cha juu
cha miaka kumi.

(2) Mwajiri atatakiwa kumlipa kiinua mgongo wakati wa kusitisha ajira ikiwa-
(a) mfanyakazi amemaliza miezi 12 ya utumishi wa moja kwa moja na mwajiri; na
(b) kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (3), mwajiri amesitisha ajira.

(3) Masharti ya kifungu kidogo cha (2) hayatatumika-
(a) katika usitishwaji kwa sababu za utendaji mbovu;
(b) kwa mfanyakazi ambaye amechishwa kwa sababu za uwezo, kutoendana au mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri lakini ambaye atakataa bila sababu za msingi kukubali ajira mbadala na mwajiri huyo au mwajiri mwingine.

(4) Malipo ya kiinua mgongo chini ya kifungu hiki hayataathiri haki nyingine za mfanyakazi za kulipwa kiasi kingine kilipwacho chini ya Sheria hii au sheria nyingine zilizoandikwa

Kusafirishwa kwenda mahali pa kuajiriwa
43.
-(1) Kama mkataba wa mfanyakazi umesitishwa katika mahali ambapo sipo mfanyakazi alipoajiriwa, mwajiri atatakiwa aidha,
(a) kumsafirisha mfanyakazi na vitu vyake kwenda sehemu aliyoajiriwa;
(b) kulipa gharama za usafirishaji wa mfanyakazi kwenda mahali alipoajiriwa; au
(c) kumlipa mfanyakazi posho ya usafiri kwenda sehemu aliyoajiriwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na posho ya gharama kwa kila siku wakati wa kipindi, kama kipo, kati ya tarehe ya kusitishwa kwa mkataba na tarehe ya kumsafirisha mfanyakazi na familia yake kwenye sehemu aliyoajiriwa.

(2) Posho iliyotajwa chini ya kifungu kidogo cha (1)(c) itakuwa sawasawa na angalau nauli ya basi kwenda kituo cha basi kilicho karibu na sehemu ya kuajiriwa.

(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “kuajiri” maana yake kumshawishi mfanyakazi kwa kuajiriwa na mwajiri au wakala wa mwajiri.

Malipo katika kuachishwa na cheti cha ajira
44.
-(1) Katika kusitishwa kwa ajira, mwajiri atatakiwa kumlipa mfanyakazi-
(a) ujira wowote wa kazi iliyofanyika kabla ya kuachishwa kazi;
(b) likizo yoyote ya mwaka inayodaiwa na mfanyakazi chini ya kifungu cha 31 kwa likizo ambayo mfanyakazi hajachukua;
(c) malipo yoyote ya likizo ya mwaka iliyoiva wakati wa mzunguko wa likizo usiokamilika ukiamuliwa kwa kufuata kifungu cha 31 (1);
(d) malipo yoyote ya notisi chini ya kifungu cha 41(5); na
(e) malipo yoyote ya kiinua mgongo yanayodaiwa chini ya kifungu cha 42;
(f) posho yoyote ya usafiri ambayo inaweza kuwa inadaiwa chini ya kifungu cha 43.

(2) Baada ya kuachishwa, mwajiri atatakiwa kumpa mfanyakazi cheti maalumu cha utumishi.
 
Kesi ya meli, kesi ya kuvunja kituo cha mafuta kule mwanza ziliishia vipi?
Mkuu kama sikosei mleta uzi anazungumzia mikataba ya watumishi wa umma na nimechangia kwa muktadha huohuo.Haya mambo ya mikataba ya biashara sina uzoefu nayo.
 
Damage ya Mtu mzembe atakayoifanya kwa miaka miwili ni kubwa mara elfu ya mshahara utakaomlipa kwa Miaka hiyo miwili.
Sidhani Kama kuna sheria inayosema Kama MTU Ana mkataba Wa miaka 5 then ukakatisha mkataba wake baada ya miaka 3 basi unapashwa kuendelea kumlipa mshahara kwa kipindi kilichobaki cha mkataba. Kwa ufahamu wangu MTU Kama huyo anastahili kupata compensation let say equivalent ya mshahara Wa wiki moja kwa kila mwezi uliobaki kwenye mkataba lakini Si mshahara kamili.

Tiba
 
Back
Top Bottom