Ualimu ni fani sawa na fani zingine. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ualimu ni fani sawa na fani zingine.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Maje Omary, Jun 21, 2012.

 1. M

  Maje Omary New Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot] Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa tz. Ajira mpya ngazi ya cheti: mwl 244,400/= afya 472,000/= kilimo/mifugo 959,400/= sheria 630,000/=. [/FONT] [FONT=&quot]Ngazi ya Diploma:[/FONT][FONT=&quot] mwl 325,700/=, afya 682,000/=, kilimo/mifugo 1,133,600/=, sheria 871,500/=. [/FONT] [FONT=&quot]Ngazi ya Degree.[/FONT][FONT=&quot] Mwl 469,200/=, afya 802,200/=, kilimo/mifugo 1,354,000/=, sheria 1,166,000/=.[/FONT] [FONT=&quot] Kwanini walimu mnanyanyaswa hivi katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Kisa cha kuwadharau na kuwapa hela kidogo ni nini? Eti sababu tupo wengi...hiyo siyo sababu. Walimu nawaombeni tuungane msimame imara kudai ongezeko la mshahara kwa 100%. Nawasilisha kwa uchungu mkubwa...maana tumekuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Tena sisi ndo tunatumika na wanasiasa..kwenye uchaguzi, sensa etc. Inatosha kupuuzwa kwa vihela hivyo, mnakosa gani ktk nchi hii?[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Nchi hii imekosa dhamira ya dhati ya kisiasa ya kuboresha elimu yetu. Wanafalsafa wa Elimu wanaamini kwamba kila mtu anafundishika. Tatizo liko katika kudharau, kuonea, kunyanyasa na kuwapuuza walimu wetu huku bado tunawataka watufundishie watoto wetu kwa bidii na uzalendo wa hali ya juu. Wenyewe wanasiasa wetu wanatuaminisha kwamba ndivyo walimu wanapaswa wawe hivyo na Mungu aliwaumba hivyo. Uliona wapi nchi inawapuuza walimu wake kiasi kwamba wazazi wanadiriki kuwachapa viboko walimu mbele ya wanafunzi wao? Halafu mwalimu afanye nini? Baada ya kufanyiwa vitendo hivyo, mwalimu aende tu kuwafundishia watoto wa hao wazazi waliowapiga viboko hadi wafaulu? Ungekuwa wewe uzalendo wa namna hii ungeupata wapi? Nadhani atakayefanya hivyo lazima awe na moyo kama wanabiifulani. [/FONT] [FONT=&quot]
  Uvumilivu unakikomo chake katika jamii, na sasa tumefikia kikomo cha uvumilivu tunatakiwa kwa umoja watu, kwa maumivu na kupuuzwa kwetu tuungane kutafuta hakiyetu. Sekta zote ni bora hakuna sekta iliyobora zaidi ya nyingine. Tena ualimu ni sekta iliyobora zaidi kwani Bila mwalimu utampata wapi huyo mwanasheria, Daktari, Injinia, Mhandisi n.k. Serikali inapswa kuwa na dhamira ya kweli katika kuiboresha sekta ya Elimu kuanzia Elimu ya Msingi hadi vyuo vikuu. Nchi nyingi duniani ambazo leo zinasifika kwa maendelea, zilianza kwa kuwekeza katika elimu. [/FONT]
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Join Date : 20th June 2012

  Posts : 1
  Rep Power : 0

  Likes Received 0

  Likes Given 0

  Nimekupenda ghafla umekuja JF vizuri....hakika wewe ni jembe.......

  Back to the point....mimi nasema ualimu ni zaidi ya fani nyingine kwasababu bila ualimu hakuna hizo fani nyingine...............I humbly submit
   
 3. G

  Gilly Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [h=3]

