TUWAIGE WAMAREKANI UDHAMINI LIGI KUU BARA USHINDANI UTAPUNGUA

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,693
MWANASPOTIAPP

Mashindano makubwa kuliko yote ya soka nchini, Ligi Kuu Bara, umeshaanza.
Mechi kadhaa zimeshachezwa tangu utepe ulipokatwa Jumatano, sasa ni mwendo wa mechi mpaka pale kitakapoeleweka nani anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.




Kuwapo kwa mdhamini kunasaidia kwa timu zisizokuwa na uwezo kuweza kutoa changamoto kwa timu kubwa. Mdhamini anaongeza ushindani na kuzifanya klabu hizo kuweza kuwa na haki sawa na nyingine zinazoonekana ni kubwa.




Lakini tofauti na misimu mingi iliyopita, ligi ya safari hii imeanza bila ya kuwa na mdhamini mkuu, hali ambayo kwa hakika si dalili njema kwa maendeleo ya ligi yenyewe na soka letu kwa jumla.




Hii ni kwa sababu kwa kiasi kikubwa klabu zetu zinategemea fedha za mdhamini wa ligi kwa ajili ya kusaidia uendeshaji na hasa ushiriki wa mashindano haya. Kampuni ya Simu ya Vodacom iliyokuwa ikidhamini ligi hiyo kwa miaka mitano, mkataba wake umemalizika.




Katika muda huo, kampuni hiyo ilikuwa ikichangia katika maeneo muhimu kupitia kiasi cha Sh2.6 bilioni ilichokuwa ikitoa kwa mwaka ambapo asilimia 57 ya fedha hizo zilienda kwa klabu kusaidia gharama za usafiri na mambo mengine.



Asilimia 16 ya fedha za udhamini zilikuwa zikilipia gharama za waamuzi. Japo wadau wengi nikiwamo mimi tulitamani posho za waamuzi ziongezeke kutokana na umuhimu na ugumu wa kazi hiyo ya kutafsiri sheria 17 za soka.




Ukiachana na gharama hizo, siku zote usimamizi wa michuano mikubwa katika mchezo wa soka kama hii Ligi Kuu Bara ambayo inahusisha timu kutoka mikoa zaidi ya tisa, na ukiangalia ukubwa wa nchi yetu, hapana shaka utaona uwepo wa gharama zisizoepukika katika usimamizi wa mechi.



Hapa namaanisha wasimamizi wa vituo, makamishna wa mechi na waamuzi ni lazima wasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa ajili ya kutimiza majukumu yao.



Ni kutokana na umuhimu huo, ndio maana asilimia 12.4 ya fedha za udhamini zilikuwa zikienda kwa waratibu ili kugharimia masuala ya kiutawala, ingawa nazo pia zilikuwa hazitoshi.




Kwa kuwa kila kitu huwa kinatokea kwa sababu maalumu, kukosekana kwa mdhamini mkuu hadi sasa kwenye ligi, kunapaswa kuchukuliwa kama ni moja kati ya hatua ambazo hata ligi kubwa barani Ulaya zilipitia kabla ya kufika hapa zilipo sasa.


Ni kutokana na hali hiyo, ndio maana tunaona Ligi Kuu Marekani (MLS) inakuwa na wadhamini watano kwa ajili ya kuonesha na kutangaza mechi za ligi hiyo.




Wadhamini hao ni makampuni yanayomiliki Vituo vya Televisheni za ESPN, FOX Sports, Univision, TSN na TVA Sports.
Kila kampuni hapo ina mechi zake tofauti na nyingine.

Hii imesaidia katika kufanya mechi zote kuwa na thamani, hata zile za timu ndogo pia zina thamani yake na zimelipiwa.



Nimetoa mfano huo wa Marekani jinsi walivyo na wadhamini watano katika eneo moja tu la kurusha matangazo, kwa sababu siku zote sisi binadamu hutakiwa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa.





Katika dunia ya sasa hakuna jambo jipya ambalo halijawahi kufanyika huko nyuma, kinachobadilika labda ya mfumo tu. Udhamini wa Ligi ya Soka ya Marekani, ni kati ya udhamini uliojikita katika maeneo ya msingi kiasi cha kusababisha klabu kutamani kuendelea na ligi hiyo.





Ni kwa sababu gharama zote za msingi katika uendeshaji wa ligi hiyo, zinalipwa na wadhamini.\ Kwa mfano, msimu uliomalizika wa 2017/2018, fedha za udhamini zilitoka katika kampuni zilizogawanyika katika maeneo makuu saba:- asilimia 10 ya udhamini ilitoka kampuni za chakula, asilimia 10 nyingine kutoka kampuni za kibenki, asilimia 10 ilitoka kampuni za usafiri wa ndege, asilimia 10 kutoka kampuni za madawa, asilimia 10 kutoka hospitali na zahanati kwa ajili ya matibabu.





Pia, asilimia nyingine 10 ilitoka kampuni za bima, asilimia nyingine kama hizo kutoka kampuni za mawasiliano ya simu za mkononi na asilimia 30 zilizobaki zilitoka kampuni zinazofanya biashara nyingine.
Ukiangalia mgawanyo huo wa kampuni zinazodhamini Ligi ya Marekani, utaona moja kwa moja kuwa gharama katika maeneo mengi kwa klabu imeshapunguzwa. Huu ni wakati wa kuangalia namna bora ya kuiga utaratibu wenye manufaa kwa ligi yetu. Yafaa sasa wapatikane washirika wa maendeleo wataokaosaidia kuziba mapengo ya gharama zilizopo katika ligi yetu ili kusaidia kuleta maendeleo tunayoota katika ndoto zetu kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom