jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,951
- 29,533
Kiukweli toka Magufuli aingie madarakani upinzani umeshindwa kupata hoja au ajenda ya kuisimamia yenye maslahi kwa umma wa Tanzania.
miaka ya 2006/7/8 wapinzani waliibua ajenda ya ufisadi na ukwepaji kodi kwa makampuni ya madini.
Ajenda hii ya ufisadi ilikuwa endelevu na hatimaye wananchi wakaikubali na CCM ikashinikizwa kufanya yale iliyouafanya ili isife.
Ajenda hii isingeweza kufifishwa iwapo wapinzani wasingempokea yule mtuhumiwa mkuu wa ufisadi aliyetajwa na vinywa vya wanachadema.
Baada ya Magufuli kuingia Ikulu alihakikisha anaibeba ajenda hii ya ufisadi kama takwa la wananchi na hivyo kuwafanya wapinzani wakose ajenda kwani CCM imeamua kupambana na ufisadi na kwa bahati mbaya upinzani umebeba nasaba za ufisadi.
Hivyo kwa sasa wapinzani wako kwenye jitihada kubwa za kujaribu kupata na kuobua ajenda mpya itakayoendana na aina ya wanasiasa walionao.
Hili limekuwa ni jambo gumu sana na ndio maana tunajionea ukinzani na vituko bila hoja au ajenda inayoweza kubebwa na jamii.
Nchi hii ni changa sana kimaendeleo na hivyo kuna hoja nyingi au ajenda nyingi zinazoweza kuibuliwa na upinzani au hata wabunge wa CCM wenye hulka ya upinzani,ambazo zinaweza kupata muitikio mzuri wa jamii na pia zikasaidia kuendeleza nchi.
Sioni ni sababu gani hasa inayowafanya wapinzani kutojaribu kupitia ilani ya CCM na kuona maeneo yenye mapungufu katika ilani hiyo na kuandaa hoja au ajenda kinzani dhidi ya ilani hii.
Siwasikii wapinzani wakikomalia maswala nyeti kwa mfano elimu bure kwa nini CCM iliahidi elimu bure hadi form four tu na sio hadi chup kikuu kama ilani ya Chadema ilivyotaka?
Siwaoni wapinza wakiishawishi serikali ije na elimu bure hadi chuo kwani wapinzani waliamini inawezekana badala yake nawaona wapinzani wakitetea mfumo wa elimu unaofanya watu wasio na uwezo kupata digrii na mikopo pasipo uhalali.
Siwaoni wapinzani wakiibeba hoja ya katiba ambayo waliitumia na kujipachika jina bila ridhaa ya wananchi..UKAWA.
Sijasikia hoja au ajenda ya wapinzano kuhusu mikataba ya gesi na mikataba mingine ambayo inalifilisi Taifa.
Siwaoni wakiandamana kudai mrabaha wa mapato ya gesi kuongezeka...!!
Nauona ipinzani kwa haiba ya chra anayerukaruka tu kwa maslahi yake ya kisiasa na sio Taifa...wapinzani wanafanya siasa ya uchaguzi tu nadala ya siasa ya kuboresha mambo.
Sioni uchangamfu wa siasa za wapinzani katika halmashauri ambazo wameshikilia ...sanasana nasikia fujo tu zisizo na maana kwa wananchi.
Sioni wapinzani wakiongelea mwenendo wa mambo ndani ya jumuiya ya EAC hasa ukizingatia yale tunayoyashuhudia kwenye EU.
Naandika waraka huu mfupi kwa uzalendo uliokithiri kwa nchi hii.
Naungana na Magufuli katika kukataza siasa ambazo zina mrengi wa kiuchaguzi nyakato hizi za kuendeleza nchi na kuovusha kutoka ilipo sasa.
Mh Rais angafanya siasa za kiuchaguzi muda huu basi hali ya nchi ingekuwa mbaya sana.
Tuungane na mheshimiwa Rais katika kukataa siasa za kimrengo wa kiuchaguzichaguzi na badala yake tujikite kwenye siasa safi za kimaendeleo...tuanzishe ajenda zenye mantiki na muelekeo wa kuiendeleza nchi.
Hebu tujaribu kuwafikirisha waandishi na wananchi katika kuifanya Tanzania mpya na endelevu kimataifa ...
Tuwasaidie wapinzano kupandisha ajenda ya kitaifa tuache siasa za kutafuta umaarufu wa kijinga.
HII NI KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!