  [/h][h=3]Mkuu, nimekukuna nini? Umenukuu moja kwa moja mchango wangu na kuuweka hapa na kuuchakachulia maneno utumike kuhamasisha mgomo wa walimu bila ridhaa yangu. Mimi nilikuwa nawapa changamoto CWT (wewe ni Mkuu kwenye CWT nini?) kwamba waache kusumbua walimu kwa kuchimba mikwara mbuzi na huku wakijua kwamba ni waoga kutekeleza migomo wanayoanzisha hadi kuwafanya walimu wawe kwenye migomo baridi. Maadili ya Ualimu hayamtaki mwalimu agome kwa sababu kufanya hivyo ni "kumudharau, kumuonea na kumunyanyasa" mwanafunzi wake ambaye anapaswa kumjenga kimaadili na kiakili. Lakini anaruhusiwa na pia anapaswa "kumpuuza" kama anafanya mambo ya kipuuzi kama vile "kuvuta bangi, kutokusoma, kukaidi na kudadisi maagizo n.k." katika jina la demokrasia ya mawazo-kama maagizo ya kufundisha kwa "njia shirikishi". Utaratibu huu hauruhusu walimu kuwabana watoto wasome. Watoto wanakuwa huru zaidi kufanya watakavyo. Ndiyo maana mwalimu mmoja wa S/M Buguruni (kesi yake iliandikwa humuhumu JF) alihukiumiwa kifungo kwa kumchapa mwanafunzi wake viboko viwili vitatu ili kumkanya. CWT hawakumtetea ingawa ni mwanachama wao. Walipaswa wamuwekee "advocate". Mwalimu sasa anasota rumande, kazi na mume amepoteza na watoto wake wanasota na huenda wanalelewa na mama wa kambo. Mgomo baridi wanaofanya walimu uko katika mfumo wa "kupuuza wanafunzi" kwa kisingizio cha kutekeleza "njia shirikishi ya kujifunzia". Kwa hiyo wanawaacha "kama walivyo"!. Yaani aliingia darasa la kwanza "hajui kusoma wala kuandika-na kama hajitumi mwenyewe-ataondoka darasa la saba hajui kusoma wala kuandika!". Hapana kazi ya Ualimu ni zaidi ya kazi nyingine. Yataka moyo!

  Mkuu, mchango wangu uliutoa kwanye post hii:[/h][h=3]Walimu ni kada ilopoteza muelekeo.[/h] Started by Malolella, 19th June 2012 11:43
   
 4. G

  Gilly Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu, hivi kesi za walimu waliopigwa viboko na DC huko Bukoba na kuacha ujumbe wa "message sent!" na CWT kuja juu na kuchimba mkwara kwamba watamshitaki iliishia wapi? Tabia ya DC yule ilinakiliwa na wanakijiji fulani sehemu fulanifulani huko Mikoa ya Magharibi (niliisoma humuhumu JF) na baadaye Manispaa ya Morogoro nao waliripotiwa wazazi kugawa "mkong'oto" kwa walimu wa shule yao moja. Matendo hayo yalifuatiliwa sana na walimu na ufumbuzi umefichwa (kama vile kuwasahaulisha walimu) ambalo ni kosa. Hakuna mtu mwenye kumbukumbu nzuri kama mwalimu. Kuwa na kumbukumbu nzuri ni sifa kuu ya mwalimu la sivyo utakwama darasani.
  Kesi iliyoanzishwa na CWT kuupinga mkataba wa kitapeli, JK anaiita "mikataba mibovu" wa Taasisi ya Fedha ya BayPort kwa kutoa mikopo kwa walimu vijijini kwa mikataba ya ki-IPTL-IPTL au ki-Dowans-Dowans imefikia wapi? BayPort nayo imekuwa mwiba mkali sana kwa walimu. Waliokopa kwao wanajutia vikali. Wengi wamekwishamaliza mikopo yao siku nyingi ila sasa wanakatwa riba inayokua siku hadi siku. Kwa utaratibu uliowekwa, hawataachwa kukatwa. Wenyewe BayPort wanasema wanawakata kwa kufuata sheria za nchi za kutowakata zaidi ya 1/3 ya mishahara yao. Ukizingatia mishahara ya walimu ni midogo wanaweza kukatwa hadi watakapostaafu? Huu ni unyonyaji wa kikundi kidogo cha watu kuwanyonya kikundi kingine na uvumjifu wa Katiba ya nchi yetu. Si bado inafuata Siasa ya Ujamaa? Rejea Azimio la Arusha pamoja na marekebisho yake.
   
Loading...