Uadui kati ya Tanzania na Kenya ni wa hatari kuliko nchi zote duniani

Derspiegel

JF-Expert Member
May 30, 2016
285
242
Kumekuwepo historia za uadui mkubwa miaka ya nyuma kati ya mataifa mawili hasimu hapa duniani. Kuna mifano mingi sana ya mataifa yaliyokuwa na uadui mkubwa baina yao. Hata hivyo nyingi ya hizo, mataifa hasimu hayakuwa na sifa zinazoshabihiana hasa katika ukubwa wa mataifa hayo na wingi wa watu. Mfano Greek city states walikuwa na uadui mkubwa na waajemi (Persians/Iranians). Hata hivyo, kulikuwepo utofauti mkubwa kati ya mataifa hayo huku Persia ikiwa ni kubwa zaidi ya mara kumi.

Hata hivyo mataifa yaliyokuwa na uadui mkubwa sana na yaliyokuwa yakifanana kwa sifa nyingi - ukubwa, watu, rasilimali na ujirani/imepakana, ni pamoja na Athens vs Sparta, Rome vs Carthage, France vs Germany, Britain vs Germany, USA vs USSR, South Korea vs North Korea, India vs Pakistan na Iran vs Iraq. Kati ya hiyo mifano niliyoitaja, ni India vs Pakistan pekee zilizozidiana sana kieneo na watu.

Katika Afrika, mataifa yake bado ni machanga na hivyo kumewahi kutokea vita vichache kama ifuatavyo: Ethiopia vs Eritrea, Tanzania vs Uganda, Ethiopia vs Somalia, Nigeria vs Cameroon. Waafrika tatizo lao kubwa limekuwa ni civil wars.

Ukiangalia kwa kuchunguza vizuri katika nchi zote duniani ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuwa maadui, hakuna uadui potential sana, kama sisi Aftika Mashariki tunaoenda kuwa nao in years to come. Kwa ujumla, uchumi wa Kenya ni mkubwa zaidi ya ule wa Tanzania.

Hata hivyo, kinachopelekea kuwepo kwa potentiality ya uadui mkubwa kati ya mataifa haya mawili ni: mpaka mrefu, kuwepo milima mirefu na miinuko mirefu (zinazidiwa tu na Ethiopia), idadi kubwa ya watu (zinashika namba 6 na 7 ina Afrika), hali ya hewa inayofanana sana, kilimo cha mazao makuu yanayofanana (chai, kahawa, pamba, pareto, mkonge na horticulture), miundombinu inayohudumia landlocked countries (Rwanda, Burundi na Uganda), chumi zinazoongoza Afrika Mashariki, utajiri wa hifadhi za wanyama (ndizo zenye mbuga za wanyama very rich duniani), mafuta na gesi vilivyoanza kugundulika kanda za pwani, makabila yaliyoingiliana (wajaluo, wakurya, wamasai, wandorobo, wadigo, wangassa na mengine.

Ukiviangalia kwa ukaribu hivyo vigezo utaona ndiyo nchi pekee kubwa kabisa duniani kwa sasa, tangu Ujerumani vs Ufaransa (1871 - 1945), ambazo zina vitu vingi zinafanana.
 
Wabongo tuna kelele nyingi tu...kiuhalisia tunawazidi Kenya kwa natural resources lakin wenzetu wamejitahidi ku utilize resources zao effectively ndio maana wametupiga gap...!tusipobadilka tutaendelea kujipa moyo tu kuwa tunashindana na Kenya lakini kiuhalisia wametuzidi sana na tunahitaji nguvu ya ziada..!
 
Mchome unaweza ukawa sahihi kuwa tunawazidi natural resources lakini uwe makini sana na hili neno resources na natural resources, kwani kitu ambacho tumekuwa tukikisahau ni ardhi. Ardhi yenye rutuba ni resources ya kwanza kabisa kuliko kitu chochote, ikifuatiwa na hali nzuri ya hewa (achana na madini maana ni kitu cha muda mfupi tu hicho).
Ni kwenye ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa, ambapo wakenya na nchi zote zilizotuzunguka ndipo walipotuachia.
Kweli asilimia karibia 70% ya Kenya ni arid land lakini ile asilimia nyingine 30% ni bora mno kama jinsi tunavyosifia ardhi za Arumeru, Moshi, Bukoba, Muleba, Ngara, Ukerewe, Rungwe, Kyela, Mbinga, Ileje, Lushoto, Kasulu, Morogoro, Njombe, Mbozi na Tarime. Haya ni maeneo yenye hali nzuri ya hewa na rutuba nyingi hapa nchini.
Hata hivyo, pia hapa kwetu hayo maeneo ni kama asilimia 20% ya nchi nzima. Hivyo utaona kuwa, wakenya wana maendeleo kwani zaidi ya asilimia 85% (zaidi ya milioni 35) wanaishi kwenye hiyo asilimia 30% ya ardhi, wakati sisi wanaoishi kwenye ardhi nzuri ni chini ya asilimia 30 (wastani wa watu milioni 15).
 
