Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Siku zote mimi naamini moja kati ya sababu ya watu kuchanganyikiwa maishani ni kuwa na mategemeo makubwa juu ya kile walichoakiamini au walichoaminishwa kwa muda mrefu kwamba wanakistahili kukipata na siku ikifika wakakikosa basi hapo ndipo matatizo huanza, na sababu ni kwamba kile walichokiamini au aminishwa hakikuwa na uhalisia wowote ule, ni kwamba walidanganywa au kujidanganya!
Hivyo basi ninachotaka kusema ni kwamba sisi kama Watanzania tumekuwa tukiamini na kuaminishwa kwamba nchi yetu ni tajiri sana kuna wengine hata wanaamini kwamba nchi yetu ni moja kati ya nchi tajiri Duniani na hii ni kila kitu kuanzia, Madini, ardhi, Mito, Maziwa na Bahari, Mafuta na Gesi mpaka misitu na kuna wengine pia wengi tu wanaamini kwamba nchi yetu ndiyo yenye vivutio vizuri vya Utalii klk zote Duniani!
Sasa basi pmj na ukweli kwamba hivyo vitu tunavyo lkn nchi yetu siyo tajiri klk zote Duniani au hata hapa hapa Afrika tu, na vitu vyote tulivyonavyo wengine pia wanavyo, yaani hatuna upekee wowote ule kwenye haya mambo, hivyo tuache kujidanganya na tuache kuwa na mategemeo makubwa klk uhalisia kwani matokeo yake ni kuja kuwa na maisha yasiyo kuwa na furaha huko mbele!!
Hivyo ningependa WatanZania watambue hilo kwamba nchi yetu ina rasilimali nyingi lkn siyo kwamba tuna Rasilimali nyingi klk wengine hapana, kila nchi ina Rasilimali, hivyo tushushe mategemeo na matarajio yetu na turudi kwenye uhalisia, hii itatusaidia huko mbele kuishi maisha ya kuridhisha na yenye furaha!