Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,660
- 1,801
Katiba mpya itakayopunguza kabisa mamlaka ya rais. Ni dhahiri Katiba hii haitoshi kwa Tanzania ya sasa.
Katiba tuitakayo itabidi itoe uwezo wa wazi na hatua za wabunge kuweza kuweka muswada wa kumvua madaraka rais.
Kila kitu kina wakati wake. Hivi sasa wakati wa Katiba inayoendana na wakati umewadia. Vinginevyo itaishia kupiga kelele kwenye mitandao tu huku viongozi wakijiona ni wao pekee wenye maamuzi kwa Watanzania wote.
Nadhani wana harakati na wapinzani waanze kuacha malalamiko yote na waelekeze sauti kwenye kutaka Katiba mpya.
Itakuwa pia ni kwa maslahi ya mabadiliko, kwani kwa Katiba hii hakuna kitakachobadilika ila sura tu!