Uamsho+Ukristo+Muungano

MndemeF

Member
Jan 15, 2011
35
5
Nimekaa kimya kwa muda mrefu nikiwaza kilichotokea hivi majuzi huko kisiwani Unguja. Najiuliza hivi Wakristo wa visiwani wana makosa gani hadi kuchomewa nyumba zao huko ZNZ? Yaani muungano na Ukristo vina mahusiano gani? Lakini yote kwa yote nahisi hizi ni kero za muungano. Wazee wa Uamsho tafadhalini waelezeni wafuasi wenu yakuwa muungano na ukristo ni vitu viwili tofauti kabisa. Yaani wapeni elimu ili watoe maoni yao kwenye katika katiba mpya. Kwa maoni yangu muungano ni mzuri ila muundo wa muungano uangaliwe upya. Yaani kuwe na serikali tatu yaani JAMHURI YA MUUNGANO, SERIKALI YA ZNZ NA SERIKALI YA TANGANYIKA. Baada ya hapo kuwe na rais wa muungano ambaye atachaguliwa kutoka pande zote za muungano, halafu kuwe na magavana ambao wataongoza serikali za ZNZ na Tanganyika. Kila upande uwe na uhuru kamili kama vile bendera, fedha, wimbo wa Taifa nk. Kila upande uwe na Uhuru wa kujiunga na juumuiya yoyote ya kiuchumi duniani au hata ya kidini ili mradi tu kuwe na kura ya maoni kutoka kwa wananchi.

Tukiweza hayo nadhani kila upande utajihisi kuwa upo huru. Mapigano hayatasaidia lolote. Hivi leo hii Wakristo nao wakiamua kuchoma Misikiti mamabo yatakuwaje? Tukiamua na siye wabara kuwafukuza Wazanzibari waliojazana huku kwetu mambo yatakuwaje. Tafadhali UAMSHO tumieni busara.
 
Back
Top Bottom