Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 39,935
- 61,723
Wikiend hii sitaki kutembelea maeneo ya starehe kabisa, bali nataka niitumie vizuri kwa kuwinda vindege mbalimbali; kama nitapata kanga, njiwa, kwelea kwelea, kware n.k sawa tu, na kama nitabahatisha wanyama wadogowadogo itakuwa vizuri pia.
Hapa nimeandaa manati, ndala za matairi (katambuga), kaptula ngumu ya jinsi na shati gumu la kadeti, kibuyu cha maji, na mahindi ya kukaanga.
Nimepanga katika uwindaji huu, niende na mdada mmoja machachari wa jf angalau na yeye akajifunze namna ya kutumia manati.
Kama kuna wazoefu wa kuwinda humu, tukutane mbugani na manati zenu.