Tuvute subira kwanza kuipongeza serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuvute subira kwanza kuipongeza serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Nov 25, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mramba,Yona na mafisadi wengine kweli wamepelekwa mahakamani lakini bado hawajahukumiwa. Hata hatufahamu hatima ya mali zao ambazo wamezipata kwa njia za kifisadi.Lakini wapo pia mafisadi wengine wengi ambao bado wako mtaani wanatanua huku wakitung'ong'a.Wengi tunawajua ingawa serikali hii ya ajabu inasema haiwajui ingawa ina vyombo vyote vya usalama.Sijui hata kitengo cha usalama kina kazi gani, nadhani kimepoteza maana kabisa.Kingevunjwa tu,kwa vile kinapoteza bure hela ya walalahoi.Katika hali hii tutafanya makosa kabisa kuanza kuipongeza serikali katika hatua hizi za awali kabisa.Ni vema tusubiri mpaka wale wote wenye tuhuma wafikishwe mahakamani,wahukumiwe na kufilisiwa.Hatuna shaka kabisa kwamba shutuma dhidi yao ni za kweli kabisa.Kipato chao cha halali kisingewafanya wawe matajiri wa kutupwa.Tunaisubiri serikali.
   
Loading...