Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Nimesoma taarifa ya Tume ya Uchaguzi (NEC) kuwa imepokea mapendekezo ya jina la Mchungaji Getrude Rwakatare kuwa mrithi wa mama Sophia Simba kwenye ubunge viti maalumu na Tume imempitisha (kumteua) kushika nafasi hiyo.
Kwa kadri ya uelewa wangu mama Sophia Simba alikua mbunge kwa sababu ya uenyekiti wake UWT. So nilitarajia ambaye angerithi mikoba ya Sophia Simba UWT ndiye angependekezwa pia kuwa mbunge.
Jumuiya za wanawake kwa vyama vyote (CCM na upinzani) hutoa nafasi maal...umu kwa wenyeviti wa jumuiya hizo katika ubunge wa viti maalumu. Orodha ya mapendekezo ya wabunge wa viti maalumu ya CCM iliyoenda NEC mwaka 2015 jina la kwanza lilikua la mama Sophia Simba, kwa sababu alikuwa ndiye mwenyekiti wa akina mama wote wa CCM (by then). Hii ina maana kuwa kama CCM ingepata nafasi moja tu ya viti maalumu basi nafasi hiyo ingekuwa ya Sophia Simba. Huu ni utaratibu wa kawaida katika vyama vyote.
Hata orodha ya wabunge viti maalumu CHADEMA iliyoenda NEC mwaka 2015 jina la kwanza lilikua Mhe.Halima Mdee maana yeye ndiye mwenyekiti wa akina mama wote wa Chadema. Hii ina maana kwamba kama Halima asingegombea ubunge wa Kawe, halafu CHADEMA ikapata nafasi moja tu ya ubunge viti maalumu basi nafasi hiyo ingekuwa ya Halima.
Kwa mantiki hiyo basi, aliyepaswa kurithi mikoba ya Sophia Simba bungeni ni yule ambaye angerithi pia mikoba yake ya UWT.
CCM wafanyeje?
Kwanza CCM wakubali wamekosea kimkakati kupeleka jina la mrithi wa Sophia bungeni kabla ya kufanya uchaguzi wa UWT ambapo mwenyekiti ambaye angechaguliwa angekuwa mbunge (by default).
Kwa sasa CCM wanaweza kufanya yafuatayo:
1. Kumchagua mama Rwakatare kuwa Mwenyekiti wa UWT.
2. Kuhakikisha nafasi ya Uenyekiti wa UWT inarithiwa na mwanamama ambaye ni mbunge tayari.
3. Unless otherwise tutegemee kwa mara ya kwanza katika historia ya CCM Mwenyekiti wa UWT ambaye si mbunge.