Tuzungumze kuhusu watoto

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,095
22,729
HABARI ZENU WAPENDWA.

Siku ya leo nikiwa katika mapumziko nimeketi kwenye mgahawa fulani(sitautaja) nakunywa zangu mtindi hapa wilayani moshi mkoani kilimanjaro kakaja katoto kakiume umri kama miaka mitano. Yule mtoto aliingia na baba na mama yake eneo hilo. Walipoingia yule mtoto bila kupoteza muda akawahi akaja kwenye meza yangu, huku anatabasamu na kasura kake ka kimalaika akanifanya nisahau kuwa nipo duniani nikahisi nipo bustani ya edeni na malaika kaja kunisabahi. Kwa kawaida yangu huwa nazungumza na watoto kwa sauti ya utulivu na huwa natumia sentensi zilizonyooka na wala siongei na mtoto as if nina majipu mdomoni mfano siwezi mwambia "hujambo toto njuli" bali husema kwa sentensi iliyo nyooka namna hii "hujambo mtoto mzuri" .

Sasa basi, yule mtoto akaja akatabasamu na akapanda kwenye kiti akanisalimia shikamoo uncle, nikamuitikia marahaba, haujambo mtoto mzuri akajibu nikamuuliza jina lake akaniambia anaitwa clemence na tuliendelea kubadilishana maneno as if nazungumza na mtu mzima mwenzangu kwa maana kwa umri wake aliyajibu maswali bila kigugumizi wala haya au uoga lakini pia mtoto alikuwa na energy ambayo si ya kawaida kwa watoto wa umri wake kwa maana alikuwa ana ile drive ambayo inakufanya mtu mzima uzungumze naye kwa shauku ya kutaka kujua ni mtoto wa nani.

Wazazi wake wakaja na walipofika walinisalimu kwa ukarimu na kwa ustaarabu wa hali ya juu(wanaonekana ni couple yenye upendo na maelewano ya hali ya juu) walitaka kunisalimu na kumchukua clemence wao ili wanipishe kwa maana wamenikuta pekee yangu ili nao wakaketi katika meza yao ila sikuunga mkono nikawaambia kwakuwa clemence ameshawaonyesha mahala anapotaka kukaa hebu wasisite kumjoin. Basi ikawa burudani kwa maana kulianza mjadala mzito sana juu ya swala la uzazi na malezi ya watoto kisasa na namna ya kumjenga mtoto kuja kuwa mtu muhimu baadae kimaadili na kiutendaji yaani weledi. Mada hii ili onekana kuwavuta sana wazazi hawa ambao walitaka kushare nami na kujifunza mengi toka kwangu. Kiukweli yale mazungumzo yalikuwa very interesting na nikajifunza mengi lakini muhimu nikajihoji na kuwahoji wao pia kuwa swala la kupata mtoto na malezi limekaaje kwa hapa nchini.

Baba clemence alinijuza swala la malezi ya mtoto kuwa yamegawanyika katika level au matabaka ma'nne (4), ambayo ni level ya kwanza ni baba na mama, ya pili ni ndugu au wanaukoo wa pande mbili za baba na ,mama , ya tatu ni jamaa,marafiki, majirani na wanajamii waliomzunguka mtoto,taasisi za kidini au ngo's zinazodeal na watoto direct au taasisi yeyote ya binafsi inayodeal na watoto, na ya nne ni serikali na taasisi zake kama vile shule, wizara zinazodili na maswala ya watoto moja kwa moja kama wizara ya afya, ustawi wa jamii, n.k! alizungumza mengi sana hapa jinsi namna gani hizi sekta nne zilivyo na muingiliano katika kumlea na kumkuza huyu mtoto kwa kupokezana na kwapamoja hadi pale huyu mtoto atakapokuwa mtu mzima na kurejesha baraka kwa jamii iliyomlea. Kufeli kwa ushirikiano baina ya hizi sekta nne tayari kunaandaa mazingira mabaya ya kupata rasilimali watu ambao ni msaada kwa taifa au wa kutegemewa na taifa katika kuleta maendeleo.

