Tuzitafakar kwa makinii ghiliba za kisiasa za Sumaye!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuzitafakar kwa makinii ghiliba za kisiasa za Sumaye!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mystery, Oct 8, 2012.

 1. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,996
  Likes Received: 6,777
  Trophy Points: 280
  Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, aliongea na waandishi wa habari jana tarehe 7/9/2012. Jambo kubwa alilolizungumzia, ni namna alivyopigwa mweleka na Waziri wa nchi ofisi ya Rais [uwekezaji na uwezeshaji] Mary Nagu, katika uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa [NEC] wilayani Hanang'. Katika maelezo yake, alieleza moja kwa moja kuwa sababu kubwa iliyomwangusha kwenye uchaguzi huo ni rushwa iliyokithiri ambayo yeye mwenyewe ameiita ni ya mtandao, ambapo mtu mwenye mapesa yake ya kumwaga, anaweza hata kuwaingiza wajumbe anaowataka, hadi kufikia wilaya 80, kwa lengo la hao watu waje wamsaidie mbele ya safari, katika ukweaji wake katika ngazi za kisiasa!! Akaendelea kudai kuwa katika CCM ya sasa mgombea hachaguliwi kwa namna anavyotoa maelezo mazuri ya namna atakavyowatumikia wananchi bali anachaguliwa kutokana na uwezo wake wa kugawa pesa kwa wapiga kura!! Vile vile alieleza kuwa pamoja na mapungufu aliyoyaona kwenye uchaguzi huo, hatakata rufaa na hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote cha siasa cha upinzani, kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti. Na vile vile akaendelea kusisitiza kuwa yeye hana ugomvi wowote na mbunge wa jimbo la Monduli, Edward Lowasa, kama vinavyoripoti baadhi ya vyombo vya habari.Sasa hapa ndipo panapokuwa na maswali mengi yanayokosa majibu. Ameleza kuwa yupo mtu mwenye nguvu ya pesa, ambaye anaweza hata kununua wapiga kura wa wilaya hata zinzofikia 80 ili wachaguliwe watu, watakaokuwa kwenye mtandao wake, ili wakati muafaka utakapofika wamwezeshe kufikia kwenye malengo yake ya kisiasa. Kitendawili hiki hata ukimpa mtoto wa chekechea, jibu la moja kwa moja atakalokupa ni kuwa mtu huyo si mwingine bali ni Edward Lowasa!! Kwa maana hiyo wananchi wengi hatuelewi ni kwa nini Sumaye aliendelea kumsafisha Lowasa na kusema hana ugomvi naye, kwa maana hahusiki na maswahiba yaliyomkuta, badala yake angemchana LIVE na kututahadharisha watanzania kuwa tumwogope kama ukoma mtu wa aina hiyo anayesaka kuingia Ikulu, kwa udi na uvumba, hata kwa kutumia matrilioni ya mapesa, kama ambavyo Mwalimu Nyerere, alitutahadharisha wa-TZ, kwenye uchaguzi wa mwaka 1995. Kwa Sumaye kueleza kuwa hana ugomvi na Lowasa, ni ghiliba kubwa ya kisiasa, kwa kuwa inafahamika kwa kila mmoja wetu kuwa, pesa ya Lowasa ndiyo iliyombeba Mary Nagu, na wajumbe wengine wa NEC wa wilaya takribani 79 nyingine na hivyo kufanya jumla ya wajumbe wa NEC waliopita kwa matrilioni ya Lowasa, kuwa ni kutoka wilaya 80!! Wanajamvi wa JF tuutafakari kwa makini huu mwenendo wa siasa wa chama cha Magamba!!
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bado sijaona cha maana alichosema, siasa za bongo haziwezi awaachie akina lowassa, wameingia ccm wamemkuta na wataondoka watamuacha
   
 3. m

  malaka JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Laana ya usaliti!!
   
Loading...