Tuusaidie upinzani kupata hoja ya kujishikiza!

Sasa ulitaka uwaone wapinzani wapi wakati matangazo ya bunge hayarushwi na mikutano yao hairuhusiwi. Kuna hoja unaweza kutoa ukidhani unawafanyia watawala kazi nzuri kumbe unawaharibia kabisa kwa kuibua mambo yanayochafua hali ya hewa ktk bongo za wananchi. Fikiria kwa post yako hiyo, umepika chuki kwa watu wangapi dhidi ya watawala!
Unamaanisha hoja za wapinzani ni lazima zipitie au kutokea bungeni?

Kuna social media mnazozitumia kurusha upuuzi au vituko kwa nini hamtumii?
 
Wal
Kiukweli toka Magufuli aingie madarakani upinzani umeshindwa kupata hoja au ajenda ya kuisimamia yenye maslahi kwa umma wa Tanzania.

miaka ya 2006/7/8 wapinzani waliibua ajenda ya ufisadi na ukwepaji kodi kwa makampuni ya madini.

Ajenda hii ya ufisadi ilikuwa endelevu na hatimaye wananchi wakaikubali na CCM ikashinikizwa kufanya yale iliyouafanya ili isife.

Ajenda hii isingeweza kufifishwa iwapo wapinzani wasingempokea yule mtuhumiwa mkuu wa ufisadi aliyetajwa na vinywa vya wanachadema.

Baada ya Magufuli kuingia Ikulu alihakikisha anaibeba ajenda hii ya ufisadi kama takwa la wananchi na hivyo kuwafanya wapinzani wakose ajenda kwani CCM imeamua kupambana na ufisadi na kwa bahati mbaya upinzani umebeba nasaba za ufisadi.

Hivyo kwa sasa wapinzani wako kwenye jitihada kubwa za kujaribu kupata na kuobua ajenda mpya itakayoendana na aina ya wanasiasa walionao.

Hili limekuwa ni jambo gumu sana na ndio maana tunajionea ukinzani na vituko bila hoja au ajenda inayoweza kubebwa na jamii.

Nchi hii ni changa sana kimaendeleo na hivyo kuna hoja nyingi au ajenda nyingi zinazoweza kuibuliwa na upinzani au hata wabunge wa CCM wenye hulka ya upinzani,ambazo zinaweza kupata muitikio mzuri wa jamii na pia zikasaidia kuendeleza nchi.

Sioni ni sababu gani hasa inayowafanya wapinzani kutojaribu kupitia ilani ya CCM na kuona maeneo yenye mapungufu katika ilani hiyo na kuandaa hoja au ajenda kinzani dhidi ya ilani hii.

Siwasikii wapinzani wakikomalia maswala nyeti kwa mfano elimu bure kwa nini CCM iliahidi elimu bure hadi form four tu na sio hadi chup kikuu kama ilani ya Chadema ilivyotaka?

Siwaoni wapinza wakiishawishi serikali ije na elimu bure hadi chuo kwani wapinzani waliamini inawezekana badala yake nawaona wapinzani wakitetea mfumo wa elimu unaofanya watu wasio na uwezo kupata digrii na mikopo pasipo uhalali.

Siwaoni wapinzani wakiibeba hoja ya katiba ambayo waliitumia na kujipachika jina bila ridhaa ya wananchi..UKAWA.

Sijasikia hoja au ajenda ya wapinzano kuhusu mikataba ya gesi na mikataba mingine ambayo inalifilisi Taifa.

Siwaoni wakiandamana kudai mrabaha wa mapato ya gesi kuongezeka...!!

Nauona ipinzani kwa haiba ya chra anayerukaruka tu kwa maslahi yake ya kisiasa na sio Taifa...wapinzani wanafanya siasa ya uchaguzi tu nadala ya siasa ya kuboresha mambo.

Sioni uchangamfu wa siasa za wapinzani katika halmashauri ambazo wameshikilia ...sanasana nasikia fujo tu zisizo na maana kwa wananchi.

Sioni wapinzani wakiongelea mwenendo wa mambo ndani ya jumuiya ya EAC hasa ukizingatia yale tunayoyashuhudia kwenye EU.

Naandika waraka huu mfupi kwa uzalendo uliokithiri kwa nchi hii.

Naungana na Magufuli katika kukataza siasa ambazo zina mrengi wa kiuchaguzi nyakato hizi za kuendeleza nchi na kuovusha kutoka ilipo sasa.

Mh Rais angafanya siasa za kiuchaguzi muda huu basi hali ya nchi ingekuwa mbaya sana.

Tuungane na mheshimiwa Rais katika kukataa siasa za kimrengo wa kiuchaguzichaguzi na badala yake tujikite kwenye siasa safi za kimaendeleo...tuanzishe ajenda zenye mantiki na muelekeo wa kuiendeleza nchi.