Baba clemence alizidi kunipa mifano kama ya hapo nchi kama china na hata Finland kuwa ni mataifa ambayo yanatambuwa na kufanyia kazi muingiliano wa sekta hizi 4. Na wametenga bajeti na hata mijadala ya utungaji wa sheria na mikakati ya kimaendeleo huwa inatazamia sana uwepo wa hizi sekta katika taifa. Kwao kuwekeza kwa mtoto ni ajenda ya muhimu na si ya kufanyia majaribio au kuipigia domo tu bila vitendo. Maswala ya malezi, uzazi, chakula cha mtoto, elimu, makuzi, kumjali, afya, nakadhalika ni ajenda ya kitaifa na sio vikundi vya watu au baadhi ya wanajamii au taasisi. Hii inasaidia sana katika kuchannel wao kama taifa wanaelekea wapi baada ya miaka 100 ijayo.
Kwa mafano alizungumzia kuwa ni target ya kila wazazi au couple kumshape mtoto wao awe productive kwa asilimia 100 na sio kubahatisha na maneno kama kila mtoto na baraka zake kisha kufumurumusha watoto kama unafungua timu ya mpira. Tathimini ya haya mataifa ni kuwa ubora wa mtu wao m'moja miaka ijayo uwe ni sawa na watu miamoja katika maifa kama yetu, yaani ni kuwa kama ukiweka kichwa cha mtoto wa familia ya mfinland anauwezo wa jitihada ya kuleta maendeleo ambayo kwa nchi kama tz hayo maenedeleo yatahitaji vichwa mia moja ambavyo vina degree tofauti tofauti.

Tulizungumza mengi kwakweli ila swali nililooondoka nalo pale baada ya yale majadiliano ya maana na ya msingi na ya kimaendeleo yaliyodumu kwa muda wa saa kama mbili hivi mahala pale pale tulipokutana ni kuwa hivi je watanzania tunatazamiaje kizazi chetu miaka 100 ijayo baada ya sisi kusepa. Hivi hawa watoto ambao mama zao ni masistaduu, baba masharobaro viduku, ndugu katika ukoo wenye ghubu na visirani na wasiotaka kujali watoto wa ndugu zao, jamii yenye mtawanyiko wa tabia na maadili na kila dosari isiyoelezeka, taasisi zisizotimiza wajibu zilizoainisha katika makabrasha, serikali (ukiachia awamu hii) ambazo hazijatoa dira kamili juu ya mtaala rasmi wa uzazi na malezi ya watoto katika level zote nne, hivi nini kinatujia huko mbeleni wadau, je, tukae kimya miaka iende yatukute ya kutukuta, au tuchukue hatua sasa?!

Swali nawaachia mnijibu kwa mapana na marefu.
 
Abarikiwe baba Clement, malezi ya mtoto ni Zaidi ya nguo na chakula, kuanzia ujauzito unatakiwa uanze kuongea na mwanao akiwa tumboni, hii inamfanya anazoea sauti yako pia mnaanza kujenga bond, akizaliwa unaongea nae, na anavyokuwa akiuliza maswali mjibu vizuri kwa ufasaha, inamsaidia kupanua uwezo wa kufikiri.

Haya ni magumu ku yatimiza, kwanza wazazi wanatumia muda mwingi makazini au katika sehemu zinawaingizia kipato, unamwacha mtoto na housegirl, au unampeleka mtoto boarding school akiwa bado mdogo.
,
 
Hivi kuongea na mtoto tumboni ni kweli anakusikia au Hollywood tu?
 
anasikia mkuu.. wangu nilikuwa nikiongea naye namshika kwa juu ya tumbo unaona anacheza cheza hadi raha
Hongera kwa kuzaa kwanza...sasa akicheza hivo ina imply nini... Kwa mie ambae sina mtoto hio kitu bado sijaipata pata fresh
 
Hongera kwa kuzaa kwanza...sasa akicheza hivo ina imply nini... Kwa mie ambae sina mtoto hio kitu bado sijaipata pata fresh
ukiwa naye tumboni utajua.. unapokuwa naye ni kama upo na mtu pembeni asiporespond unakuwa na wasi wasi ..
 
