Kiwalani finest
Senior Member
- Jul 6, 2024
- 116
- 85
TUJISOMEE, TUJUWE MIFUMO ILI TUNAPOJENGA HOJA ZIWE NI HOJA ZENYE MASHIKO
Ninakumbuka Tarehe 31/03/2025,
Profesa Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana,
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania,
Akiwa anaongea mbele ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Tukisoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu, ukurasa wa 425:
Mwisho wa kunukuu.
Tanzania ni nchi iliyochanganyikana,
Na watu wema,
Na pia watu wabaya.
Wote tunasomeka na kuitwa Watanzania.
Nchi hii ni yetu sote.
Askofu Dkt. Josephat Mathias Gwajima,
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Na vile vile Mbunge wa Jimbo la Kawe,
Tarehe 26/03/2025, alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Ili nchi iwe na amani na utulivu kwa kila mmoja wetu —
Awe mwenye utimamu wa akili,
Awe hana utimamu wa akili,
Wote hawa wanahitaji kupata amani na utulivu.
Hivyo, watu waadilifu na wasomi ndani ya nchi hukaa na kuandaa utaratibu wa kuleta amani na utulivu.
Hutengeneza sheria kuu iitwayo Katiba.
Kisha hutengeneza Kanuni, Miongozo na Taratibu, ambazo kimsingi hazipaswi kukiuka Maelekezo ya Maandiko Matakatifu.
Nchi huweka watu wa kusimamia maandiko hayo.
Watu hao huapa kwa Mwenyezi Mungu,
Wakiwa wameshika maandiko matakatifu kwa imani zao,
Ya kuwa hawatayaendea kinyume maandiko ya nchi.
Tafsiri sahihi hapa ni:
Watu wamekufuru kiasi kwamba,
Ni kama wanakuwa na baadhi ya viongozi wao wa kidini
Wakiwaandalia aya wazitakazo wao kwa nia ovu ya kuwacheza shere wananchi waliowachagua kuwa viongozi.
Hawajisikii kusoma maandiko yote kama yalivyo,
Kwa kuwa wakiruhusu, watakutana na tafsiri sahihi ya maneno “Unafiki” na “Ukafir.”
Profesa Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania,
Tarehe 30/03/2025, akiwa katika Busati la Masjid Mtoro, alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Katika nyakati tulizomo, zimejawa na watu wanafiki na makafiri waliobaki kujitamkisha jina la Mwenyezi Mungu huku wakifanya matendo ya wazi ya:
Kinyume na walivyoapa.
Haya yote yanatokea kwa sababu Watanzania hawajijui wala hawajipi muda kujifunza mifumo ya nchi yao,
Badala yake wanashabikia mpira kuliko mifumo.
Matokeo yake:
Huko ndiko kutenda haki —
Na wala si kusubiri miaka mitano kwa mtu aendelee kuonyesha Unafiki na Ukafir.
Zama tulizomo:
Baadhi ya viongozi hawafuati tena vitabu vya kimfumo.
Wanatumia hisia zao na machawa kuhalalisha maovu.
Wanaitumia dini kama burudani.
Mfano:
Tuwakatae.
Shekhe Muharram Rashid Mziwanda,
Tarehe 13/03/2025, akitoa darsa alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Shekhe Walid Alhad Omar Kawambwa,
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Tarehe 29/03/2025, alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Akiwa katika Baraza la Eid,
Tarehe 31/03/2025, alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Sasa, Mkuu wa Nchi keshatoa maelekezo.
Utu wetu tuuonyeshe kwa kuchukua hatua kwa haki na usawa.
Tujiepushe na kushangilia fukara anapoadhibiwa huku mhalifu mkubwa analindwa kwa rushwa.
Wakili Othman Masoud,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Ex Mwanasheria Mkuu,
Tarehe 02/04/2025, alisema:
Mwisho wa kunukuu.
TUSOME KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 1977, TOLEO 2005:
Tuitumie kwa uelewa na kusudi ili kuleta maana ya kweli ya Katiba.
Profesa Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana,
Akiwa katika Baraza la Eid, mbele ya Rais Samia alisema:
Mwisho wa kunukuu.
