Tutarajie kina Jairo wengine Bunge la Bajeti?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Dalili ya mvua ni mawingu wahenga walisema. Katika bunge la bajeti la mwaka jana lilishuhudia kutimia usemi usemao "za mwizi ni arobaini" baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Nishati na madini David Jairo kupatwa na hatia ya kuhonga baadhi ya wabunge ili kupitisha bajeti ya wizara yake.

Kabla watanzania hawajasahau ya Jairo, ni majuzi tu tumeshuhudia mbunge wa Bahi akifikishwa mahakamani kwa kosa la kupokea rushwa ili kupitisha bajeti ya halmashauri ya Mkuranga. Je, katika bunge la bajeti linaloanza vikao vyake June 12, 2012 tutarajie TAKUKURU ifanye kazi yake? au TAKUKURU itaendelea kuwalinda mafisadi as usual?

Kama TAKUKURU haiwezi kukamata wala rushwa wantanzania tuendelee kuishi kwa hisani za watu kama Betrice Shelukindo ili waibue tena Mawaziri na Wizara zao watakaobainika kuhonga ili bajeti zao zipite bungeni waendelee kununua majumba na magari ya kifahari.
 
Back
Top Bottom