Inawezekana kabisa huyo anayeingia Chuo Kikuu kupitia "Recognition of Prior Learning - RPL" akaandika kwa ufasaha kuliko ulivyoandika, kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, matumizi (sahihi) ya kituo kikubwa, kituo kidogo, herufi kubwa, ndogo na utohoaji wa maneno ya Kiingereza!
Ninavyofahamu, utaratibu RPL umekuwa ukitumiwa na Vyuo vya hapa Nchini kwa miaka mingi. Mitihani ya sasa ya RPL inaweza kufananishwa na Mitihani iliyokuwa ikiiwa "Malticulation Test/Examinations". Utaratibu huu sio mgeni na huna haja ya ama kuwaogopa, kuwaonea wivu au kuwa na wasiwasi na hao unawaita "kenge" kwa vile wanajiunga na Elimu ya Chuo Kikuu kupitia utaratibu wa RPL.
Fahamu vilevile kuwa utaratibu wa RPL unatambulika, unakubalika na kutumika Kimataifa. Utaratibu huo unatumika katika Mataifa yaliyoendelea mfano Marekani, Kanada, Uingereza, China, Japan, Urusi, n.k. na zinazoendelea kama Tanzania, Kenya, n.k.
Mengine utayapata kupitia "Google Search Engine".
na ww ni RPL nn mkuu ndugu yangu,mbona imekugusa sn, then iyo inayozungumziwa apo na matriculation test ni tofauti kwakua matriculation test zinasimamiwa na chuo husika na zinafanywa na wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na chuo husika thats why nikatoa ushauri ni bora na vyuo vikatoa entrance exams ambayo ndio sawa na matriculation test uliyozungumzia. "pamoja tunajenga"
na ww ni RPL nn mkuu ndugu yangu,mbona imekugusa sn, then iyo inayozungumziwa apo na matriculation test ni tofauti kwakua matriculation test zinasimamiwa na chuo husika na zinafanywa na wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na chuo husika thats why nikatoa ushauri ni bora na vyuo vikatoa entrance exams ambayo ndio sawa na matriculation test uliyozungumzia. "pamoja tunajenga"
Asante kwa ufafanuzi Mkuu. Hapana, kwa sasa mimi sio RPL. Nilibahatika kupita bila kukwama Darasa la Saba, Kidato cha IV, Kidato cha VI na IFM (ADA na PGD). Ninajiandaa na Msc mwaka huu. Hata hivyo, Elimu haina mwisho, siku zijazo naweza amua kubadili fani, mfano nikapenda kujiunga na SUA kwa Taaluma ya Kilimo, pengine nitatakiwa kupitia RPL! Ni mfano tu!
Kuna vilevile watu wenye uwezo darasani, lakini hawakubahatika kuendelea na Elimu ya Juu kama wewe na mimi, pengine kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao, umasikini, uyatima, ajali, uchache wa Vyuo miaka iliyopita, n.k. je ni haki kuwaita kenge na kuwafungia fursa za kujiendeleza kielimu?
"Pamoja tunajenga"!
Kweli mtu wa darasa la saba bado sana [emoji85] [emoji86]Habari wana jamvi!
Mimi kuna swala linanichanganya na kama ningekua na mamlaka wala nisingekubali lipite, ni Ili swala la recognition of prior learning.
Yani huwezi kuniambia darasa la saba umpe mitihani mitatu ya kucolify kwenda chuo kikuu alafu yote apige B then aende chuo kikuu mm kwa ushauri wangu nadhani kuna haja kama alivyosema mdau mmoja wa jf vyuo viweke entrance exams nadhani ii itakua njia nzuri kuwapukutisha kenge wote ktk kundi la mamba.
Sijui wana jamvi mnalizungumziaje ilo.