Tutafakari kwa pamoja kuhusu sukari

Tutafakari kwa pamoja kuhusu sukari

mushi

Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
10
Reaction score
3
TUTAFAKARI PAMOJA KUHUSU SUKARI
tangu kuwepo kwa dunia hii, kumekuwepo au kupita kwa mifumo mbali mbali ya kiuchumi, kisiasa na kiutawala. lakini katika kupita huko kwa dunia katika vipindi mbalimbali dunia haikuwahi kulandana kabisa, namaanisha kwamba wakati jamii fulani ilipokuwa kwenye mfumo fulani, jamii nyinyingine ilikuwa katika mfumo mwingine ambao jamii hiyo nyingine labda ilishapitia kwenye mfumo huo au ingeupitia baada ya kumalizana na mfumo ulionao.
kwa mtindo huu wa maisha ya kidunia, kama MWANAHISTORIA makini si rahisi kupata shida ya kutambua jamii fulani ilipotoka, lipo na kwanini ipi hapo na baadae itaelekea wapi. fuatana nami utanielewa zaidi.

toka kuundwa kwa Dunia hii dunia imepata kushuhudia mifumo mikubwa kinzani miwili, mfumo wa kibepari na kijamaa
mfumo wa kibepari umekuwa ukijikita zaidi katika biashara huria (free trade), uchumi wa viwanda, uchumi usio na mipango maalum (unplaned economy) nk.....

kwa upande mwingine mfumo wa kijamaa umekuwa ukijikita katika uchumi unaosimamiwa na serikali (planned economy), usawa (equality), nk

kutokana na mifumo hii dunia imejikuta ikigawanyika hasa matatizo au mafanikio ya kiuchumi yanapotokea...... nikukumbushe juu ya "great economic depression" ambayo iliikumba dunia wakati huo na kusababisha dunia yote kuyumba kiuchumi kasoro tuu nchi zile zilizokuwa zikitumia mfumo wa kijamaa (socialism) hii ilitokana na hizi nchi za kibepari kutokuwa na "planned economy" hivyo watu kufanya biashara kiholela tuuu.....lakini nchi za kijamaa hazikudhurika kwani walikuwa na "planned economy"

baada ya utangulizi huo tuje sasa nchini kwetu..... nchi iliyoanza kujitawala kwa mfumo wa ujamaa na kupotea njia....ikaelekea wapi mimi sijui ila twende pamoja

toka raisi magufuli aingie madarakani amekuwa akipigana kuifanya nchi hii iwe nchi ya viwanda na kuwa nchi yenye uchumi wa kati.....je itawezekana?

Siku moja akiwa amealikwa kwenye KIGODA CHA MWALIMU raisi wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa aliulizwa swali lililokuwa kama la kebehi na lawama hivii.... "ni kwanini alibinafsisha viwanda vyote vya serikali na eti kwamba aliuwa uchumi wa nchi kwa kufanya hivyo.....majibu yalikuwa hivi.......baada ya yeye kuingia madarakani alirithi viwanda takribani 48 vya serikali na kuviendeleza.
katika viwanda hivyo kuanzia bodi zote za viwanda na wakurugenzi wake walikuwa watanzania lakini baada ya miaka zaidi ya mitano zaidi ya nusu ya viwanda vile vilikuwa kama sikufa basi vilikuwa kwenye hali mbaya ndio maana akaamua kuvibinafsisha ili angalau vifanye kazi kwa tija kuliko kufa kabisa

je alifanya kosa hapo?? ........ tutafakari sote
aliendelea mbele kuhoji kwamba uchumi bila viwanda hauwezi kukuwa hivyo ni vyema kuzuia bidhaa za nje zisiingie ndani ili viwanda vyetu vipate kuzalisha na kuuza kwenye soko la ndani na nje pia. swali likaja.
je watanzania tuko tayari kutumia bidhaa zisizo na ubora tukisubiri viwanda vyetu vikuwe kiubora????....... akatolea mfano:
je tupo tayari kuvaa kaniki kama miaka ya 1970????
haya tunayoyaona yanatokea ndio yaliyonifanya nimkumbuke raisi wa awamu ya tatu.... kwamba tuko tayari kuumia ilitupate mafanikio tunayoyataka????

hata mwaka haujafika tumeanza kulia eti bei ya sukari ipo juu kilo 3000...... kwa mtindo huu tutafika?????
kwa mtazamo wangu ni lazima tuumie ili tuyafikie maendeleo tunayoyataka.

namalizia na hili dogo: eti suala la kuwapangia wafanya biashara namna, wakati wakuuza bidhaa linafanywa na watu gani? wanaoamini kwenye ujamaa au wabepari?
hili nitaendelea nalo kwenye sehemu ya pili ya maandiko haya

IMEANDIKWA NA B MUSHI

"the history of man, is the history of his/her class struggle"
 
Hata hao mabepari wana utaratibu wa fair competition ktk biashara, siyo mtu afanye biashara yake kiholela tu.

Adhabu ya wanaokiuka utaratibu huo wa fair competition ni kali kuliko hii ya kwetu kwa hao tunaowaita wahujumu uchumi. Acha kukurupuka sheria itachukua mkondo wake.
 
Back
Top Bottom