Tutegemee miaka mitano ya mwisho kuwa ni migumu zaidi

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,336
21,434
Amani iwe kwenu wana jamvi

Jamani tusipeane moyo wala kujidanganya kuwa miaka mitano ijayo ndio kutakuwa na pesa na mzunguuko wa kiuchumi kwa wananchi hilo tusahau ikiwa huu muhula wa kwanza hali ni mbaya mpaka inatisha,

Bajeti haitekelezeki katika mambo ya msingi na kama kuminya ndio kumeminywa yaani serikali inachukua mpaka ushuru wa mchicha sokoni na bado bajeti haikidhi na hakuna dalili ya mrejesho wa wananchi

Rais anataka kutimiza yote alioahidi kwenye kampeni na ikumbukwe mengine aliyatoa kichwani sio kwenye ilani,

labda tumkumbushe rais kuwa kazi zote hawezi kumaliza kwenye vipindi vyake vya uongozi kuna mwengine atakuja malizia mtu mwingine asiogope kukosa sifa mbona mengi ayafanyao ni awamu ya nne yeye hana hata moja ,

Labda ni ile barabara ya moroko na vile vitanda muhimbili

Natumaini hiyo miaka mitano ijayo anaweza rejesha hata kodi ya kichwa maana mapato yatakuwa haba na bajeti kama hivi ndio inabuma serikali haitaki kutafuta vyanzo vipya vya mapato
basi wekezeni kwenye kilimo mpate kuongeza mapato na kuondokana na hili wimbi kubwa la majobless,

Hilo ni gumu bajeti ya kilimo lazima inunue ndege kuwaonyesha waliosema siwezi

Weka mipango ya ndege utapata wapi pesa na vyanzo vyake
Sasa ndugu zanguni tutegemee hali ngumu zaidi ya ile ya baada ya vita ya kagera maana mkuu atataka kukamilisha kila kitu katika dakika za mwisho wa utawala wake wakati pesa ya ndani haitoshi na misaada pia haitoshi

tusubiri ada za shule kurudi kama kawaida!

Tanzania ipo kila fundi gonga anataka kutengeneza aina ya jiko lake

Ahsanteni!
 
ina maana inataka kuturudisha maisha ngapulila wacha niweke sawa seaman book yangu nitambae mapema kabla hilo balaa halijafika!
 
17972082_1486737891368540_8860078786586125181_o.jpg
 
Kama hukujenga au hukupata pesa enzi za kikwete.basi tarajia kufa au kuzeeka ukiwa kapuku wa kutupwa
La kujenga ni mipango kuna ambao hawakunga kipindi cha nyerere wakajenga kipindi cha mwinyi na wengine kipindi cha ben hawakujenga wamejenga kipindi cha kikwete na huyu atapita watu watakula tu
 
Back
Top Bottom