Nani alikwambia kwamba ukerewe kuna ardhi nzuri ?
 
Mbona Kenyans peace tu mkuu. Hahahaa umeandika very serious lakini uhalisia ukienda Kenya utagundua watu wala hawana time kuchukia waTz kama media inavyotaka watu waamini.
 
Kenya na Tanzania ni ndugu aise, hii nyingine yote ni siasa na porojo za elites na wanasiasa, tembea Kenya kama Mtanzania uone kama kuna mtu atakusumbua, ama akubague kwa kuwa wewe ni Mbongo, hivyo hivyo kwa wakenya waliopo na wanaotembelea Tanzania. mabishano ya hapa kwenye mtandao tusichukulie kama kuna siku tutakuja pigana, mwanzisha mada ni mchochezi tu. umoja ni nguvu.
 
Hii mada haizungumzii upeace wa wananchi wa nchi husika, isipokuwa uwezekano wa migogoro mikubwa ya kibiashara huko mbeleni kutokana na kuwa na rasilimali zinazofanana.
Na kiukweli hii ni siyo changamoto ya watanzania isipokuwa ni presha ndio iko kwa wakenya.
Kihistoria, hao jamaa wamekuwa na wivu na rasilimali zetu na jinsi tusivyokuwa na uwezo wa kuziendeleza vyema, ndiyo maana huwa wanatangaza Mlima Kilimanjaro kuwa uko kwao kwani ukiwa Kenya ndio unaufaidi zaidi kulikp kwetu ambako unakuwa umefunikwa na mawingu mara nyingi. Pia huwa wanawaaminisha watu kuwa ukiwa Kenya kwenye mbuga yao ya Masai Mara unapata maajabu yote ya Serengeti hasa uhaji wa nyumbu na pundamilia kutoka Tanzania kwenda Kenya.
Ukitaka kujifunza reality kidogo ya huko tunakoelekea, angalia mzozo wa bomba la mafuta la Uganda. Pia angalia wakenya kwa kushirikiana Kagame walivyoweza kuishawishi Uganda na kutaka kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na Tanzania ilibaki ikiungwa mkono na Burundi pekee, huku tukiitwa ni watu tunaokwamisha kuendelea kwa Jumuiya hiyo.
Vilevile usisahau kuwa, hao jamaa waliona sana wivu baada ya Tz kumfurumsha "Idd Amin kwenye vita ya 1978 - 1979, huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza duniani tangu WW II, kuteka mji mkuu wa nchi nyingine na kuanzisha serijali mpya.
 
Wanachotushinda zaidi wakenya, ni human development. Majority ya wakenya (85%), wana asili ya maeneo yenye hali nzuri ya hewa, hivyo wana uwezo mzuri kulinganisha na watanzania ambao majority wanaishi maeneo makame na yanayopata mvua za wastani wa mm chini ya 1000, kiwango kidogo kuweza kuivisha varieties nyingi ya vyakula.
 
Hata hivyo, kitakachotusaidia sana baadaye ni population explosion ya watanzania kulinganisha na wao. Ni kwa njia hii tunaweza kushindana nao vyema kwani tunaweza kufidia udhaifu wetu katika quality - based human resources kwa kuwa na quantity based human resources nyingi zaidi kama jinsi tunavyoona China ikitegemea quantity (1.3 billion pop.) kushindana na USA yenye quality (300 million pop.).
Hivyo tukiwa na watu wengi, ndio tunaanza kuangalia rasilimali nyingine kama madini ambapo hadi sasa wanatupiga mbali kwa kuwa na mafuta huku na sisi tukiwazidi kwa gesi (futi za ujazo trillion 53).
 
Baada ya hapo tutaweza kulinganisha pia resources ya maji ambayo inaweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji. Kwenye hili Kenya wako nyuma kidogo kwani wana mto mmoja tu mkubwa wa Tana na asilimia kama 17% ya Ziwa Victoria, wakati sisi tukichukua 51% ya ziwa hilo. Aidha tuna maziwa mengine yenye maji mengi kuliko hata Victoria ya Tanganyika na Nyasa, pamoja na mito mikubwa ya Rufiji na Ruvuma.
Tanzania tuna eneo kubwa la Bahari ya Hindi kuliko Kenya kama mara mbili.
 
