Tutorial assistant vs lecture kuna utofauti?

Mkuu TA ni ngazi ya kwanza kwenye kuajiriwa kama Mhadhiri. Huyu huwa na Shahada ya kwanza tu ya tasnia yake. Akipandishwa anakuwa Assistant Lecturer akiwa sasa na Shahada ya Uzamili/Umahiri. Akipata Shahada ya Uzamivu anakuwa Lecturer.

Kimsingi,Lecturer ni ngazi ya juu kuliko TA. Na hata elimu zao ni tofauti. Hivyo,mishahara ni tofauti pia.
 
naomba kujuzwa kuna utofauti kati ya TA(tutorial assistant) na lecturer mwenye idea please

tutorial assistant ni mkufunzi tu wa ngazi ya chini ambaye kamaliza shahada yake ya kwanza na huwa anafanya tu majukumu ya instructions kwa wanafunzi kwa maelekezo ya mhadhiri wa somo husika. lecturer ni mhadhiri halisi wa somo husika na huyu huwa ana elimu ya shahada ya uzamivu ( phd ) na yeye ndiyo mpango mzima kwa ufundishaji na kwa kukuongezea tu ulisahau pia kuuliza na huyu assistant lecturer kwani ngazi zao huko vyuoni huanzia na tutorial assistant kisha assistant lecturer na lecturer. huyo assistant lecturer huwa anafanya kazi za kufundisha pia na mara nyingi hufundisha wanafunzi wa kuanzia mwaka wa pili na watu humu vyuoni na hawa elimu zao huwa ni shahada ya pili au shahada ya uzamivu. nadhani nitakuwa nimekufumbua japo kidogo na ngoja niwaachie na wengine. nimependa sana spirit yako ya kuwa inquisitive na inaonekana utakuja kuwa academician mzuri sana huko baadae.
 

haya wasomi
 

nashukuru sana
 
Tutorial Assistant - Bachelor's degree

Assistant lecturer - Masters degree

Lecturer - Phd

Senior Lecturer - Phd + paper +research

Associate Professor - Phd +papers+research +mazaga kibao

Professor - Phd + papers +research +mazaga kibao +mazaga kibao zaidi

Natumai umeeleewa
 
Unaweza kuwa senior lecturer bila kuwa bila kuwa na PhD, but una masters na mzoefu kazini
 
Public universities nyingi za TZ unaweza kuwa lecturer (kutegemeana na research-based publications) hata kama huna PhD ila huwezi kupanda kuwa Senior lecturer bila PhD
 
Unaweza kuwa senior lecturer ukiwa na shahada ya uzamili ni suala la maandiko (papers)
 
Secrets unapanda na Master kuwa senior Ly lecture
 
hiyo ilikuwa zamani, sasa hivi kama huna PhD huwezi kuwa lecturer

Mbona ifm vijana wa bachelor wanafundishwa na walimu wenye bachelor na hao walimu wana bachelor wanajiita lecturers. Soma kitabu chao cha mwongozo na uone. Ifm bachelor hufundishwa na bachelor wenzao.
 
Mbona ifm vijana wa bachelor wanafundishwa na walimu wenye bachelor na hao walimu wana bachelor wanajiita lecturers. Soma kitabu chao cha mwongozo na uone. Ifm bachelor hufundishwa na bachelor wenzao.

☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺
 
☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺

Mkuu toka umejiunga hii ndio post yako ya kwanza, unasoma ifm nini?
soma prospectus ya ifm uone alafu uulize mwl wa somo na uangalie kwenye prospectus utaona wenye bachelors ndio waalimu wa wanafunzi wa bachelor wanajiita lecturers.

Ifm ukiwa na masters wewe ni full lecturer. ni aibu na hatari kwa mstakabali wa elimu Tanzania.
 

Naanzaje kusoma IFM kwa mfano?😂😂😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…