Tuwapuuze wanaotumia mitandao ya kijamii kuvichafua vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa.

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Wadau

Tanzania yetu ilijengwa kwa moyo wauzalendo mkubwa na waasisi wetu wawili Mwl Nyerere na Sheikh Karume rais wa kwanza wa Zanzibar. Kutokna na uzalendo wao waliijenga nchi yetu kwa misingi ya haki na kuheshimiana kwa kutumia mifumo ya vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama.

walivijenga vyombo hivyokwa ustadi mkubwa na wa hali ya juu hali iliyovifanya kuwa miongoni mwa vyombo vya usalama bora kabisa na imara duniani hali iliyovipelekea kuheshimika mpaka leo hat.

Leo Kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na vyombo hivyovya ulinzi na usalama, hakuna mtu yeyote au taifa lolote litakalothubu kutuchezea hata serikali ya Makaburu wa Afrika kusini kabla ya mzee Mandela wanalitambua hilo walijaribu kufanya vitimbi vingi lakini hawakufanikiwa.

Vyombo vyetu vya usalama vimefanikiwa kuilinda Tanzania yetu, kiasi ambacho nchi yetu imekuwa na amani pamoja na utulivu tofauti na nchi nyingine jirani zetu ambazo zimekuwa na machafuko ya mara kwa mara hata mpaka nchi hizo hizo kuwa kama shamba la bibi ambapo maadui wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kuwachonganisha raia wa nchi zao.

Lakini cha ajabu leo hii kuna watu wanaotumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii kuvishambulia vyombo vyetu hivyo hususani Usalama wa Taifa kwa kuwa tu, mgombea wake aliyekuwa akimtaka ameshindwa kwenye uchaguzi na vyombo vya ulinzi vilikuwa imara kwa kuthibiti hali yeyote mbaya ya kuleta machafuko nchini.

kikawaida Usalama wa Taifa huwa hawajibu shutuma zozote zinazowakabili, hivyo kupeleka watu hao wasio na nia njema na nchi yetu kutumia mwanya huo kukishambulia chombo hicho ambacho kinafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na vyombo vingine katika kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Kutokana na vyombo hivyo leo hii tunaweza kwenda popote ndani ya nchi yetu na kurudi bila bugudha yeyote, mmakonde anaweza kutoka Mtwara na Kwenda Mwanza na Mara na kufanya shughuli zake kisha akarudi kwa usalama na amani kabisa, pia anaweza hata kuhamia huko huko na kuendesha shughuli zake za kimaisha tofauti na nchi nyingine zilizotuzunguuka.

Pia hata wageni wamekuwa wakija na kwa shughuli mbali mbali pamoja na kufanya utalii ni kwa sababu tu ya amani tuliyonayo amabayo inalindwa na vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama.

Ndugu zangu tuwapuuzie wale wote wanaotumia majukwaa mbali mbali ikiwemo mitandao ya kijamii ili kuwachochea wananchi wavichukuie vyombo vyao vya ulinzi na Usalama. Tuuwaambie wazi wazi kuwa hatupo tayari kuchonganishwa na vyombo vyetu vya Usalama na tunaviamini kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya kwa kutulinda.
 
Unajua kuna wakati mtu anaweza asielewe hali ya utulivu na amani inayoendelea,na mipango ya kuhujumu nchi ambayo vitendawili vyake huteguliwa kabla ya kuleta madhara,hiyo ni kazi ya usalama,asiyejua maana haambiwi maana
 
Back
Top Bottom