Hebu tujaribu kuwafikirisha waandishi na wananchi katika kuifanya Tanzania mpya na endelevu kimataifa ...

Watanzania tujifunze kuwabana wanasiasa kwa kile walichotahidi...tumpime na tumsumbue Magufuli kwa ahadi zake za kipindi cha uchaguzi.

HII NI KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
ivyomtoa Slaa kwa ujuaji wao kumbe kila mtu amepewa karama yake. Wamrudishe Slaa kama hawajapanda chati!
 
Wal

ivyomtoa Slaa kwa ujuaji wao kumbe kila mtu amepewa karama yake. Wamrudishe Slaa kama hawajapanda chati!
Kama Dr slaa anakipaji c mmsajili hapo Lumumba? eti ana karama , kwnn msimchukue awasaidie kuua upinzani? ...au ndo hasira za UDC mnazihamishia chadema?
 
Sasa ulitaka uwaone wapinzani wapi wakati matangazo ya bunge hayarushwi na mikutano yao hairuhusiwi. Kuna hoja unaweza kutoa ukidhani unawafanyia watawala kazi nzuri kumbe unawaharibia kabisa kwa kuibua mambo yanayochafua hali ya hewa ktk bongo za wananchi. Fikiria kwa post yako hiyo, umepika chuki kwa watu wangapi dhidi ya watawala!
Unamaanisha hoja za wapinzani ni lazima zipitie au kutokea bungeni?

Kuna social media mnazozitumia kurusha upuuzi au vituko kwa nini hamtumii?
 
Kama Dr slaa anakipaji c mmsajili hapo Lumumba? eti ana karama , kwnn msimchukue awasaidie kuua upinzani? ...au ndo hasira za UDC mnazihamishia chadema?
Usinichekeshe. UDC kwa level yangu ni Cheo kidogo saana! Wewe unachojua ni Lummumba na Ufipa Baasi. Wengine sisi ni Neutral what we want ni maendeleo baasi hayataletwa kwa kutoka Bungeni huku bado wananyemelea posho shame on them. Tusingekuwa na strong woman saa hizi wangekuwa wanaenda kulala na posho wanachukua. They have let us down kwa kweli!
 
Acha kujishebedua ww ...una Hadhi gani mpka uuone UDC ni level ndogo kwako? Au ndo sizitaki mbichi hz? vijana wa Lumumba mmepauka midomo kwa njaa Kali ,maana posho zimekuwa adimu kutoka b7 hadi 2500 tu ...
 
Pole sana kwa post hii nimegundua wewe ni level gani? Sasa ndio nikueleze sitaki sema mengi ila UDC kwangu mimi ni level ndogo sana. Sijasema UDC ni level ndogo naomba unielewe hapa najilingani sha na mimi kwangu ni level ndogo Umenielewa sijui!
 
Sijawahi kuona ukileta uzi fikirishi au wenye hoja,ni mwendelezo wa vioja kuwatumikia mabwana zako hao madikteta uchwara!
 
Pole sana kwa post hii nimegundua wewe ni level gani? Sasa ndio nikueleze sitaki sema mengi ila UDC kwangu mimi ni level ndogo sana. Sijasema UDC ni level ndogo naomba unielewe hapa najilingani sha na mimi kwangu ni level ndogo Umenielewa sijui!
Teh teh teh ...na mm nimegudua kuwa ww hustahili hiyo nafasi ...kifupi unastahili kuwa afisa mtendaji wa mtaa....
 
Teh teh teh ...na mm nimegudua kuwa ww hustahili hiyo nafasi ...kifupi unastahili kuwa afisa mtendaji wa mtaa....
Pole yako naona hicho Cheo Cha Afisa mtendaji wa Mtaa ndio umekiona Kikubwaaa saana kwako. Anyway sikulaumu alal in all Afisa mtendaji, DC, Rc wote hao ni watu muhimusaaana katika maendeleo ya nchi yetu hivyo hebu waache wafanye kazi wengine wenye professional zetu pia tufanye kazi husika. Cha muhimu kila mmoja kwenye nafasi yake afanye kazi ukiwemo wewe sio kukaa kulia lia hapa ukadhani maendeleo yanakuja kwa kulia lia!
 
Mtendaji Wa mtaa ndo size yako na si vinginevyo...
 
Mtendaji Wa mtaa ndo size yako na si vinginevyo...
Dah inaonekana hicho cheo unakipenda kweli maana hakikukauki mdomoni! Hongerah sana ila si haba kila mtu anafurahia kupanda hatua moja. Ila kumbuka hicho cheo ni cha muhimu sana Tanzania hii usidhani utafika huko na kuanza zungusha mikono! Mind you! Hii Serekali ni ya hapa kazi tu! Maana hamkawii kufika na kuazna kususa kuingia kazini kisa huelewani na bosi wako badala ya kujenga hoja!
 
Haya bhana mwana mvua ..ww si utakipata kwa kuzungusha kiuno?
 
Back
Top Bottom