Tuviachie vyombo vya usalama! Ooh sorry, vyombo vya dola

Tuviachie vyombo vya usalama! Ooh sorry, vyombo vya dola

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,727
Reaction score
11,952
Hii sio kauli mpya. Na kwa kumbukumbu zangu sikumbuki ni lini vyombo vinavyoitwa vya usalama vilitoa majibu panapotokea matukio ya uhalifu dhidi ya watu wanaokosoa serikali au wanaharakati wengine.

Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa porini ili afe, Dr. Steven Ulimboka.

Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la mauaji ya Dr. Senghondo Mvungi.

Tumeviachia vyombo vya usalama kutekwa na kuteswa kwa Absalom Kibanda.

Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la mauaji ya Prof. Mwakyusa

Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kumwagiwa tindikali Mh. Saed Kubenea

Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kupotea Ben Saanane

Tumeviachia vyombo vya usalama miili ya watu saba iliyokuwa kwenye mifuko, iliyotupwa mto Ruvu.

Tumeviachia vyombo vya usalama kumwagiwa tindikali wazungu kule Zanzibar

Tumeviachia vyombo vya usalama mauaji kwa kuchinjwa, Alphonse Mawazo

Tumeviachia vyombo vya usalama kulipuliwa mikutano ya Chadema kwa mabomu ya Arusha.

Tumeviachia vyombo vya usalama tukio la kulipuliwa kwa mabomu ofisi za IMMMA

Leo Lissu anapigwa risasi nyingi kwa lengo la kuuawa, kauli ni ileile! Tuviachie vyombo vya usalama.

Nikumbusheni ni matukio mangapi kati ya hayo hapo juu yaliyotolewa majibu na hivyo vinavyoitwa vyombo vya usalama!

Sijawahi kuona kitu kinachoitwa chombo cha usalama katika nchi yangu. Kuna vyombo vya dola! Kwa hiyo kauli rasmi iwe "TUVIACHIE VYOMBO VYA DOLA".

Maana yake ni kwamba tusitegemee kuwe na majibu yoyote ya kuridhisha kama dola ndio linahusika na matukio ya uhalifu. Chombo cha dola hakiwezi kukamata dola!

Kuna nchi zina vyombo vya usalama. Kwa mfano CIA ya Marekani. Ndio maana CIA wanaweza kumchunguza Rais wa nchi yao ya Marekani. Kwa sababu ni chombo cha usalama kwa ajili ya wamarekani. Hata pale CIA wanapotuhumiwa kufanya uhalifu, mara nyingi huwa kwa nchi zingine, sio Marekani.

Sisi huku tuna vyombo vya dola kwa ajili ya kulinda dola, sio vyombo vya usalama kwa ajili ya usalama wa taifa lote/raia wote. Tuna vyombo vya dola kwa ajili ya dola na watu wanaopendwa na dola, na wanoonekanekana kushabikia dola.

TUVIACHIE VYOMBO VYA DOLA kama tulivyoacha huko nyuma, na bahati nzuri watanzania ni watu wa kuacha.

Lakini ole wetu, wanyonge watakapochoka na kuamua kurudisha ngumi! OLE WETU.
-------------------------------------------------------------

Mr mkiki.
 
Asante kwa kurekebisha heading yako...
 
Naungana na wewe mtoa mkuu.

Ni mpumbafu pekee ndiye anayeamini kuwa nchi hii ina vyombo vya usalama.

Kwahiyo ukiamini nchi hii ina vyombo vya usalama wewe ni mpumbafu tu, hakuna jina lingine unaweza kuitwa. Wewe ni pumbafu tu.
 
"Toka lini ukamkamata na kumshtak mkeo kwa kukuzalia watoto" n Lema alisema haya. Africa kuna kitu knaitwa chama dola, hao ndo ujipa mamlaka makubwa yakufanya lolote hata kuua, kutesa n.k narudia kaul yako, "tuviachie vyombo vya dola" a.k.a "chama dola"
 
Policcm walisemaga zamani.
Vyombo vya dola, CCM imetuaribia nchi ni mpumbavu tu asiyefaham hili.
Magufuli amekuja kutuvuruga watanzania.
 
Tiss. The Highest Gang in the Nation of Tanzania. The Gang is well known as "Watu Wasiojulikana".

Tunaomba Tushirikiane Kupambana na hili kundi la Watu wasiojulikana.

Ushauri:
Naomba ukiona unafuatwa fuatwa na wasiojulikana jitahidi kuwaangamiza kwa uwezo wako.
 
Jeshi la police lipo kwaajili ya kurinda serekari Si kwahajiri ya wananchi
 
Tatizo ni hako kamkwara ulikomaliza nako.siku ukichoka watu watakupumzisha wehemu salama basi.
 
Back
Top Bottom