Tuweke historia ya madawati

Crocozilla

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
469
335
Nategemea kuja na mada ya kushawishi wananchi tushirikiane na serikali iliyopo madarani kuchangia katika utengenezaji wa madawati kupitia watu na vikundi mbalimbali. Mimi nakijta kwa watu binafsi na vikundi binafsi tu.

Kwa kuwa sasa tunaanza kuona maana na kulipa kodi nashawishika kujitoa kuchangia na kuhimiza wenzangu tufanye hivo.

Hata marekani na ulaya maendeleo katika sekta muhimu kama elimu yaliletwa kwa pamoja kati ya serikali na wananchi kushiriki mfano kujenga shule, vyuo, maktaba, ununuzi wa samani za shule na vyuo, vitabu na nyenzo nyingine.

Madhalani, kuna vikao vya harusi nimeona sehemu wamechangia madawati hata kama 2 tu huo ni mchango tosha na wanaweka historia yao kwa bi na bwana harusi milele. Ebu tuendelee hapo, vikundi vya mpira, wacheza bao, michezo yote kwa ujumla wake, umoja wa waendesha bodaboda, hata mama na baba lishe, umoja wa wafanya biashara fulani, koo fulani, umoja wa kabila fulani, wakazi wa mkoa fulani waishio sehemu fulani, mafundi fulani, mtu fulani, marafiki fulani nk nk

Naamini kwa umoja weru tunaweza. Tuweke historia. Inawezekana! Nitarudi baadae nikiwa kamili
 
Nakuunga mkono asilimia 100? baada ya mingo kadhaa, tunawainua watoto/ wajukuu wetu kutoka chini! Hongerah Mh. Magufuli tutakuunga mkono!
 
chukulia dawati moja linagharimu elf10, na madawati yanayotakiwa ni laki moja na elf60, ukijumlisha unapata 1,600,000,000.. nafikiri hii ni hela ya muda mfupi tu kwa serikali, wala haishindwi kuyatengeneza ila wameamua tu kutukamua wananchi
 
Inamaaana,serikali imekosa fedha,,,,ya madawat wakat tunalipa kod,,,,,, wameamua tu kutunyoa wananch
 
Back
Top Bottom