Tutazunguka wee lakini mwisho wa siku tutalazimika kukubali hoja ya kuunda Tume Huru ya uchunguzi

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,315
Iwapo ACASIA watashikilia msimamo wao wa kupinga findings za kamati kuhusu viwango vya madini vilivyoko katika mchanga wa dhahabu, nawaambieni mapema kuwa tutalazimika kurudia uchunguzi huu chini ya Tume Huru tutake tusitake.

Findings za hii kamati sidhani kama zinaweza kuwa na nguvu kisheria na pia kukubalika katika mahakama za kimataifa kwani kamati hii imeundwa na mlalamikaji na zaidi wajumbe wa kamati hii walikuwa ni kutoka upande mmoja tu unless upande wa pili ulishirikishwa kwenye kila hatua na kulikuwa na kusaini nyaraka kukubaliana na matokeo ya uchunguzi kwa kila hatua baina ya pande zote mbili.

Tofauti na hapo,sitashangaa iwapo msuluhishi(mahakama) ataagiza uchunguzi urudiwe upya chini ya msimamizi ataekubaliwa na pande zote mbili na kwa kutumia kamati itakayowashirikisha wajumbe kutoka pande zote mbili na hii itatokea tu iwapo hoja ya sisi kuibiwa itaonekana kuwa na mashiko mahakamani na pia wizi huu usitokane na mkataba na sheria zinazotawala biashara hii ambazo wote tuliridhia.

Ni mtazamo wangu pia kuwa hii kamati ilipaswa kushirikisha wajumbe wengine kutoka Taasisi za ndani na nje ambazo ni wadau/wataalamu katika huu uchunguzi na pia katika hii biashara ya madini ili kupia kamati ile sura ya kimataifa na zaidi kuingozea credibiliy.

Wangeweza pia hata kuwa-include wanasheria wa mahakama ya kimataifa ambayo inayotajwa katika mkataba wetu kama mashuhuda.

Yaani kuwe na mazingira ya ku-suggest ACASIA wanatuibia kwa kutoa viwango vya madini ambavyo ni tofauti na uhalisia lakini isiwe ni kutokana na mikataba na sheria zinazo-govern hii biashara.

Time will tell.
 
Hili jambo halitamalizwa na tume hii ya rais, ni lazima tutaishia mikononi mwa tume huru ambayo na Tanzania tutakuwa na watu wetu humo. Hii nani ataisikiliza wakati jambo lenyewe sio la kuishia Kisutu?!
 
Mpaka sasa sielewi ni kwanini walikosa busara kujumuisha wajumbe kutoka ACASIA na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ili kuipa kamati credebility.
 
Hivi hamuoni kuwa accacia wanaweza kulalamika na kutokuwa tayari kushiriki kwenye uchunguzi wa kitaalam kwa dhana/madai kuwa serikali imepandikiza madini kwenye mchanga ili ionekane kuwa mchanga unaosafirishwa unakuwa na kias kikubwa cha madini na kwamba hii imefanyika kipindi cha serikali kufungua makontena na kuchukua sample kwa ajili ya uchunguzi wao?? nadhan mistake kubwa imefanyika kufanya uchunguz bila kushirikisha upande wa pili.
 
Na hili lipo waz kiukwel hamna namna unaweza kuwabana hapa yote ya yote..kama kwel takwim nikwel wataruka futi 100 kule nakudai MAKANIKIA yamechakachuliwa
 
ww unawashwa na nn? tulia wanaume wafanye kazi. kwanza issue ya BOENG umeishia wapi?
Hata kina Lissu mliwabeza hivi hivi.

It is pity that in our country the intelligent people have only forums to express their ideas whereas the unintelligent ones have forums as well as power and mandate to implement their ideas.
 
Mpaka sasa sielewi ni kwanini walikosa busara kujumuisha wajumbe kutoka ACASIA na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ili kuipa kamati credebility.

Ni muendelezo wa ile habbit of not thinking things through. Jiulize walitaka kufanya nini na hii taarifa huku wakijua fika wanadeal na multilateral treaty
 
Mpaka sasa sielewi ni kwanini walikosa busara kujumuisha wajumbe kutoka ACASIA na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ili kuipa kamati credebility.
Makamera yaliwaponza!!
Wanapendaga shilawadu kiashiria cha kuijua akili ya mtu
 
Back
Top Bottom