Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,677
Ndani ya siku hizi mbili kumekuwa na taarifa za kufufuka kwa ndege ya ATCL aina ya DH-8 Q300 inayofanya safari zake toka Dar na Kigoma.Tofauti na matarajio ya wengi kuwa tutawapa moyo wahandisi wetu wazawa kwa kitendo hicho,hali imekuwa tofauti...watu wanakashifu na kuwavunja moyo hawa wataalanu wetu wachache waliobaki ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana kuirudisha ndege hii angani.
Hali ya kudhoofu kwa shirika la ATCL sio matokeo ya kitengo cha Ufundi(Line Maintanance and Hangar Maintanance) bali ni matokeo ya sera na maamuzi mabovu ya wanasiasa ambao mara nyingi wamekuwa wakaidi kusikiliza ushauri wa Wataalamu.Hata mwaka 2002 wakati Serikali ya awamu ta tatu ilipokuwa inabinafsisha ATCL kwa SOUTH AFRICA AIRWAYS Wataalamu wengi sana walipinga lkn wanasiasa hawakusikia,mpaka SAA(Mkaburu) alipofanikisha "kuliuwa" shirika letu na kuturudishia likiwa taabani wakati la kwake likiwa motomoto.
Wahandisi wa ATCL wanapaswa kupongezwa kwa kutumia utaalamu wao wa ndani tena katika Hangar(Gereji ya ndege) iliyo Tanzania kuifumua ndege yote,kuifanyia matengenezo na baada ya ukaguzi wa kitaalamu toka TCAA ndege imeweza kurudi angani.Hii si kazi ndogo,ni kazi kubwa sana na yenye utaalamu mkubwa,Serikali yetu ingekuwa na sera nzuri juu ya Usafiri wa Anga,Tanzania ingekuwa kitovu cha "Maintanance" kwa ndege za nchi nyingi za jirani maana tuna wataalamu waliobobea ambao ni matokeo ya sera "rafiki" za Mwalimu JK Nyerere juu ya usafiri wa anga.Imefikia wakati mpaka kupaka rangi ndege zetu na kuweka "Location Indicator na flight Registration number" tunapeleka Wilson Airport-Nairobi.
Wataalamu wa anga tulio nao ni wale wa kizazi cha Nyerere,baada ya hapo Serikali zilizofuata hazikujiibidisha kusomesha wataalamu kwa kada za urubani na uhandisi,ukitazama hata ndege ndogo za "General Aviation" zinazotumika na watalii kama "Charter na Schedule flights" marubani wake ni kutoka Kenya,Botswana,Afrika Kusini na nchi za Ulaya,Watanzania hawazidi wanne au watano ambao wapo hapo kwa nguvu za familia zao na baba zao kuwa sehemu ya marubani wa enzi za Nyerere.Itafikia kipindi hata ndege za mashirika binafsi ya ndani kama Precision na Fastjet kuanzia "Cabin Crews,Engineers & Pilots" ni wageni...haka kanchi mchawi gani kakarogaaaaaaaa!!!!!!Miaka hiyo kuanzia ndege za ATCL na zile za Serikali (TANZANIA GVT FLIGHT AGENCY) zilifanyiwa matengenezo hapa hapa ndani ya nchi na watu hawakushangaa,ila leo sbb watu wamezoea kupeleka nje ili wale "per diem" basi hata kazi ya uweledi iliyofanywa na wahandisi wetu tunaibeza.
Ikumbukwe Wahandisi hawa wana leseni za ufundi zinazotambuliwa kimataifa,hivyo kazi wanayoifanya inatambuliwa kimataifa,na mpaka ndege inaruhusiwa kuruka manake imekaguliwa kwa viwango vya kimataifa,tuache kubeza wataalamu wetu wa ndani bali tuwatie moyo,kudorora kwa ATCL sio kwa sabb ya wataalamu bali ni kwasbb ya Wanasiasa-Wafanyabiashara wenye maslahi katika usafiri wa anga,walioamua kuipeleka ATCL ICU ili mashirika yao binafsi yapate kufanya kazi.
Inafikia mahali hata Mashirika makubwa ya kimataifa ya ndege kama Etihad,Emirates,KLM,SwissAir,Oman Air,Qatar nk yanashindwa kupata "Station Engineers" Watanzania wanaoishi Dsm na wanalazimika kuajiri wageni kutoka kwao wakati wangeweza kumuweka "Line Maintanance Engineers" mzawa ili kupunguza ghalama,lkn kwa vile hakuna basi wageni wanajaa ktk nafasi ambazo zilipaswa kuwa za wazawa,ndio wazawa watapatikana wapi wakati "National Career" ambayo ni ATCL wanasiasa-wafanyabiashara waibadirisha na PW???Hatujaandaa kizazi kingine cha wataalamu katika sekta ya usafiri wa anga,tuna vijana wengi wenye vipaji..wenzetu Rwanda na Kenya wanawekeza kwa kasi kwa vijana wao katika usafiri wa anga,leo vijana wengi wadogo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati ktk utaalamu wa mambo ya anga wanatoka Rwanda na Kenya,sisi bado tunakimbizana na kuhakikisha kamati ya NISHATI NA MADINI anawekwa chini ya Mbunge wa chama dola wa Viti Maalumu na kamati ya PAC makamu wake ni mtu ambaye hata hesabu za kidato cha pili za Sequency and Series hakuzikokotoa.
Wakati huo ATCL ilichanja mbuga toka Dsm ya Mzizima mpaka Heathrow ya Malkia Elizabeth,tukachanja anga juu kwa juu mpaka Hungary..huko kote ulikuwa ukishuka ni lazima utaona nembo ya ATCL.Tuliazimisha wataalamu ktk nchi jirani kama Msumbiji,Zimbabwe na Namibia.Mwalimu alianzisha Chuo cha Usafari wa Anga (TANZANIA CIVIL AVIATION TRAINING CENTRE) mpaka leo Tunafundisha wataalamu kutoka nchi zote za kusini mwa Afrika,Kati,Mashariki mpaka Magaharibi ya Afrika katika mambo ya "Air Traffic Management,Aerodrome and Grounds Aid,Aviation Meteorology,Aeronautical Information Service and Aviation Security".....Tunafundisha watu wa Air Traffic Controllers kwa nchi nyingi za kimataifa..hii ni kazi ya JK Nyerere.
Tuwashukuru Wahandisi wetu kwa kurudisha DH-8 Q300,Welcome back ATCL "THE WING OF THE KILIMANJARO"....Now our Call Sign and Location Indicator will cross the winds and clouds of our beautiful Land......