Uaminifu na kudumu kwa ndoa

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Hili siyo eneo langu lakini limenigusa. Gazeti la Nipashe, Jumapili Januari 24, 2016, limetoa nukuu ya Balozi Christopher Liundi:

"Ukitaka usalama na mkeo usiulize idadi ya rafiki zake wa kiume kabla ya ndoa, akijipodoa usimtazame, akimaliza umsifie. Mpe fedha kwenda dukani lakini ufuatane naye. Ukinunua nyama usihesabu vipande".

Ni wazo changamoto kwa ndoa za vijana siku hizi ambao wengine huenda kwenye madhabahu wakiwa wajawazito.

CHUNGUZA CHAMBUA AMUA CHUKUA HATUA
 
Nahisi hata aliyeandika nae kaandika lakini hajaelewa,ugolo mtupu..
LUBEDE: Nimeanza kwa kusema siyo eneo langu la kujidai kitaaluma ila kama mwanandoa limenigusa. Ushauri uliotolewa na Mahundi ni mzito unao hihitaji tafakuri ya kina kwa wana ndoa.

LUBEDE kati yako na mimi nani katoa ugolo. Huna neno usichangie. Matumizi ya maneno ya staha ni kipimo cha ustaarabu na uungwana

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
TAFAKARI CHUKUA HATUA[/QUOTEME
MWENGESO:Nikutaarifu tu kuwa nipo ndoani,na yawezekana kitambo kabla yako,haya mambo hayana menyu,nimesema ugolo sio kwa kukurupuka,afu tofautisha busara na unafiki,kama ndoa yako unahisi inahitaji hayo yaliyoandikwa hapo basi hongera kwako na umshukuru mungu wako siku moja upepo usibadili uelekeo,utakuja kuniunga mkono hapa,mimi ni nyani mzee,kila nnachochangia huwa nakuwa nna idea nacho,hakuna uzito wowote hapo kwa taarifa yako.
 
LUBEDE: Sina nia ya kuendeleza malumbano. Naamini nukuu hiyo ni suala zito katika kujenga jamii yenye maadili badala ya kuweka humu JF mijadala ya watu au matukio.
 
"Ukitaka usalama na mkeo usiulize idadi ya rafiki zake wa kiume kabla ya ndoa, akijipodoa usimtazame, akimaliza umsifie. Mpe fedha kwenda dukani lakini ufuatane naye. Ukinunua nyama usihesabu vipande".

Nadhani huyo yuko mbali na Ndoa za siku hizi!
Ukitaka salama na mkeo usimfuate fuate na kuhoji marafiki zake wawe wa Kike au Kiume-kiufupi awe huru muda wote na kufanya alitakalo na kulipenda-hilo mmoja. La pili uwe na mapene na usiwe mchoyo kutoa- tatu kitandani uwe safi kama Messi! Mengine nyongeza tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom