Umeoa wewe, na kama umeoa, ndoa yako ina muda gani. Maisha ya ndoa hayana mfumo maalum, ndio maana Bibllia ianaelekeza Wanaume kuishi na wanawake kwa akili sana (ina maana unaweza kuwa namba 1-10), nao waelekezwa kuwapenda waume zao. Chezea wanawake wewe, jinyenyekeze siku zote uone, unatakikiwa kuwa mtu wa katikati. Mambo yakiwa vizuri unacheka na my wife wako mpaka jino la mwisho, akikurofisha unakuwa mkali kama Nyati wa Selous. Kama ukiendekeza namba kumi, siku ukibadilika, itabidi umwambie mkeo hiyo tabia nani kakufundisha ikiwa ni pamoja na marafiki zako kupigwa marufuku kufika hapo kwako.