Tuung'oe mfumo wote, ndio salama yetu kama taifa

Tuung'oe mfumo wote, ndio salama yetu kama taifa

HORSE POWER

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
2,328
Reaction score
1,666
Ndugu wanajf,habari zenu. Kwanza nawaomba mnikaribishe kwenye hili jukwaa letu ili tushirikiane katika kuelimishana na kuhabarishana. Nikija katika maudhui ya andiko langu,nimekua nikifuatlia mambo mengi yanayoendelea nchini mwetu,nimegundua kwamba watanzania wengi (sio wote) bado hasa hawajajua tatizo hasa la nchi yetu ni nini.

Wengi wameishia kulalama tu na kulaumu watu. Tatizo la msingi la nchi yetu ni MFUMO (sio mtu) MZIMA WA UTAWALA ulioasisiwa,kuatamiwa,kukuzwa na kukomazwa na chama hiki dhalimu cha CCM.

Na ninaposema mfumo wa utawala,namaanisha serikali,taasisi na mashirika ya umma,idara za serikali,mahakama na vikosi vya ulinzi na usalama n.k. Moja ya alama ya mfumo mbovu wa utawala ni kukithiri kwa WIZI (sio ufisadi),kukosekana kwa UWAJIBIKAJI na mambo ya kujuana. Tumesikia kashfa nyingi tu za wizi nchini lakini hakuna hatua za maana zinazochukuliwa kwa sababu ni wizi uliohusisha mfumo,sio mtu au kikundi cha watu.

Elimu yetu imekwishakufa sasa hivi watawala wetu wanaichimbia kaburi,shilingi yetu inshuka thamani na dola inapaa kwa kasi na watawala wetu wapo kimya,kilimo kimesahauliwa,kodi lukuki za kipuuzi kwa mlalahoi,kuawa kwa viwanda na hakuna juhudi za kuanzisha viwanda,mikataba ya maangamizi kwa umma,mauaji ya albino,polisi kuua raia,idara ya usalama wa taifa kuwa idara ya usalama wa watawala kubaki madarakani,umeme usio na uhakika n.k.

Hayo ni matokeo ya utawala mbovu,ulioshindwa,usiojali na usiowajibika. Nini kifanyike? Ndugu zangu,hakuna siku nchi hii itapata maendeleo stahiki ikiwa CCM itaendelea kuwa madarakani. Hakuna.

Ni utawala wa chama hiki dhalimu uliotufikisha katika hali hii mbaya ya kutangatanga nyikani. Bila ya kuking'oa chama hiki na kufumua mfumo wote nyang'au wa utawala uliopo na kuusuka upya,tutaendelea kuwa maskini na omba omba. Ni lazima kuwang'oa hawa watawala waliotusaliti na kuwa mawakala na mamluki wa ubeberu. Nasisitiza tena,tunalazimika KUUNG'OA MFUMO WOTE, SIO KUBADILISHA MTU.

Nawashangaa na kuwasikitikia wale wanaomshabikia huyo Maghufuli,sio atafanya nini cha maana kwenye mfumo huu nyang'au na ulioshindwa wa CCM. Tukajiandikishe kwa wingi,tukaifanye kazi hii OKTOBA. Nawasilisha!
 
Ili kuondokana na huu mkwamo wa kiuchumi, kisiasa na kijamii sharti kwanza tuking'oe hiki chama
 
Tuondoe mfumo wa magufuli na Lukuvi, tuweke mfumo wa Lowasa Karamagi, Tibaijuka na Rostam? acheni mzaha wa kijinga.
 
mfumo dhalimu wa maccm uondoke,Tunauondaje?Tuvuluge kwanza mizizi na ngome za ccm
 
hayo ndio mawazo yetu sisi kina gogo la shamba tunaunga mkono hoja mia kwa mia, na ndio maana ukifanikiwa kumteka adui yako unakuwa mwenye faida zaidi kuliko kumuua
 
Back
Top Bottom