Nikashtuka katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni, nikiwa kimya kabisa bila ya kusema neno.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
— Mathias Mugerwa Kahinga
Ninakumbuka Tarehe 31/03/2025,
Profesa Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana,
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania,
Akiwa anaongea mbele ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema:
"Jambo la kufikiri ambalo Mungu ametuambia katika Qur’aan...
Ametuambia, na kila mara akituambia…
Mungu anataka tuzitumie vizuri zile akili zetu.
Mungu anasemaje!?
Hamtumii akili zenu ninyi katika kufikiri mambo!?
Hivi hamfikirii vizuri mukaingia ndani katika kufikiri!?
Katika jambo lolote, ukitaka kujifanya ni sharti ufikiri vizuri.
Ukitaka kufanya jambo, fikiri mwisho wake.
Je, ninyi mumefikiri vizuri!?"
Mwisho wa kunukuu.
Tukisoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu, ukurasa wa 425:
- Nchi maana yake ni sehemu ya ardhi isiyofunikwa na ardhi.
- Maana nyingine: Nchi ni sehemu ya ardhi iliyogawanyika kisiasa kwa mipaka na kutambulikana kwa taifa.
Mwisho wa kunukuu.
Tanzania ni nchi iliyochanganyikana,
Na watu wema,
Na pia watu wabaya.
Wote tunasomeka na kuitwa Watanzania.
Nchi hii ni yetu sote.
Askofu Dkt. Josephat Mathias Gwajima,
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Na vile vile Mbunge wa Jimbo la Kawe,
Tarehe 26/03/2025, alisema:
"Tunatakiwa Watanzania kuamka.
Hii nchi siyo mali ya mtu, ni nchi ya Watanzania wote.
Mtanzania, amka!
Mimi silali, kama unalala ni wewe."
Mwisho wa kunukuu.
Ili nchi iwe na amani na utulivu kwa kila mmoja wetu —
Awe mwenye utimamu wa akili,
Awe hana utimamu wa akili,
Wote hawa wanahitaji kupata amani na utulivu.
Hivyo, watu waadilifu na wasomi ndani ya nchi hukaa na kuandaa utaratibu wa kuleta amani na utulivu.
Hutengeneza sheria kuu iitwayo Katiba.
Kisha hutengeneza Kanuni, Miongozo na Taratibu, ambazo kimsingi hazipaswi kukiuka Maelekezo ya Maandiko Matakatifu.
Nchi huweka watu wa kusimamia maandiko hayo.
Watu hao huapa kwa Mwenyezi Mungu,
Wakiwa wameshika maandiko matakatifu kwa imani zao,
Ya kuwa hawatayaendea kinyume maandiko ya nchi.
Tafsiri sahihi hapa ni:
- Mtu anayeyaendea kinyume maandiko ya nchi,
- Anakuwa kwanza kamkosea Mwenyezi Mungu na Mitume wake.
- Pili, amewakosea Watanzania waliomuamini na kumpa dhamana ya kusimamia maandiko ya nchi.
- Anapoteza sifa za kuendelea kuifanya kazi hiyo,
- Na anakuwa amehitimu kuitwa Mnafiki na Kafir asiye na nidhamu kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake.
Watu wamekufuru kiasi kwamba,
Ni kama wanakuwa na baadhi ya viongozi wao wa kidini
Wakiwaandalia aya wazitakazo wao kwa nia ovu ya kuwacheza shere wananchi waliowachagua kuwa viongozi.
Hawajisikii kusoma maandiko yote kama yalivyo,
Kwa kuwa wakiruhusu, watakutana na tafsiri sahihi ya maneno “Unafiki” na “Ukafir.”
Profesa Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania,
Tarehe 30/03/2025, akiwa katika Busati la Masjid Mtoro, alisema:
"Kuficha jambo ambalo Mungu kaliteremsha ni ukafir."
Mwisho wa kunukuu.
Katika nyakati tulizomo, zimejawa na watu wanafiki na makafiri waliobaki kujitamkisha jina la Mwenyezi Mungu huku wakifanya matendo ya wazi ya:
- Ubaguzi
- Upendeleo
Kinyume na walivyoapa.
Haya yote yanatokea kwa sababu Watanzania hawajijui wala hawajipi muda kujifunza mifumo ya nchi yao,
Badala yake wanashabikia mpira kuliko mifumo.
