Tuwe na Imani Imara, Tusiogope

Tuwe na Imani Imara, Tusiogope

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
111
Reaction score
214
Tuwe na Imani Imara, Tusiogope

Imani Ni nini

Katika imani za kidini, imani imara isiyokuwa na mashaka ni kitu cha lazima. Imani hafifu ni sawa na kuwa vuguvugu. Yaani, siyo baridi wala siyo moto. Kama Yesu Kristo alivyosema, katika Ufunnuo 3:15-16: "Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu".

Wakati Danieli yuko kwenye maombolezo ya siku 21 kuhusu vita vikubwa alivyofunuliwa, alitiwa moyo: Danieli 10:19: “Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu”.

Hofu ni mlango wa adui, ambapo ujasiri katika Neno la Mungu ni ufunguo wa mafanikio. Mwenye imani imara huongezewa nguvu na Mungu.

Hebu tuangalie mifano michache inayohuasiana na hofu au kutoogopa.

Kuna mistari ya kusimamia wakati wa hofu na mashaka, na vitisho vya adui na majaribu yake yote
yajapo. Simama nayo, na utauona wokovu wa Bwana.
Baadhi ya mistari hiyo imeoneshwa hapo chini.

Majaribu Mazito
Isaya 40:29
: “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo”.
Isaya 41:10: Israel kuhakikishiwa msaada wa Mungu: “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.

Kumtumikia Mungu
1Nyakati 28:20
: Mfalme alipoagizwa kujenga hekalu: “Kisha Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya Bwana”.
Matendo 18:9: Paulo alipokuwa Korintho kueneza injili, alipata wapinzani wengi. “Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, usiogope, bali nena, wala usinyamaze”.

Sauti ya Kifo
Waamuzi 6:23
: Malaika wa Bwana alipoonana na Gideon uso kwa uso: “Bwana akamwambia, Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa”.
2Samweli 12:9 "Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni.
13 “Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa”.

Kuogopa Kuhusu Uzao wa Tumbo Lako
Isaya 43:5
: Ahadi ya matengenezo na ulinzi: “Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi”.
Mwanzo 35:17: Raheli aliposhikwa na utungu wa kuzaa: “Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine”.
Mwanzo 21:17; Hajiiri na Ishmaeli walipoondoka kwa Ibrahim: “Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko”.

Ukiwa Peke Yako
Isaya 41:13
: Israel kuhakikishiwa msaada wa Mungu: “Kwa maana mimi, Bwana Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, usiogope; mimi nitakusaidia”.

Kuingia mji mwingine
Yoshua 1:9
: Agizo la Mungu kwa Yoshua: “Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na
moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Kumbukumbu 1:21: Waisraeli wakaribia kuingia Kanaan: “Tazama, Bwana, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike”.
Mwanzo 46: Yakobo alipohamia Misri na jamaa yake yote: 3 “Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. 4 Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako”.

Kupata Taarifa za Ghafla za Kuhuzunisha
Mithali 3:25
: usalama wa kweli: “usiogope hofu ya ghafla, wala uharibifu wa waovu utakapofika.
26 Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe”.

Majeshi ya Adui Yanapojipanga
2Wafalme 6:16
: jeshi la Shamu lilipotaka kupigana na jeshi la Israeli: “Akamjibu, usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao”.
Zaburi 27:3
: wimbo wa Mfalme Daudi “Jeshi lijapojipanga kupigana nami, moyo wangu hautaogopa, vita vijaponitokea”.

KWA HIYO, UKIWA NA IMANI IMARA, WALA USIOGOPE. MUNGU YUPO PAMOJA NAWE MUDA WOTE, KUKULINDA NA KUKUTIA MOYO KATIKA MAZINGIRA YO YOTE UTAKAYOKUWA NAYO.

KINACHOTAKIWA NI KUWA NA IMAMI, IMANI, NA IMANI IMARA KWA MUNGU.

IMANI IMARA MAANA YAKE NI KUSHIKA NENO LA MUNGU NA KULITEKELEZA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom