Tutaboresheje elimu ya nchi yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaboresheje elimu ya nchi yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlangaja, Jan 30, 2011.

 1. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yameonesha kwamba baada ya mda si mrefu tutalizika kabisa taifa letu, kwani ni dhahiri elimu yetu inazidi kushuka kwa kasi ya ajabu. Inasikitisha sana, wanafunzi waliofaulu na wenye uwezo wa kujiunga na kidato cha tano ni asilimia 10.5 tu. Hii ina maana kwamba wanafunzi watakaoingia vyuo vikuu mwaka 2013 ni wanafunzi 40000 ambao ni sawa na wanafunzi watakaodahiliwa katika chuo kikuu cha Dodoma tu.
  Ndugu zanguni hebu tujadili ili tupate ufumbuzi wa suala hili. Taifa linazidi kudidimia. Binafisi nimeshangaa sana hili kutokea kwani, mwaka jana serikali imeongeza bajeti ya wizara ya elimu hadi kufikia asilima 18%. Tukisema shida ni fedha tutakuwa tunajidanganya. Mimi nimetafakari na kuona kwamba tatizo ni ufuatiliaji na kutokuwajibika. Hivi wakuu wa shule wanawajibika kwa nani? Je wakifelisha ni hatua gani wanachukuliwa?
  Mimi nilisoma katika shule moja ya kidini, haikuwa na walimu wa kutosha na kwa sababu hiyo tulikuwa tunaazima walimu kutoka shule ya jirani ya ambayo ni ya serikali. Walimu hao hawakuwa na mda wa kutosha madarasani kwetu, lakini kwa kutumia walimu hao hao tuliweza kufaulu vizuri sana na kuwa shule ya kwanza kimkoa katika masomo waliofundisha.
  Hivyo mimi nilijifunza kwamba tatizo la shule za serikali ni usimamizi mbovu, wakuu na walimu hawawajibiki . Mfano, unakuta shule haina ratiba ya wanafunzi ratiba ya wanafunzi kujisomea kabisa, wanaojisome ni wale wenye mwamko binafsi tu. Ikikumbukwa kwamba hawa ni vijana wadogo na hawaelewi elimu ni nini. Hii imetupelekea hapa tulipo.
  Jana kwenye kipindi cha tuongee asubuhi cha star tv, nilimsikia mjumbe mmoja alitoa wazo zuri sana ambalo nadhani likifanyiwa kazi litakuwa dawa ya ugonjwa huu. Mjumbe alisema kwamba nchi nyingi duniani baada ya kuona elimu inashuka serikali iliamua kuwapa wazazi kuponi ambazo ziliwawezesha kuwapeleka watoto wao shule ambazo walipenda. Hii inaanisha kwamba kila mzazi alimpeleka mtoto wake kwenye shule bora na zinazofundisha vizuri na kufaulisha wanafunzi. Kutokana na hali hiyo shule za serikali zilianza kukosa wanafunzi kabisa. Sekta binafsi ilifungua shule nyingi zaidi na hivyo wigo wa elimu ulipanuka zaidi. Kutokana na hali hiyo shule za serikali ilibidi zijifunge mkwiji ili kukabiliana na changamoto hiyo. Hii imepelekea elimu kupanda katika nchi hizo na sasa wanafurahia matunda ya elimu. Mfano wa nchi hizo ni marekani, Afghanistan, Afrika ya kusini na mataifa mengi ya ulaya.
  Wana JF mnaonaje mfumo huu? Mbona mfumo wa Vocha za kilimo umewezekana. Je vocha za Elimu zitashindikana?
  Naombeni mawazo yenu!
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuiboresha elimu yetu is simply next to impossible because the powerful want it that way.Fools are easier to rule!
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuwepo na serikali ya kikanda/kimkoa kwenye elimu peke yake...

  Kila mkuu wa mkoa apewe task ya kuhakikisha walimu, shule, na vifaa maalum vya shule vinapatikana katika shule mkoani kwake

  Regional resource must be mobilized to meet those ends..wizara inaongeza na coordiante hizo effort..
   
 4. E

  Emmanuel mwasha New Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu kwa Tz inashangaza. Hesabu za kuchagua ndio mbinu gani za kuwaboresha watoto wetu.
   
Loading...