kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,718
- 14,150
Majeshi yetu yako imara na yanasifiwa kimataifa kutokana na weledi wake lakini pia kutokana na uwezo wake wa kuweza kuchanganyika na raia wao. Hii inawarahisishia uharaka wa kupata habari njema na mbaya za adui.
Miaka yote raia huwa hawaogopi kupanda basi moja na askari wao na kupiga stori bila hofu yoyote. Hii ilituwezesha Tanzania kubaki kuwa kisiwa cha amani. Nadhani tuendelee na utamaduni wetu huu wa kuyaheshimu sana majeshi yetu bila ya kuyaogopa kupita kiasi, Rais Nyerere aliyafanya hivyo na matunda yake tumeyaona.