Matokeo yake:
- Kumekuwepo na changamoto nyingi zitokanazo na ukosefu wa uelewa kuhusu mifumo.
- Kiongozi anapochaguliwa, siku hiyo hiyo huanza kufuatiliwa kama kweli anafuata Ilani, Katiba, Kanuni, Miongozo na Taratibu.
- Asipofuata, hata awe wiki moja kazini, anapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa maandiko ya kimfumo.
Huko ndiko kutenda haki —
Na wala si kusubiri miaka mitano kwa mtu aendelee kuonyesha Unafiki na Ukafir.
Zama tulizomo:
Baadhi ya viongozi hawafuati tena vitabu vya kimfumo.
Wanatumia hisia zao na machawa kuhalalisha maovu.
Wanaitumia dini kama burudani.
Mfano:
- Kiongozi anakataliwa na wananchi,
- Lakini kwa kutumia rushwa na machawa, anarudi tena kupewa uongozi.
- Wanauza ofisi za chama kinyume na sheria,
- Lakini bado wanalindwa na viongozi wa karibu na wale wa dini kwa unafiki.
- Hawa si viongozi wa haki. Ni wa hovyo.
Tuwakatae.
Shekhe Muharram Rashid Mziwanda,
Tarehe 13/03/2025, akitoa darsa alisema:
"Sisi tunaendekeza maisha ya dunia,
Tunasahau raha za akhera,
Ndiyo bora sana tena ndiyo zenye kudumu.
Waweza kuwa Mheshimiwa hapa duniani,
Ila siku ya Kiama ukawa dhariri katika madhariri."
Mwisho wa kunukuu.
Shekhe Walid Alhad Omar Kawambwa,
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Tarehe 29/03/2025, alisema:
"Tatizo siku hizi, mawaidha yamekuwa burudani.
Kama mwimbo hivi.
Mtu akisikia mawaidha, anasema:
Fulani anatoa mawaidha zaidi ya mwingine.
Kama vile tunaimba.
Raha ya mawaidha — Mungu atujaalie na sisi tutoe.
Mawaidha — ninyi yakiwafikia, mlie."
Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Akiwa katika Baraza la Eid,
Tarehe 31/03/2025, alisema:
"Chama chetu tunakuja na slogan isemayo:
Kazi na Utu.
Tusonge mbele."
Mwisho wa kunukuu.
Sasa, Mkuu wa Nchi keshatoa maelekezo.
Utu wetu tuuonyeshe kwa kuchukua hatua kwa haki na usawa.
Tujiepushe na kushangilia fukara anapoadhibiwa huku mhalifu mkubwa analindwa kwa rushwa.
Wakili Othman Masoud,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Ex Mwanasheria Mkuu,
Tarehe 02/04/2025, alisema:
"Wizi linaonekana kama vile si jambo kubwa.
Maana halisi ya wizi ni kutokufuata utaratibu tu.
Tumekupa biashara yetu utuendeshee,
Sasa tunataka hesabu.
Wewe (tuliyekupa biashara) hutaki tufanye hesabu."
Mwisho wa kunukuu.
TUSOME KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 1977, TOLEO 2005:
- Ibara 12(1)(2)
- Ibara 9 (a, b, f, na h)
- Ibara 13(1)(4)(5)
- Ibara 8(1) (a, b, c)
- Ibara 26(1)(2)
- Ibara 29(1)(2)
Tuitumie kwa uelewa na kusudi ili kuleta maana ya kweli ya Katiba.
Profesa Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana,
Akiwa katika Baraza la Eid, mbele ya Rais Samia alisema:
"Katika chaguzi zetu —
Iwe ni Diwani,
Iwe ni Wabunge,
Iwe ni Rais —
Angalia yule mtu ambaye unamuona atakufaa na atakayeweza kukusaidia.
Siyo kujichagulia-chagulia tuu.
Na unacheka-cheka tuu.
Mtu unaona hasemeki vizuri, ila tu kwa maneno ya kukuchombeza unakubali-kubali tuu.
Muislam anayejielewa hawi katika kitu cha namna hiyo."
Mwisho wa kunukuu.
Mtu mwenye akili, anaambiwa kidogo ila anaelewa sana.
Nikashtuka katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni, nikiwa kimya kabisa bila ya kusema neno.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
— Mathias Mugerwa Kahinga