Tuweni makini:nimekuta nyoka ndani ya choo cha kukalia

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,958
​

Jamani tuweni makini na hivyo vyaa vya kisasa vya kukalia kabla ya kukimbilia kukaa na kujisaidia

jaribu kuchungulia ..mimi nimekutana na jinyoka kubwa sana aina ya Cobra ndani ya choo ona

picha hapo juu..nisinge chungulia kabla basi ------ yangu yangekuwa chakula cha nyoka....
 
Asante MziziMkavu kwa kunithibitishia wasiwasi wangu wa siku nyingi nilipomkuta chura kwenye libakuli la choo cha kukaa. Niliwaza kwamba kama chura anaweza kufika kwenye libakuli la choo, hata nyoka pia anaweza. Wazo hilo limenifanya kuwa mwangalifu sana niendapo chooni! Natezama mara mbilimbili ile sehemu yenye maji kama kuna kitu cha ziada zaidi ya maji kwa kuogopa kwamba upo uwezekano wa mdudu/mnyama usiyemtarajia kuwa pale!
Nitaongeza umakini sasa!
 
Last edited by a moderator:
haijawahi kusikika wala kutokea duniani si mijini kwenye vyoo vya kukaa wala porini ambako watu wanajisaidia kwenye majani nyoka kumng'ata binadamu maataakoo!kwa jinsi maataakoo yalivyoumbwa nyoka akiyaona tu yanamsogelea hutoka mbio yanamtisha

hivyo hakuna haja ya kuogopa kwenda kubwa we kaa tu nyoka kama yupo atakimbia ila kwa wanaume ukienda ndogo ukifungua na kunyooshea mashine kwenye choo kama nyoka yupo anaweza kudhani nyoka mwenzie hivyo anaweza kumrukia na kumjeruhi "nyoka" wako hivyo wanaume tuwe makini hapo
 
kifupi nyoka wengi kama si wote ni mahiri pia katika maji,kwenye vyoo vya kukaa nyoka huweza kuingia kupitia mfumo wa maji taka!na panya pia ni mahiri mno kupitia hapo,yeye hata ukimkimbiza sebuleni akiingia humo anatokea ndani kwa ndani mpaka ktk chamber!!
 
Asante MziziMkavu kwa kunithibitishia wasiwasi wangu wa siku nyingi nilipomkuta chura kwenye libakuli la choo cha kukaa. Niliwaza kwamba kama chura anaweza kufika kwenye libakuli la choo, hata nyoka pia anaweza. Wazo hilo limenifanya kuwa mwangalifu sana niendapo chooni! Natezama mara mbilimbili ile sehemu yenye maji kama kuna kitu cha ziada zaidi ya maji kwa kuogopa kwamba upo uwezekano wa mdudu/mnyama usiyemtarajia kuwa pale!
Nitaongeza umakini sasa!
mkuu hii nikawaida sana kwa sisi dereva guide wa maporini tunakutana sana na nyoka chooni,kuna sehemu inaitwa kisima ngedaa achaa asee nijambo la kawaida
 
Asante mkuu kwa tahadhari hii,hata mtoto wangu alinisimulia jinsi alivyopona na kugongwa na nyoka chooni shuleni kwao
sasa kupitia post yako napata mawazo kwamba kwa kuwa choo za ndani zina muunganiko na mazingira ya nje tena kwenye septic tanks ambako ndiko makao makuu ya wadudu,ni rahisi nyoka kufuata njia inayopeleka maji machafu na hatimaye kuingia ndani.Nimekusoma na nitachukua tahadhari.

Ila kwa kuangalia bichwa ya huyo nyoka anaonekana kama chatu vile hasa hiyo ya ndani ya choo,na hata hayo madoa doa.
 
​

Jamani tuweni makini na hivyo vyaa vya kisasa vya kukalia kabla ya kukimbilia kukaa na kujisaidia

jaribu kuchungulia ..mimi nimekutana na jinyoka kubwa sana aina ya Cobra ndani ya choo ona

picha hapo juu..nisinge chungulia kabla basi ------ yangu yangekuwa chakula cha nyoka....

Mungu eeeh epusha balaa hili. Siku moja niliona katika chaneli fulani ya kitafiti lakini sikuamini kwasababu inadaiwa nyoka alipanda kupitia kwenye mabomba mpaka akaja kuonekana kwenye choo cha ghorofa ya kumi. Kumbe kweli naanza kuamini. Mshukhuru Mungu ndugu yangu.
 
uwiiiii nmeogopaje!!!!! Aiseeee!!!! Me kabla na baada ya kujisaidia nnatabia ya kucheck na kuflush ! Nmezoea hivyo tuu kwa usafi wa tamuu yangu ila naona sasa kumbe najilinda pia.
Em pata picha angeng'ata tamuu yako! Doct anashauri ikatwe kwa usalama wako!!
Uwiii
mshukuru Mungu
 
haijawahi kusikika wala kutokea duniani si mijini kwenye vyoo vya kukaa wala porini ambako watu wanajisaidia kwenye majani nyoka kumng'ata binadamu maataakoo!kwa jinsi maataakoo yalivyoumbwa nyoka akiyaona tu yanamsogelea hutoka mbio yanamtisha

hivyo hakuna haja ya kuogopa kwenda kubwa we kaa tu nyoka kama yupo atakimbia ila kwa wanaume ukienda ndogo ukifungua na kunyooshea mashine kwenye choo kama nyoka yupo anaweza kudhani nyoka mwenzie hivyo anaweza kumrukia na kumjeruhi "nyoka" wako hivyo wanaume tuwe makini hapo
Umenifurahisha sana Mc Tilly Chizenga! Yaani umbo la ------ ya binadamu ni tishio kwa nyoka!!! Ndo nimeisikia leo. Asante.
 
Last edited by a moderator:
pole mkuu, umenipa kazi ya kuwa makini kwa makazi ninayo ishi huku nje ya mji....
 
uwiiiii nmeogopaje!!!!! Aiseeee!!!! Me kabla na baada ya kujisaidia nnatabia ya kucheck na kuflush ! Nmezoea hivyo tuu kwa usafi wa tamuu yangu ila naona sasa kumbe najilinda pia.
Em pata picha angeng'ata tamuu yako! Doct anashauri ikatwe kwa usalama wako!!
Uwiii
mshukuru Mungu

Unaogopa kukatwa utamu teh teh teh teh
 
Wakina sie tunaopenda kwenda chooni usiku na giza bila kuwasha taa dah...Maana nikiwasha taa nahofia usingizi utakata!!
 
Back
Top Bottom