Twendeni tukamuage, tukamzike kamanda Mawazo

Twendeni tukamuage, tukamzike kamanda Mawazo

So sad just like a candle in the wind!
 
mbegu hudondoka ardhini nayo baada ya muda huchipua na kuzaa matunda mengi zaidi.RIP COMRADE MAWAZO.
 
RIP Kamanda. Damu yako inatupa ushujaa mkuu, moyo na ujasiri uliotukuka katika kupata nuru mpya katika Taifa hili. kama vile damu ya Yesu ilivyowaletea wakrito imani ya kukombolewa kwao kutoka katika uovu wa shetani. AMINA AMINA AMINA
 
Mola awatangulie na amlaze mahala pema peponi kamanda Mawazo.
 
nawashukuru makanda wote walioguswa na msiba huu wa mpendwa wetu KAMANDA MAWAZO Mungu awape moyo wa amani Watanzania R I P KAMANDA
MBELE YAKO NYUMA YETU
 
Machozi yanatiririka. Kapumzike kamanda umetuacha wakiwa ila mawazo yako tutayaendeleza.
 
Pumzika kwa amani kk hakuna maneno yanayoweza kujitosheleza kuelezea mchango wako ktk ujenzi wa tanzania yenye haki.
 
Geita atafikia wapi?

Jumapili trh 22/11/2015 tutauchukua mwili wa mpendwa wetu kutoka jijini Mwanza kwenda Geita mjini kwa ajili ya wakazi wa Geita nao kupata fursa ya kumuaga kipenzi chetu na mwenyekiti wetu wa chama ambapo hilo zoezi litafanyika hadi jioni na baada ya zoezi hilo tutauchukua mwili wa mpendwa wetu na kuelekea nyumbani kwao kijijini jimboni Busanda, tutalala pale na kesho yake siku ya Jumatatu ndo itakuwa siku ya kumpumzisha mpendwa wetu MAWAZO katika nyumba yake ya milele hapa jijini Mwanza.

Tunaendelea kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali za nchi wengi kutoka Arusha na Daressalaam, na tunatarajia kupokea ugeni mzito sana hapa jijini na geita kwa ajiri ya kamanda MAWAZO.

Napenda kulisihi Jeshi la Polisi kuwa wastarabu hasa police wa hapa Mwanza, manayake kwa ninavyoona wengi sana wenye magari, wenye pikipiki, wenye baiskel na watembea kwa miguu watajitokeza hivyo kusababisha msongamano katika barabara za jiji, hivyo busara ya polisi inahitajika, mabomu sio suluhu ya kila kitu.

TWENDENI TUKAMUAGE, KUMPUMZISHA KAMANDA MAWAZO.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom