Twendeni tukamuage, tukamzike kamanda Mawazo

Twendeni tukamuage, tukamzike kamanda Mawazo

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,505
Reaction score
8,256
Kwa wale wazalendo wanaohitaji kutoa heshima za mwisho kwa member mwenzetu wa Jamii forums kamanda AC MAWAZO Utaratibu uko hivi:

Siku ya Jumamosi trh 21/11/2015 tutauchukua mwili wa mpendwa wetu kutoka hospitali ya bugando na kuupeleka nyegezi luchelele kwa ndugu yake kwa ajili ya wakazi wa jiji la mwanza na viunga vyake kutoa heshima za mwisho kwa kamanda wetu, hili zoezi litafanyika siku nzima ya Jumamosi na mwili utalala palepale Luchelele.

Jumapili trh 22/11/2015 tutauchukua mwili wa mpendwa wetu kutoka jijini Mwanza kwenda Geita mjini kwa ajili ya wakazi wa Geita nao kupata fursa ya kumuaga kipenzi chetu na mwenyekiti wetu wa chama ambapo hilo zoezi litafanyika hadi jioni na baada ya zoezi hilo tutauchukua mwili wa mpendwa wetu na kuelekea nyumbani kwao kijijini jimboni Busanda, tutalala pale na kesho yake siku ya Jumatatu ndo itakuwa siku ya kumpumzisha mpendwa wetu MAWAZO katika nyumba yake ya milele hapa jijini Mwanza.

Tunaendelea kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali za nchi wengi kutoka Arusha na Daressalaam, na tunatarajia kupokea ugeni mzito sana hapa jijini na geita kwa ajiri ya kamanda MAWAZO.

Napenda kulisihi Jeshi la Polisi kuwa wastarabu hasa police wa hapa Mwanza, manayake kwa ninavyoona wengi sana wenye magari, wenye pikipiki, wenye baiskel na watembea kwa miguu watajitokeza hivyo kusababisha msongamano katika barabara za jiji, hivyo busara ya polisi inahitajika, mabomu sio suluhu ya kila kitu.

TWENDENI TUKAMUAGE, KUMPUMZISHA KAMANDA MAWAZO.
 
RIP MAWAZO!!! Najiuliza nashindwa pata jibu namkumbuka sana sugu!!Mikononi mwa polisi!!!
 
Binafsi nawatakia kila la kheri katika maandalizi hayo ya kumpumzisha Kamanda Mawazo, sina jinsi tu ya kuweza kuhudhiria kutokana na majukumu, ila tupo pamoja sana katika wakati huu mgumu.........KUIPENDA CHADEMA SIKUJUTII HATA KIDOGO PAMOJA NA MADHILA YANAYOKUTA MAKAMANDA WAKE.
 
Nenda kamanda Mawazo.... tulikupenda.... bwana ametoa na binadamu wamechukua.... mbegu uliyo ipanda itadumu milele....watz wako tayari kwa mabadikiko... its a matter of time....
 
rip kamanda mawazo damu yako hakika haitapotea bure wewe daima tutakuenzi kwa mchango wako katika chama chetu na mabadiliko ya nchi yetu tz
 
R.I.P mawazo, Ujasiri wako unatupa moyo, binafsi nilivunjwa mkono Geita ila nitarudi kuwasalimia, nitapeleka na salamu zako pia.
Tangulia kamanda!
Tuliobaki tutajitahidi tusife mapema.
 
Back
Top Bottom