Tusiwe wepesi wa kuhukumu

KICHINJIO 15

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
823
628
Habari zenu jaman!
Wikendi hii naomba tutafakari kisa hiki:

Kuna mwalimu wa shule ya sekondari alikuwa amezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji. Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni.

Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni kabla ya mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita yule mwanafunzi na kumsifia sana mbele ya darasa.

"Rose, simama. Darasa, Mpigieni makofi "Rose" kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia enhe"

Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka huyo "Rose" Yule mwanafunzi alimwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo. Mwalimu akamruhusu

"Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa. Nimelelewa na mama yangu tu. Simjui ndugu yeyote. Mama yangu alipokumbwa na maradhi alipelekwa hospitalini lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatuna pesa, hakuweza kupelekwa popote kwa vipimo zaidi."

Rose alifuta machozi yaliyoanza kutiririka mashavuni. Mwalimu jicho nyanya. Rose akaendelea

"Hivyo, nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba, kuchota maji, kumsafisha mama yangu, kumwandalia chakula chake kabla ya kuonda kuja shuleni na kazi zingine zote." Rose alinyamaza kidogo."

"Lakini leo nimewahi kwa sababu mama yangu alifariki wiki lililopita. Kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndo maana leo nimewahi shuleni."

Rose hakuweza kuongea tena. Taratibu akakaa kitini huku akilia kwa kwikwi

Darasa zima liligeuka mahala pa msiba.

WITO: Walimu wasiwe wanapenda kuwapa wanafunzi adhabu bila kuwapa nafasi ya kujieleza sababu za kufanya makosa hayo. Wakati mwingine watoto hao huhitaji watu wa kuwasikiliza kwa sababu kwao hawasikilizwi. Ukionyesha upendo huwa inasaidia kuwabadili kitabia (mbaya kwenda nzuri)
 
inatafakarisha sanaa.bahati mbaya tulio wengi tu napopata nafasi za ki malaka hua tuna jisahau sana,na kudhani kua tunajua mambo yote.ukweli ni kwamba maisha haya yana mambo mengi sana ambayo huwezi yatambua ukiwa mtu wa kukurupuka.asante ulie leta huu uzi hapa jukwaani
 
Ila ticha hana kosa ni mwanafunzi angempatia huo udhuru sidhan km angrchapwa na angeweza ht kusaidiwa na walimu.
My take:uoga wako ndo umaskini wko me sinaga siri eti nisiongee maãna unaweza kuongea ikAwa msaada mkubwa kwako.
Tuwe tunaongea matatizo yetu kukas kimya unachapw kila cku ndo nn ss
 
inatafakarisha sanaa.bahati mbaya tulio wengi tu napopata nafasi za ki malaka hua tuna jisahau sana,na kudhani kua tunajua mambo yote.ukweli ni kwamba maisha haya yana mambo mengi sana ambayo huwezi yatambua ukiwa mtu wa kukurupuka.asante ulie leta huu uzi hapa jukwaani
Asante pia mkuu.
 
Ila ticha hana kosa ni mwanafunzi angempatia huo udhuru sidhan km angrchapwa na angeweza ht kusaidiwa na walimu.
My take:uoga wako ndo umaskini wko me sinaga siri eti nisiongee maãna unaweza kuongea ikAwa msaada mkubwa kwako.
Tuwe tunaongea matatizo yetu kukas kimya unachapw kila cku ndo nn ss
Mkuu, kuna walimu ambao huwa hawawasikilizi kabisa wanafunzi wakikutwa na kosa. Wao wanaamini ktk adhabu kwanza maelezo baadaye. Sasa nijieleze nini wakati nimeshaadhibiwa?

Hii ipo hata kwa baadhi ya familia. Wazazi huweza kumwadhibu au kumhukumu mtoto kuwa hana adabu bila kujipa muda wa kujiuliza chanzo cha tabia/makosa hayo.
 
Duh nimemkumbuka Kitwanga kulewa bungeni na kufukuzwa kazi. Magufuli msikilize kwanza Kitwanga ujuwe kulikoni pengine Lugumi ndio kasababisha yote hayo.
Haahaaaa. Hapa kazi tu.
Yawezeka alikuwa stressed au alichotakiwa kuwasilisha kilikuwa kizito angekuwa soba.
 
Ila ticha hana kosa ni mwanafunzi angempatia huo udhuru sidhan km angrchapwa na angeweza ht kusaidiwa na walimu.
My take:uoga wako ndo umaskini wko me sinaga siri eti nisiongee maãna unaweza kuongea ikAwa msaada mkubwa kwako.
Tuwe tunaongea matatizo yetu kukas kimya unachapw kila cku ndo nn ss
Ni kweli mkuu. Mwanafunzi alipaswa kueleza matatizo yake mapema kwa walimu. Japo naamini hii habari hapa ni tamthilia lakini bado ina fundisho kwa wenye matatizo na pia wanaowabeza wenye matatizo.
 
Kuna video clip moja uwa inazunguka Whatsapp story yake inafanana sana na hii mada. Kuna mwanafunzi mmoja aliyekuwa akichelewa kila siku shuleni na kuadhibiwa na mwalimu wake kila mara.

Siku moja mwalimu wake akachukua pikipiki na kwenda kumfuatilia huyo mwanafunzi ili kujua kinachomsababisha achelewe kila siku. Akiwa njiani akamwona mwanafunzi yule, mama yake na kaka yake wako kando ya barabara porini huku mama yao akimvua sare yule mwanae mwingine na kumvalisha sare hiyo yule mwanafunzi aliyekuwa akifuatiliwa na mwalimu. Yule mwalimu hakuamini alichoshuhudia.

Kumbe yule mwanafunzi mchelewaji kutokana na umasikini wa nyumbani kwao, ilikuwa inambidi atumie sare moja na kaka yake. Hivyo alikuwa analazimika kumsubiri kaka yake atoke shule kisha wakutane sehemu na yeye kubadili mavazi yake na kuvaa sare ya kaka yake ndipo akimbie kwa mguu kwenda shule.

Ni story ya kugusa sana mioyo ya wengi wanaojali utu.
 
Wakumbuke walimu wako walikuwa na tabia kwa wanafunzi waliokuwa wanakutwa na makosa, hasa uchelewaji.
Yeye Rose kwa nini hakusema kwa nini anachelewa mpaka kasubiri mama afe?
Tusilaumu walimu kwa kuwa tunajua kutunga hadithi...
Walimu wametujenga sana na kutusaidia na adhabu ya viboko iendelee kuwapo...
 
Back
Top Bottom