Ugonjwa wa Homa ya Matumbo (Typhoid): Dalili na tiba yake

Chupayamaji

Hili tatizo la typhoid limekuwa ni janga japo watu wanachukulia masihara. Mimi nna mwaka wa 3 bado nasumbuliwa na sio mimi tu nawaona na wengine wengi around me ni hivohivo. Japo wengne wanaona completely.

Kama kuna anaetibu kiuhakika typhoid sugu na inayojirudia mara kwa mara, naomba anisaidie japo sio bure.
 
Ukiumwa typhoid kwa lugha nyepesi umekula mavi.so watch out kula na kunywa yako sababu wengine hawazingatii usafi
 
Nakushauri upime hospital kubwa haswa za serikali kama una hiyo shida ya typhoid hospital nyingi za private especially dispensary level zimeshakatazwa kupima ila coz ya maslahi wengi bado wanapima,serikali inakataza njia ya rahisi inayotumiwa ambayo ni tile method ambayo nyingi reagent zake ukipima huwa inaonesha unayo typhoid so serikali inataka itumike njia ya culture and sensitivity (upandikizi)ambayo ndio sahihi kwa asilimia 100
 
Habari za mishemishe wanajamvi,

Ni matumaini mu wazima wa afya, kwa wale wagonjwa na waliokumbwa na matatizo Mungu awajaalie.

Going straight to the point, kuanzia mwaka 2017 nilipata maumivu makali ya kichwa, ilikuwa mwezi wa kumi na hii ilinilazimu kuenda hospitali, nikafanyiwa vipimo vya Malaria, Typhoid na ugonjwa wa homa ya matumbo.

Baada ya majibu kutoka nikaambiwa nina Typhoid hivyo nikaanza dozi ya vidonge 30 ambavyo nilikunywa kwa takribani siku 20.

Lakini ikawa ikifika muda wa usiku ninachoka sana, macho yanaona maruerue (blurred vision) na hata nikianza kusoma hata kajitabu kenye kurasa hata 100 uchovu unakuwa mwingi, nikaamua kuyabwaga hayo madawa hali ikatulia lakini mwaka 2018 hali ya maumivu ya kichwa ikarudi tena wakati huu hadi sehemu za joints zilikuwa zinauma, wakati wa long call feaces was bloody.

Nikarudi tena hospitali na kupima na kukutwa na Typhoid nikapewa tena dawa za kutumia ni zilezile naikaona nizitumie tu lakini hali ilijirepeat tena lakini kwa muda huu nilimaliza dozi, baada ya muda Typhoid ilitulia lakini imekuwa ikijirudia rudia ambapo mwaka 2019 na mwanzoni mwa mwaka huu tena tatizo limejirudia tena.

Sasa nilikuwa naomba ushauri wenu je inawezekana nina allergy na hii dawa au ni matatizo mengine yamejificha chini ya Typhoid ambayo ninatakiwa kuyapima kama yapo ni yapi?
 
Tafuta majani ya huu mti wa matunda yanaitwa songwa chemsha kunywa kwa siku mara 2 tu kwa siku 5 tuu hutaskia tena kitu inayoitwa typhoid.

images%20(1).jpeg
images.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio tatibu lakn nijuavyo hakuna usugu kwenye typhoid ila inawezekana hata mazingira anayoishi mgonjwa, kama maji anayotumia, vyakula anavyokula!!
 
Kama typhoid kweli hilo tatizo dogo achana na kusumbuka hizo dawa. Chukua nanasi ioshe menya maganda yake yachemshe vizuri chuja ile togwa yake kuwa unakunywa kama kawaida unavyokunywa maji. kwa muda wa week mbili nenda kapime alafu rudisha majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dim Ray, Asalam aleykum, (Amani iwe juu)
Kwakua umeitaji dawa ya typhoid ngoja niitaje hapa kwa faida ya wasomaji wote na ALLAH atawapa nafuu tuseme Amin.

MAHITAJI
1.KITUNGUU SWAUMU
2.MAZIWA FRESH

MATUMIZI
Menya vitunguu vyako kwa idadi utakayoona ni rafiki kwako mana wenye matatizo ya pressure hawatakiwi kula vitunguu vingi.
Ukimaliza kumenya twanga au kwa wale majasiri wanaweza wasivitwange.
Ukishamaliza chukua maziwa vichemshe vitunguu pamoja na maziwa.
Baada ya maziwa yenye mchanganyiko wa vitunguu swaumu kuchemka weka kwenye kikombe na kunywa.
Kama vitunguu haujavisaga itakubidi uvitafune wakati wa kunywa hayo maziwa mana vitakua chini kabsa baada ya kuchemka utavitoa na kuviweka kwenye kikombe....

ZINGATIA
Dawa hii unakunywa mara×2 asubuhi na usiku... dozi yake ni ya siku 2
Asubuhi hakikisha unakunywa kabla haujala chochote inapendeza zaidi ukachemsha na kunywa kabla ya kupiga mswaki ukanywa then ukapiga mswaki kuondoa harufu ya kitunguu
Usiku hakikisha unakunywa hii dawa baada ya kula chakula cha usiku na hauna ratiba ya kula tena kitu chochote ndio unakunywa hii dawa
hakikisha unakunywa maji ya kutosha

DAWA HII INATIBU TYPHOID KWA SIKU 2 TU.. KWA UWEZO WA ALLAH

NB: kama umeenda hospital ukapima ukakutwa na typhoid haina haja ya kununua dawa za vidonge rudi home tengeneza hii dawa kunywa asubuhi na jioni kwa siku 2 then utareta mrejesho

kama umeshaanza kutumia dawa za dukani bhasi hakikisha unamaliza dozi then kama itakuwa bado ipo ndio utumie hii dawa baada ya kumaliza dozi yako nimesema hivi ili kuhepuka kuchanganya dozi mbili kwa wakati mmoja

Ukiona huu ujumbe umekusaidia unaweza share kwa wengine wasio jua ili na wao wapate kupona....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom