Assalaam Alaykum,
Nataraji ndugu zangu, mpo salama na wenye furaha pamoja na familia zenu
Naomba niseme nililolikusudia
Yamebaki masiku machache,masiku ambauo,huenda yakatupa dira ya miaka 5 mbele. Dira hiyo huenda ikawa ni njema na yenye furaha au kinyume chake Muhimu kwasasa ni kila mtu kulingania amani ya Nche yetu. Amani inathamani katika jamii kuliko haki ya mtu mmoja mmoja.
Labda huenda ukastaajabu Kwann amani katika jamii ni bora zaidi kuliko haki ya mtu mmoja mmoja?
Jawabu fupi
Kuna wakati ni lazima mtu ajitoe mhanga kwa kupata maumivu makali,kwasababu ya Watu waliomzunguuka
Amani na Haki
Sehemu kubwa vinakaa pamoja,lkn kuna wakati huenda vikaachana kwasababu....
Tulinde amani zaidi,kwasababu ni sehemu ya kujipanga tena vzr katika kutetea haki yako
Tujifunze kuitafuta haki ndani ya amani
Na wala tusijifunze amani ndani ya haki
Vizazi vyetu
Vinahitaji amani,katika kuyaendea mambo mbalimbali
Basi,tusiwe wa mwanzo kuivunja amani kwa makelele ya Wachache na maslahi yao
Amani ni muhimu katika ustawi wa Jamii
Nawatakia siku njema