andrewmsumeno
Member
- Aug 20, 2014
- 17
- 0
Kwanza nawatakieni heri ya x mas wadau .Kisa kilichotokea Juzi ni cha kuogopesha ,nina msichana yupo hapa kwangu ,juzi narudi kitoka job nakuta milango ipo wazi nashtuka naanza kutafuta nyumba nzima haonekani najaribu kuuliza majirani hawajamuona ,huku ndani ameacha mtoto wa miaka 3 kalal. Hiyo ilikua kama saa 2 hivi tukatafuta pale mtaani mpaka saa 6 hivi ikabidi tulale ili kesho tulipoti polisi .Kesho yake nkalipot polisi mungu mkubwa nkakuta kuna binti kaokotwa huko mwenge Saa 8 usiku ,kumbuka mi naishi Makongo juu kumuangalia ni yule niliyekua namtafuta .Nashkuru mungu kwa kumpata pia mtoto wangu yuko yuko salama .Tulivyomhoji akasema alidanganywa na mtu kua atampeleka mahali pazuri zaidi ya pale ,hivyo alijaribu kutoroka but wakapotezana na yule mtu ndo akaokotwa na kupelekwa kituoni,na huyu binti ni mgeni jijini.Kwa kweli aliniharibia siku kabisa na maamuzi yangu kesho ni kumrudisha kijijini kwao Iringa .Angalizo jamani hawa mabinti wengine ni shida du