Tutegemee Baraza jipya baada ya Muda

Tutegemee Baraza jipya baada ya Muda

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
38,560
Reaction score
48,906
Wakosoaji na wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanatuhumu kwamba Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Ndugu Rais lina mkono wa Chama na si mapendekezo yake.

Usahihi ama makosa ya hiyo kauli yanafahamika na Ndugu Rais mwenyewe na waliohusika katika mchakato mzima wa upatikanaji wa baraza lenyewe.

Tunachokiona tu wengine ni kushukuru kwa upatikanaji wake ambao utampunguzia mzigo mzito ndugu Rais wa kukimbia huku na kule.

Ila ukijaribu kuangalia kwa upande mwingine, utaona kwamba, Ndugu Rais anajiondoa na lawama za manazi na wakongwe katika chama kwa kutoa nafasi kwa walioteuliwa ili juhudi na uchapakazi wao ndio ziwahukumu wao na si iwe yeye aliyewahukumu kabla ya kupata nafasi.

Ni utendaji kazi pekee ndio utawabakiza au utawaondoa, katika nafasi zilizopo. Ingawa nia ya dhati kabisa ya kuja na sura mpya katika duru za siasa za nchi hii inaonekana, na hili litatimizwa.

Katika kipindi cha miaka miwili toka sasa, tarajia kuona sura mpya kabisa katika baraza na zilizojaa wachapakazi ambao watalipeleka Taifa hili katika hatua nyingine kabisa.

Sina haja ya kusema kwamba uteuzi ulikua wa fadhila kwa chama, hapana, bali ni hatua ya kwanza muhimu ya kuelekea kule Ndugu Rais anapopataka.

Nasubiri tukijaliwa, kuona hili baada ya miaka miwili.
 
Umenena vema braza! Jioni wapi maeneo tupige Nyagi kidogo.
 
Tofauti ya Magufuli na Jk ni kwenye kabila tu, zaidi ya hapo huwezi wa tofautisha alikopita jk na magu anapita mule mule, CCM ni ile ile na watu ni wale wale na matendo yao yaendelea Yale Yale
 
Tofauti ya Magufuli na Jk ni kwenye kabila tu, zaidi ya hapo huwezi wa tofautisha alikopita jk na magu anapita mule mule, CCM ni ile ile na watu ni wale wale na matendo yao yaendelea Yale Yale
Nina imani mabadiliko makubwa yatakuwepo with time,
 
Hakuna cha uchapa kazi kama hakuna hela, tra tukusanyieni hela tutapiga kazi, haki na wajibu
 
Nina imani mabadiliko makubwa yatakuwepo with time,
Hatuwezi kuishi kwa imani kuwa kesho itakua nzuri wakati tunaendeleza mfumo ule ule leo.

Magufuli hawezi kushindana na chama chake, iwe ni leo au hata hio kesho
 
Magufuli hawezi kwenda kinyume moja kwa moja na matakwa ya Chama chake
kweli nia anayo lakini kuitimiza kama anavo taka itakuwa vigumu sana.
 
Probation period ni miezi 6, tuvute subira, tuwape muda, leceiter city kabla, na baada ya ranieri ni tofauti, wachezaji ni wale wale.
 
Probation period ni miezi 6, tuvute subira, tuwape muda, leceiter city kabla, na baada ya ranieri ni tofauti, wachezaji ni wale wale.
Umenena mkuu, tuwape muda, na tumpe muda ndugu rais,
 
Naunga mkono hoja, Huo ndo ukweli wenyewe. Big up bro umeona mbali sana.
 
Hilo kwa Mwenye uelewa wa jicho la tatu halitamsumbia kuliona, hili Baraza ni la CCM na Magufuli ameteua tu, na you can easily see ile siku tangu tangazo la kuitwa waandishi wa habari na mda wa tukio Magufuli alionyesha kutokuwa na furaha kabisa na hata majibu ya maswali aliyoulizwa hakujibu kwa furaha na kiufasaha, hapo yaonyesha alilazimishwa na kauli yake ya atayefanya sherehe ajiandae kufukuzwa soon itaanza kufanya kazi, let's wait n see.
 
Back
Top Bottom