Hii
Kenya na Tanzania ni ndugu aise, hii nyingine yote ni siasa na porojo za elites na wanasiasa, tembea Kenya kama Mtanzania uone kama kuna mtu atakusumbua, ama akubague kwa kuwa wewe ni Mbongo, hivyo hivyo kwa wakenya waliopo na wanaotembelea Tanzania. mabishano ya hapa kwenye mtandao tusichukulie kama kuna siku tutakuja pigana, mwanzisha mada ni mchochezi tu. umoja ni nguvu.
Hii ndiyo hali ikiyowakuta Uingereza na Ufaransa. Hawakuwahi kutegemea kuungana kwa mataifa ya kijerumani - Prussia, Bavaria, Baden, Saxony na Wurttemberg. Wakati Prussia inapigana na Denmark na baadaye Austria, ilikuwa ikionekana ni dhaifu hivyo iliweza kuingia mikataba na wafaransa, waingereza na warusi kutoingiliana kwenye maslahi yao. Hivyo Prussia iliishagaza dunia wakati huo (1866)ilipoipiga Austria (kipindi hicho taifa lenye nguvu ulaya nyuma ya uingereza, ufaransa na urusi pekee).
Hata hivyo baada ya Chancellor wq Prussia Otto von Bismarck kuiongoza kuipiga ufaransa mwaka 1871 na kupelekea kuubda taifa jipya lenye nguvu kubwa ulaya, mataifa mengine makubwa hasa wafaransa, waingereza na warusi wakijilaumu sana jinsi hali hiyo ilivyotokea kutokana na tabia yao ya zamani ya kuungana mara kwa mara dhidi ya taifa kinaloonekana kuwa na nguvu nyingi (balance of power). Ujerumani imewasumbua sana watu wengine tangu hapo kwani iliharibu the old system of balance of power na kupelekea kuanzisha kwa Alliances.
Ndiko na sisi tunakoelekea years to come na siko tayari kuwa nyuma kuongea kitu ambapo kina uwezkano mkubwa wa kutokea.
Hii hali haluioni coz Aftika bado ni masikini lakini siku Afrika tukianza kuexperience maendeleo makubwa, utaona kuwa hapa Afrika hakuna nchi zikizopose kuwa maadui (labda ya kiuchumi tu....) kama nchi hizi.
 
Mchome unaweza ukawa sahihi kuwa tunawazidi natural resources lakini uwe makini sana na hili neno resources na natural resources, kwani kitu ambacho tumekuwa tukikisahau ni ardhi. Ardhi yenye rutuba ni resources ya kwanza kabisa kuliko kitu chochote, ikifuatiwa na hali nzuri ya hewa (achana na madini maana ni kitu cha muda mfupi tu hicho).
Ni kwenye ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa, ambapo wakenya na nchi zote zilizotuzunguka ndipo walipotuachia.
Kweli asilimia karibia 70% ya Kenya ni arid land lakini ile asilimia nyingine 30% ni bora mno kama jinsi tunavyosifia ardhi za Arumeru, Moshi, Bukoba, Muleba, Ngara, Ukerewe, Rungwe, Kyela, Mbinga, Ileje, Lushoto, Kasulu, Morogoro, Njombe, Mbozi na Tarime. Haya ni maeneo yenye hali nzuri ya hewa na rutuba nyingi hapa nchini.
Hata hivyo, pia hapa kwetu hayo maeneo ni kama asilimia 20% ya nchi nzima. Hivyo utaona kuwa, wakenya wana maendeleo kwani zaidi ya asilimia 85% (zaidi ya milioni 35) wanaishi kwenye hiyo asilimia 30% ya ardhi, wakati sisi wanaoishi kwenye ardhi nzuri ni chini ya asilimia 30 (wastani wa watu milioni 15).

mkuu despiergel,kutokana na takwimu zako mie bado naona tunawashinda wakenya kwa hiyo maliasili ardhi maana 20% ya km za mraba za tz ni kubwa kuliko 30% ya km za mraba za kenya hivyo sisi bado bora kuliko wao. na point yako kuhusu wakaazi kwenye ardhi tajwa sio kigezo maana mtu anaweza kuitumia lakini akawa anakaa mahala kwingine. ungeongelea matumizi yenye manufaa ingekua bora zaidi. asante
 
Mkuu kuna tofauti kubwa sana kati ya adui na competitor.

Kenya si adui wa nchi hii ni competitor tu, na hakuna taifa duniani lisilo na competitor.

Hata kwenye maisha ya kawaida kuna competitors, haina maana kuwa kila siku lazima mtwangane ngumi.

Ni kama simba na yanga tu.

Hili gemu huwa halihitaji hasira
 
Back
Top Bottom