Aliyoyasema Mr Clemence ni sahihi, ila ni muhimu pia tunapokua na hitaji la kuleta mtoto basi ni muhimu kuomba na kuzungumza na MUNGU..kwa maana ni muhimu wenza wote kuomba Yale yote ya msingi wanayohitaji juu ya ujio wa mtoto wao, ikiwezekana kufunga na kuomba before tendo mlozamiria la utungaji mimba..
 
ukiwa naye tumboni utajua.. unapokuwa naye ni kama upo na mtu pembeni asiporespond unakuwa na wasi wasi ..
Hii ni kweli kabisa. Imethibitishwa hata kwa tafiti, sio movies. Tafiti zinaonesha kuwa hata ukimsikilizisha muziki akiwa bado yupo tumboni, atakapozaliwa akiusikia unakuwa familiar kwake. Ndio maana inashauriwa kuwa mama asipate sana ghadhabu kwa kadiri inavyowezekana maana hisia zile mtoto anazibeba.
Kulikuwa na kisa cha mama mmoja ambaye alipokuwa mjamzito mumewe alimtesa sana. Alikuwa anapatwa na huzuni na mara nyingine hasira sana. Alipozaliwa mtoto, maisha yakawa ya kawaida tu ila kadiri miaka ilivyokuwa ikisogea yule mtoto alikuwa na hasira na baba yake. Hakujua sababu ya zile hasira na mpk akawa kijana wa miaka kama ishirini hivi; akamnyatia baba yake huku akiwa na kisu na kutaka kumdhuru kwa kutokea mgongoni. Ilikuwa ni neema tu ya Mungu kuna mtu wa tatu akamuwahi kijana kabla ya kutekeleza azma yake.
Familia ilibidi ikatafute msaada wa kisaikolojia zaidi ili kupata ufumbuzi wa hiyo shida
 
Asante mkuu kwa nyongeza ...
 
Hivi kuongea na mtoto tumboni ni kweli anakusikia au Hollywood tu?
Inasaidia sana, anaanza kuzoea sauti yako tangu akiwa tumboni. Watu wanaelewa hii unaweza kufikiri ni vichaa, unamkuta mama mjamzito anaongea mwenyewe, "mama amechoka sasa anahitaji kupumzika", "Oh sweet that kick was a harsh one". Ukielewa unajua anajenga communication skills na mwanae.
 
Hamna kitu kigumu kwa kisasi cha sasa hivi kama kum control mtoto kwenye malezi

Wazazi wa dar ndiyo wanaoongoza kwa kuharibu malezi kwa watoto

Utamkuta mzazi yupo na mtoto wake wa kike kamvalisha mavazi ya hovyo hovyo, na ndiyo tatizo la watoto kuharibika wakiwa wadogo

Yaani malezi ziro
 
Mass media imeharibu sana watoto, watoto wa primary sikuhizi wanapaka make up, tena anaomba kabisa pesa akanunue lip gloss. Wakati tunakua tulipaka Vaseline midomoni, mzazi inabidi ujue kubalance kati ya kuwa strict na kuwa mzazi bora, lazima ulete udictator ukiona mambo yanazidi kuwa mabaya.
 
Nyakati hizi mtoto unamwachia mikononi kwa MWENYE ENZI MUNGU tu...mambo ni mengi duniani tena ni ya kutisha. .MOLA mwenyewe aliye mruhusu huyu kiumbe aje duniani ni yeye mwenyewe atanifundisha jinsi ya kumlea na atoe ulinzi wake wa hali ya juu kila huyo mtoto anapokwenda. .
 
Hiki ni kitu kingine, kama wazazi si watu wa ibada, mtoto anakua anamuona baba anarudi saa nane za usiku kila siku akiwa tungi, unategemea maji yataacha mkondo yapande mlima?
 
Mass media imeharibu sana watoto, watoto wa primary sikuhizi wanapaka make up, tena anaomba kabisa pesa akanunue lip gloss. Wakati tunakua tulipaka Vaseline midomoni, mzazi inabidi ujue kubalance kati ya kuwa strict na kuwa mzazi bora, lazima ulete udictator ukiona mambo yanazidi kuwa mabaya.
Ila sio udikteta uliovuka mipaka yaani udikteta uchwara
 
Back
Top Bottom