Tuunganishe doti kuvamiwa kwa ofisi ya mawakili wa Manji na yeye kuachiliwa huru

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,657
1,992
Jamani kama mnakumbuka siku chache zilizopita ofisi za mawakili wa mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji zilivamiwa na nyaraka zote kuibiwa. Leo tunapata taarifa kuwa Manji aachiwa huru baada ya DPP kukosa ushahidi na kutoendelea na kesi.

Sasa tujiulize...

Je, hili suala ni coincidents tu au lilipangwa?

Kwa maoni yangu hili swala lilipangwa, Kivipi...

1; Ni kuwa baada ya upande wa Jamhuri kuona wazi kuwa hawana ushahidi wowote wenye nguvu dhidi ya Manji walianza kupanga jinsi ya kumuachia lakini uoga ulikuwa ni jinsi Manji atakavyo-react dhidi yao na hata kudai fidia kubwa.

Sasa mbinu ilikuwa kutafuta nyaraka muhimu za Manji ambazo kama Manji ataamua kuigeuka Serikali basi wazitumie tena kumshitaki.

Rejea mbinu zinazotumiwa na mkulu za kupata habari kama yeye mwenyewe anavyosema ya kutumia ujasusi wa kunasa mawasiliano, kufyonza habari na kuiba nyaraka muhimu.

Hii ina maana kuwa Manji hataongea lolote na akileta fyofyoko watammaliza kwa kutumia nyaraka walioziiba kwake.

Kwa wale wanaosubiri eti Manji ataongea au kudai chochote wasitegemee hilo.
 
mda ni mwalimu mzuri kila kitu kitakuwa wazi soon maana kila lifanyikialo gizani litakuja julikana tu mwanganj
 
CCM ni master plan!sio watu wenye roho ya kibinadamu kabsa wakiamua lao!
 
Back
Top Bottom